SIRI imefichuka, kwamba kiini cha mgogoro unaofukuta ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Mbeya, kinatajwa kuwa ni
kuficha udanganyifu kwenye mkopo uliochukuliwa na Kanisa hilo, takribani miaka minane iliyopita.
Raia Mwema ilielezwa kuwa
baadhi ya viongozi wa Dayosisi ya Konde, wanatuhumiwa kughushi nyaraka za Kanisa, ikiwamo mihutasari wa vikao vya Bodi kwa lengo la kuwezesha kutolewa mkopo huo (miaka 8 iliyopita).
Taarifa kutoka ndani ya Kanisa hilo zinasema,
baadhi ya wakubwa ndani ya KKKT wameanzisha mgogoro katika Dayosisi ya Konde, ili kuficha udhaifu wa deni la takribani Sh bilioni 4.7 zinazodaiwa Kanisa na benki ya kibiashara ya CBA.
Benki ya CBA Commercial Bank of Africa-ilitoa kwa Kanisa Sh bilioni 1.7, kufadhili ujenzi wa ukumbi katika chuo kikuu cha Makumila, tawi la Mbeya, kilichoko Uyole (
kilikufa kwa ubadhirifu), ambacho zamani kilitambulika kama Chuo cha Ualimu Uyole.
Hata hivyo,
mkopo huo haukutumika kama ulivyopangwa, badala yake waliokuwa viongozi wa Kanisa, walizielekeza kwenye matumizi mengine binafsi ambayo hayakufahamika na Kanisa. Mpaka sasa, deni la Benki kwa KKKT, Dayosisi ya Konde limefikia Sh. bilioni 4.7 na tayari benki hiyo, imekwenda mahakamani na kupata amri ya kulipwa deni lake.
Mkopo huo, ulichukuliwa wakati Dayosisi ya Konde, ikiongozwa na Askofu Israel Mwakyolile (Msaidizi wake akiwa Mwakihaba aliyeteuliwa kuwa Askofu sasa), huku Mkuu wa KKKT, akiwa Askofu Dk. Alex Malasusa, ambaye alimaliza utumishi wake kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa hilo mwaka 2015.
Nyaraka ambazo gazeti Raia Mwema imezipata, zinaonesha kuwa Kanisa lilitumia majengo ya hoteli ya Matema Beach yaliyopo Ziwa Nyasa Kyela, kama dhamana ya kujipatia mkopo benki.
"Askofu Mwakyolile akishirikana na Mchungaji Mwakihaba walichota fedhia za mkopo, lakini ghafla Mwakihaba ameteuliwa na Askofu Shoo kuwa Askofu wa Konde katika mazingira ya kutatanisha," alieleza mmoja wa wachungaji wa Kanisa hilo
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kinachomponza Askofu Mwaikali, ni msimamo wake wa kugoma kusaini nyaraka za kuitoa hoteli ya Matema Beach kwa "wafanyabiashara wawili mashuhuri jijini Mbeya (wamiliki wa hoteli kubwa jijini Mbeya), ambao wamekubali kulipa deni la benki (nyongeza kwa ahadi ya kusimamia hoteli kwa miaka 100).
Benki ya CBA ilipeleka shauri mahakamani kulishitaki Kanisa. Wakati huo Malasusa aliishaondoka madarakani na Askofu Shoo Akakana kulijua hilo deni.
Kanisa likaunda Tume iliyoongozwa na Askofu wa Singida, Alinikisa Mkumbo, ikabaini 'madudu' yaliyomgusa Askofu Mwakyolile na kustaafu kabla ya wakati.
Askofu Shoo alishikilia msimamo, kuwa mkopo si wa Kanisa, lakini akaamua kuwaacha akina Mwakyolile kwa sababu binafsi, Hili linalotokea sasa, chanzo chake ni hicho"
Baraza la Maaskofu la KKKT, linatarajiwa kukutana Dodoma, Jumatatu ijayo ambako moja ya ajenda zinazotarajiwa kutawala, ni mgogoro ulioibuka kwenye Dayosisi ya Konde
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kanisa hilo, maaskofu karibu wote, wamekasirishwa na kitendo cha mkuu wao wa Kanisa, Askofu Dk Fredrick Shoo kuchochea mgogoro kwenye Dayosisi hiyo na makanisa mengine ya KKKT.
"Haya mambo yakiachwa hivi, kesho hawa watu wanaweza kutengeneza magenge na kuwang'oa maaskofu wasiowataka," alieleza Askofu mmoja wa KKKT, ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
Alisema, "tunakwenda Dodoma, tukiwa tunakumbuka madhila yaliyompata mwenzetu. Tunakwenda tukiwa wamoja na tunataka vitendo hivi vya kupinduana kinyemela vikomeshwe kwenye Kanisa letu.
Chanzo: Raia Mwema, Machi 26, 2022
NB
Kwanini Shoo kajiingiza kwenye mgogoro? Baadhi wanadai siku zote toka achaguliwe Askofu Mwaikali na baadhi ya maaskofu wasomi wamekuwa tishio kwa Askofu Shoo kuchukua nafasi yake.
View attachment 2165336