Ni kitu gani kimekufanya u-conclude kuwa Dunia ni flat? Unaweza kuona only small portion ya Dunia then una-conclude Dunia yote ni flat, kwann usiseme labda ni rectangular au square?
Wewe pia hujawahi kuzunguka Dunia nzima ukafika kwenye Kingo za Dunia ukathibitisha uflat wa Dunia. Hakuna picha au video yoyote iliyowahi kupigwa either real au CGI (kama mnavyodai) ikionesha Dunia ni flat.
Kwa maelezo yako, Bado maswali yatabaki
1. Nini kimeshikilia Dunia
2. Nini kinafanya Jua na mwezi vizunguke? (Kama mnavyodai).
3. How come other planets and celestial bodies ziwe na sphere alafu ikija Kwa Dunia useme ni sahani?
4. How satellite zinaoperate kwenye flat earth conspiracy theory?
5. Moon phases na eclipses kwenye flat earth?
6. Flat earth believers mnatofautiana sana kwenye majibu yenu,
mfano: mnakataa gravity, mnasema ni bouyancy na density, lakni ww umekuja na majibu yako tena saivi maana mwanzoni ulisema ni density saivi unasema ni Kwa sabab hakuna mechanism ya kufanya vitu vipae😄😄 ilimradi tu ukwepeshe, Kwasababu ukihusisha tu bouyancy lazima uongelee gravity😄😄.
Fb = density ×gravity×volume.
View attachment 2926023
7. Majibu kuhusu Dunia kuwa sphere yamejibiwa na yamenyooka zaidi kuliko majibu ya flat earth,
mtu huwezi kuja kunijibu tu eti solar eclipse inatokea Kwa sababu Kuna vitu vina-block Jua na hivyo vitu huvijui na huwezi kuelezea ni Kwa namna Gani, inachekesha sana.
Just imagine majibu kama haya unayonipa👇👇
"Eclipses hazihusishi kabisa Dunia Kwasababu Dunia ipo stationary.... Kimsingi ni kwamba tukiwa Duniani tunachokiona ni effects za objects ambazo zinaogelea kwenye anga ku intercept due to the fact that zinapita kwenye njia moja hivyo kupelekea lunar &Sun Eclipses..."
Halafu compare na haya👇👇
View attachment 2926052
View attachment 2926055
kipi utakielewa hata kama ni wewe? Use common sense man.
Yaani watu wanatabiri occurance ya
lunar eclipse wewe unatoa majibu mepesi,
Mwaka huu itatokea marekani April 8, unadhani wanabahatisha? Au ni maigizo haya?
View attachment 2926094
Na kuhusu
moon phases Kwa upande wako huna maelezo yoyote, lakini embu angalia haya maelezo👇👇👇
View attachment 2926101
View attachment 2926132
Well explained kabisa👆👆
Kuhusu
gravity hiyo ipo wazi muda sana. Kuna applications nyingi tu za gravity
1.
Water supply designs:
Design zote za maji zinahusisha Moja Kwa Moja gravity. Flow ya maji kutoka kwenye tank inayohusisha gravity flow sio za kubuniwa Wala kubahatisha, they works. Ili maji yafike kwenye bomba lako Kwa pressure inayotakiwa gravity lazima ihusike Wala maji
hayapai.
h = density ×g.
Unadhani hizi calculations wanabahatisha?
View attachment 2926226
View attachment 2926227
2.
Gravity exploration: ambayo inatumika kwenye madini na ground water exploration. Au unadhani hizi ni hadithi? Wakati tunazi apply Kila siku na zina work out, sio simulizi kwangu nazi apply kabisa. Labda kama wewe unaona ni filamu za isidingo
View attachment 2926228
View attachment 2926229
3.
Trajectory motion pia inatumia gravity, you can't escape gravity kwenye calculations za projection.
Lakini pia kuhusu umbo la Dunia linadhihirishwa na uwepo wa vitu mbali mbali kama;
1.
Satellites, ambazo zina-revolve around the earth. Kwako inaweza kuwa hadithi lakini kwangu Mimi naviapply na vina work out japo hapa hata wewe una apply.
View attachment 2926243
2.
Gps, ambazo hutumika katika surveying tunazitumia sana,
pia Kuna hand Gps zina work Kwa maana ya Dunia kuwa sphere na inazungukwa na satellites.
And other telecommunication tools zina tumia same principle Kwa satellite.
View attachment 2926244
3.
Design software mbali mbali, kama Google earth, sewerGems, GIS zinatumia principle za kuwa Dunia ni duara hata location data tunazoingiza Kuna latitude na longtude na eastings na northings.
Mfano tu kwenye GIS Kuna World Geodetic System 1984 au
WGS 1984 datum tunayotumia kwenye GIS kama a
reference
ellipsoid, a standard coordinate system, altitude data, and a geoid.
We unadhani hizi zote ni mbwembwe au maigizo, be serious man.
4.
Energy generation: Gravity Ina contributes to renewable energy generation through hydropower, tidal power, and geothermal energy systems. Engineers hutumia gravitational forces ku-produce electricity from water, tides, na underground heat.
Au unadhani ni ngonjera hizi
View attachment 2926237
Sijui ni kipi unahitaji tena, hivi vyote haviwezi kuwepo Kwa bahati mbaya tu.