Kwanza wanakudanganya ili usiamini vitabu vitakatifu further more usiamini uwepo wa mwenyezimungu (huo ni mpango wa shetani kuwaweka waja mbali na mola muumba). Faida yao kwa duniani ni pesa tu ila after death ni majuto tu
Pili huko mwisho wa dunia kamwe huwezi jua kuna nini kwa sababu achilia mbali kujirusha, huwezi tu kujaribu kufika huko. Sababu ni barafu iliyopo huko! Barafu ya ulaya na marekani tu imewashinda ndiyo ije kuwa barafu ya huko ukingoni!
Tatu ujue kila kitu ni kwa kiwango. Kisicho na kiwango ni mola mwenyezimungu tu kwahiyo siyo lazima kila kitu mtu ajue wala siyo lazima kila kitu mtu ahoji. Kuna faida yoyote kwa muulizaji atakayoipata juu kuhoji huko? Kuna watu wamekufa hawaijui hata ndege! japo wameiona mara kadhaa kwa mbaaaali ikipita juu ya anga lakini hawakuwahi kupata wa kumuuliza hata kuhusu hiyo kitu. Je kufa kwao bila kuijia ndege unadhani ni makosa kwao?
Amesema mola aliiumba ardhi na mbingu vimeambatana (vimeshikana) kisha akaviambua (akaviachanisha) akaitandaza na kuumba vilivyomo ndani yake, kisha akasema ameumba jua na mwezi vyote vinajongea kwenye njia zao maalumu kwa muda maalumu uliowekwa. Vyote hivyo tunavitumia kwa ajili ya manufaa mbalimbali (yametajwa baadhi). Mwisho anasema basi tumwabudu yeye tu mola wa vyote hivyo na wala hajasema tutafute ukubwa wa jua/mwezi au dunia nk. Wala hajasema jua au mwezi vina umbo gani ila kasema tu vinajongea japo hazuiwi mwanadamu kutafiti mambo
uzuri ni kwamba binadamu wanafanikiwa kufanya tafiti nyingi kubwakubwa na za msingi. Ubaya ni kwamba matokeo ya tafiti nyingi hizo yanapitishwa kwenye chujio la the so called "MAMLAKA" ambapo kunaingizwa upotoshaji eidha kwa kuondoa baadhi ya yaliyokwemo au kuongeza baadhi ya yaliyokwemo au kuzuia kabisa isitangazwe tafiti yenyewe. Tena aliyehangaikia utafiti akishika msimamo juu ya kazi yake ndo kabisa hadumu. Sawa na mtaalamu/msomi anapoingia kwenye uongozi kuna vitu akitaka kuvihandle kitaalamu wanasiasa wanamzuia kwa maslahi ya siasa matokeo yake anaingia nayeye kuwa mwana siasa na akikomaa na misimamo yake ya kitaalamu...
Fuatilia huyo ARMSTRONG alisemaje baada ya tafiti zake huko angani na kilimpata nini? Fuatilia Keith Moore mtaalamu mwanaembriolojia aligundua nini kuhusu embryology na akaahidi nini na kikamkuta nini?
Kwenye Jibu lako la Kwanza,nakuomba pitia Video ya aliyesoma hiyo thread, utaona anazungumzia ishu ya kufichwa tusijue kama kuna Aliens .wengine mnasema tusijue kama mungu yupo, hapo ndipo mnapo jichanganya. (Angalia video kabla ya kubisha)
Pili kuhusu baridi,Marekani na Ulaya hakuna sehemu ambapo watu hawaiishi,,na sehemu zenye baridi kuliko zote duniani.
Google "Oymyakon" ipo Urusi (upande wa asia)...
Nje ya atmosphere baridi ni kali kuliko duniani lakini binadamu wameweza kufika,
Google na hilo kabla haujabisha...
Mkuu ,utafiti juu ya Solar SYSTEM ndiyo imesaidia katika.
-Uvumbuzi wa satelite na kujua katika umbali gani vikae, kwa kasi ipi vizunguke jua. Na matilio ipi inafaa kutengenezea vifaa vyake.
-Imesaidia kwenye uvumbuzi wa saa,na kuiweka iwe katika accuracy.
-Imesaidia katika ugunduzi wa kalenda tunayotumia. Maana hesabu ya Tarehe imezingatiwa kwenye mzunguko wa dunia.
Google uelewe why mwezi wa pili una siku 28 au 29.
Naomba unijibu swali langu huko mwisho wa dunia Gravity inafanyaje kazi.
Tumia hata reference za Sayansi (Usijetete kwa falsafa hapo)