tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
SIRI imefichuka, kwamba kiini cha mgogoro unaofukuta ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Mbeya, kinatajwa kuwa ni kuficha udanganyifu kwenye mkopo uliochukuliwa na Kanisa hilo, takribani miaka minane iliyopita.
Raia Mwema ilielezwa kuwa baadhi ya viongozi wa Dayosisi ya Konde, wanatuhumiwa kughushi nyaraka za Kanisa, ikiwamo mihutasari wa vikao vya Bodi kwa lengo la kuwezesha kutolewa mkopo huo (miaka 8 iliyopita).
Taarifa kutoka ndani ya Kanisa hilo zinasema, baadhi ya wakubwa ndani ya KKKT wameanzisha mgogoro katika Dayosisi ya Konde, ili kuficha udhaifu wa deni la takribani Sh bilioni 4.7 zinazodaiwa Kanisa na benki ya kibiashara ya CBA.
Benki ya CBA Commercial Bank of Africa-ilitoa kwa Kanisa Sh bilioni 1.7, kufadhili ujenzi wa ukumbi katika chuo kikuu cha Makumila, tawi la Mbeya, kilichoko Uyole (kilikufa kwa ubadhirifu), ambacho zamani kilitambulika kama Chuo cha Ualimu Uyole.
Hata hivyo, mkopo huo haukutumika kama ulivyopangwa, badala yake waliokuwa viongozi wa Kanisa, walizielekeza kwenye matumizi mengine binafsi ambayo hayakufahamika na Kanisa. Mpaka sasa, deni la Benki kwa KKKT, Dayosisi ya Konde limefikia Sh. bilioni 4.7 na tayari benki hiyo, imekwenda mahakamani na kupata amri ya kulipwa deni lake.
Mkopo huo, ulichukuliwa wakati Dayosisi ya Konde, ikiongozwa na Askofu Israel Mwakyolile (Msaidizi wake akiwa Mwakihaba aliyeteuliwa kuwa Askofu sasa), huku Mkuu wa KKKT, akiwa Askofu Dk. Alex Malasusa, ambaye alimaliza utumishi wake kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa hilo mwaka 2015.
Nyaraka ambazo gazeti Raia Mwema imezipata, zinaonesha kuwa Kanisa lilitumia majengo ya hoteli ya Matema Beach yaliyopo Ziwa Nyasa Kyela, kama dhamana ya kujipatia mkopo benki.
"Askofu Mwakyolile akishirikana na Mchungaji Mwakihaba walichota fedhia za mkopo, lakini ghafla Mwakihaba ameteuliwa na Askofu Shoo kuwa Askofu wa Konde katika mazingira ya kutatanisha," alieleza mmoja wa wachungaji wa Kanisa hilo
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kinachomponza Askofu Mwaikali, ni msimamo wake wa kugoma kusaini nyaraka za kuitoa hoteli ya Matema Beach kwa "wafanyabiashara wawili mashuhuri jijini Mbeya (wamiliki wa hoteli kubwa jijini Mbeya), ambao wamekubali kulipa deni la benki (nyongeza kwa ahadi ya kusimamia hoteli kwa miaka 100).
Benki ya CBA ilipeleka shauri mahakamani kulishitaki Kanisa. Wakati huo Malasusa aliishaondoka madarakani na Askofu Shoo Akakana kulijua hilo deni.
Kanisa likaunda Tume iliyoongozwa na Askofu wa Singida, Alinikisa Mkumbo, ikabaini 'madudu' yaliyomgusa Askofu Mwakyolile na kustaafu kabla ya wakati.
Askofu Shoo alishikilia msimamo, kuwa mkopo si wa Kanisa, lakini akaamua kuwaacha akina Mwakyolile kwa sababu binafsi, Hili linalotokea sasa, chanzo chake ni hicho"
Baraza la Maaskofu la KKKT, linatarajiwa kukutana Dodoma, Jumatatu ijayo ambako moja ya ajenda zinazotarajiwa kutawala, ni mgogoro ulioibuka kwenye Dayosisi ya Konde
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kanisa hilo, maaskofu karibu wote, wamekasirishwa na kitendo cha mkuu wao wa Kanisa, Askofu Dk Fredrick Shoo kuchochea mgogoro kwenye Dayosisi hiyo na makanisa mengine ya KKKT.
"Haya mambo yakiachwa hivi, kesho hawa watu wanaweza kutengeneza magenge na kuwang'oa maaskofu wasiowataka," alieleza Askofu mmoja wa KKKT, ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
Alisema, "tunakwenda Dodoma, tukiwa tunakumbuka madhila yaliyompata mwenzetu. Tunakwenda tukiwa wamoja na tunataka vitendo hivi vya kupinduana kinyemela vikomeshwe kwenye Kanisa letu.
Chanzo: Raia Mwema, Machi 26, 2022
NB
Kwanini Shoo kajiingiza kwenye mgogoro? Baadhi wanadai siku zote toka achaguliwe Askofu Mwaikali na baadhi ya maaskofu wasomi wamekuwa tishio kwa Askofu Shoo kuchukua nafasi yake.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
UPDATE 1 Jumatano, Machi 30, 2022
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
ASKOFU SHOO AIMEGA KONDE, AIGAWA KKKT
Taarifa kutoka Dodoma na Mbeya zinasema, tayari maaskofu kadhaa wa kanisa hilo, wanamtuhumu Askofu Shoo kuvuruga kanisa lao, kufuatia hatua yake ya kushindwa kuutatua mgogoro wa Konde.
"Tuko hapa Dodoma kuhudhuria mkutano wa baraza la maaskofu, lakini kwa hali inavyokwenda, hakuna namna ambayo kanisa linaweza kurudi pamoja," ameeleza mjumbe wa mkutano huo, ambaye hakupenda kutajwa jina.
Amesema, "hatua ya mkuu wa kanisa, kushindwa kuutatua mgogoro wa Dayosisi ya Konde, kumeifanya KKKT kugawanyika mapande mawili."
Raia Mwema limeelezwa kuwa kufuatia mgawanyiko huo, mkutano wa baraza la maaskofu ulioanza jana katika ukumbi wa St. Gaspard, jijini Dodoma, umehudhuriwa na maaskofu wawili - Askofu anayedaiwa kuondolewa kwenye wadhifa wake, Dk. Edward Mwaikali na Askofu Mteule, Mchungaji Godfrey Mwakihaba.
Bali, kiti cha Dayosisi ya Konde katika baraza kiliendelea kukaliwa na Askofu Dk. Mwaikali.
Taarifa ambazo gazeti hili imezipata zinasema, mara baada ya mkutano kufunguliwa, mmoja wa wajumbe, alimtaka Askofu Shoo, kulieleza jumuiko hilo, kilichosababisha kumng'oa katika kiti chake, Askofu Mwaikali, kinyume na katiba.
Alisema, hatua ya Askofu Shoo, imeligawa kanisa hilo na kulifanya kupoteza hadi yake mbele ya jamii.
Akijibu swali hilo, Askofu Dk. Shoo alisema, aliamua kuchukua hatua hiyo, baada ya kulazimishwa na Msajili wa Serikali kwa kile alichoita, "tishio la kufuta Dayosisi ya Konde."
Alipoelezwa ikiwa huo ndio msimamo wa serikali, haoni kwamba tishio la kuifuta Dayosisi ya Konde bado lingalipo na kwamba kwa sasa ni kubwa zaidi, kufuatia baadhi ya wachungaji na waamini kutopikika chungu kimoja, Askofu Dk. Shoo, hakuweza kujibu.
Lakini Raia Mwema lilipomuuliza Msajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Emmanuel Kihampa, kwamba ni sababu zipi zilizoifanya serikali kuingilia mambo ya ndani ya KKKT, haraka alisema, "hatuhusiki."
Alisema mgogoro huo haujafika mezani kwake, hivyo hayo yaliyotokea Konde, hayahusiani kabisa na ofisi yake. "Huo mgogoro haujafikishwa rasmi ofisini kwangu. Hivyo siwezi kueleza lolote kwa sasa," alieleza Kihamba, katika mahojiano na gazeti kwa njia ya simu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo, kuna uwezekano mdogo mno wa Dayosisi ya Konde, kurejea kama ilivyokuwa, kufuatia makundi mawili yanayogombana, kuchochewa na baadhi ya viongozi wao wakuu.
Baadhi ya wajumbe wenye msimamo wa wastani, taarifa zinasema, wanapendekeza ili kumaliza mgogoro huo, ni sharti kuigawanya Dayosisi ya Konde kwa kuanzisha Dayosisi mpya ya Tukuyu.
"Hawa watu hawawezi kubaki tena wamoja, hivyo njia pekee ya kulinusuru kabisa hapa lilipofikishwa na Askofu Shoo, ni kukubali kuanzisha Dayosisi mpya ya Tukuyu, kutoka Dayosisi ya Konde. Vinginevyo pale hapatakuwa na amani." Amesisitiza.
Katika hatua nyingine, habari kutoka St. Gaspard zinasema, Askofu mteule Mwakihaba ambaye aliteuliwa kushika wadhifa wa uaskofu wa Dayosisi ya Konde, katika mazingira ya kutatanisha, alivuliwa uchungaji Machi mwaka 2021, jambo ambalo linaiingiza kanisa la KKKT katika rekodi mpya.
"Hii nayo ni rekodi mpya katika kanisa letu, kwamba mtu ambaye aliwahi kuvuliwa uchungaji, leo ndio anakuwa mkuu wa Dayosisi. Tunakoelekea si kuzuri," ameeleza mchungaji mmoja wa KKKT.
Gazeti la Raia Mwema, JUMATANO, Machi 30 - Aprili 5, 2022 Ukurasa wa 4.