Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?

  • Total voters
    710
Maji yapi yenye mlima! Ni haya yakimbiliayo bondeni, yenye tabia ya kuwa chini kiasi uka suggest kwa character hiyo yangemwagika kutoka kwenye tufe la dunia?
We pumba kweli!!!!
Hivi Wewe theory ya kuundwa kwa bara umesoma hata 1 Tuanzie hapo . Nisije kubishana na mtu ambaye uwezo wake ni madogo kutengeneza hoja na kusoma. Ebu taja theory moja tuichambuwe
 
Jibu lake rahisi sana dunia Kuna mabonde, milima, mitelemko kama Kuna bonde, mlima, miinuko na mitelemko katika utawezaje kuona zanzibar.
Alafu kitu kingine kuwa uwezo wa macho yetu kuona ndo inasababisha zanzibar isionekane. Mfano nzuri angalia Anga utaona Kuna blue lakin hakuna mawingu ya blue, blue tunayoiona angani Mwisho wa upeo wa macho yetu kuona. Ukipanda mlima kilimanjaro kwa kutumia macho yetu Mji wa Nairobi huwezi kuona lakin ukitumia vifaa maaluma Mji wa Nairobi unaona bila shida.

Mwanga wa blue ni mwanga wa jua sio mwisho wa macho kuona. Macho yetu yanaweza kuona nyota ambazo zipo thousands of light years away lakini hatuwezi kuiona Zanzibar? Hata ukisamama juu ya mlima Kilimanjaro na darubini huwezi kuiona misri lakini unaweza kuiona mars. Je misri ni mbali kuliko sayari ya mars?
 
Halafu hii theory yautambarare wa dunia inakuwakuwaje naweenae! inaingiaje akilini mwako mtoa mada? Ushasikia kuna angle ya dunia popote? Hembu angalia horrizon kwa jicho la uchi la bila kutumia hata kitabu. Mada zingine huwa mnazianzisha kwa kutumia mlango gani wa fahamu?
 
Muanzisha mada ni sakala!!!
 
Muanzisha mada ni sakala!!!
Yani na wewe unamuamini kabisa...
Nyota hutoa mwanga ndo maana tunaiona... sayari ya mars hutoa mwanga ndo maana tunaiona...

Zanzibar na misri zingekuwa bondeni au kilimani ungeziona kama zingekuwa znatoa mwanga wa taa zake usiku...
 
Kuna conspiracy nyingi sana kuhusu dunia yetu.
Kuna flat earth theory na pia kuna hollow earth theory.

Flat earth conspiracy ina uzito wake ambao unaweza ukaduwaa wanaamini kwanza milima yote tunayoiona ni miti mikubwa iliyokuwa zamani.
Wanaamini pia dunia haizunguki jua, bali jua na mwezi huizunguka dunia.
Wanaamini kuwa siku zote dunia inapaa kwenda juu (wakimaanisha gravity tuliyonayo inatokana na dunia kupaa juu to infinity)
Katika hivyo vichache huibua maswali mengi.....

Haya, na kuna hii conspiracy ya hollow earth. Ambayo huzungumzia kuwa katika poles za dunia yetu, yani south na north poles zina shimo ambalo huko kuna inner earth ambayo kuna viumbe huishi ambao wako very advanced wanaitwa AGATHA.
Kuna imani ya kibudha ambao wanaamini kuna sehemu ndani ya dunia ambayo huitwa SHAMBALA ambayo hufanania na story ambayo aliitoa pilot wa marekani miaka ya 1950s ambaye alipita karibu na North pole na kuona mazingira ambayo imani ya kibudha ya china huamini hivyo.
Pia kuna issue ya Ujerumani kufanya ziara katika bara la antrantica lililopo karibia na south pole kipind cha adolf hitler. Hii ilileta maswali mengi sana kukaribia vita kuu ya pili ambapo ujerumani ilionekana ilikuwa advanced katika silaha zake za vita na kuwa na technology kubwa sana. Wamepata wapi utaalamu huo??
Hivyo inasemekana mpaka leo south pole kuna basement ambayo ni gate la kwenda huko inner earth na bado ujeruman na mataifa mengine makubwa wanalinda maeneo hayo. Na inasemekana hata hitler alikimbilia huko na hakujiua kama tunavyoambiwa..

Guys kuna lots of informations ambazo zinaweza zikapeleka mbali na ukweli... kueni makini pindi mnatafuta ukweli.. Mungu awatangulie
 
Mwanga wa blue ni mwanga wa jua sio mwisho wa macho kuona. Macho yetu yanaweza kuona nyota ambazo zipo thousands of light years away lakini hatuwezi kuiona Zanzibar? Hata ukisamama juu ya mlima Kilimanjaro na darubini huwezi kuiona misri lakini unaweza kuiona mars. Je misri ni mbali kuliko sayari ya mars?
Kwa hiyo wewe unataka kuniambia nyota mchana tunaziona kwa macho yetu , wakati gani nyota zibaonekana kwa macho yetu, ni kipi kinachozuia mchana tusione nyota .
Nimemjibu mwezako kuwa kuna mabonde, milima, mitelemko na miinuko misri hatuwezi tukaiona na kubaliana na wewe kabisa . Hakuna kitu chochote kilichopo katika kinachozuia Mars isionekane.
Alafu kingine uliwahi kujiuliza kwa Nini baadhi ya wanyama wakati wa usiku macho yao yanang'aa, Binadamu tunaweza kujificha usiku pasipo macho yako kuonekana. Ingekuwa vizuri ungekuwa una juwa jicho la Binadamu linatoa volt ngapi?
Huu ni mstali Wako "" Mwanga wa blue ni mwanga wa jua sio mwisho wa macho kuona"" hivi unapoambiwa Mwisho wa uwezo Wako wa kuona unajuwa tunamaanisha Nini.
 
Halafu hii theory yautambarare wa dunia inakuwakuwaje naweenae! inaingiaje akilini mwako mtoa mada? Ushasikia kuna angle ya dunia popote? Hembu angalia horrizon kwa jicho la uchi la bila kutumia hata kitabu. Mada zingine huwa mnazianzisha kwa kutumia mlango gani wa fahamu?

labda atusaidie kwa hili ndugu; jua linapochomoza Mashariki na kuzama Magharibi, hili linawezekana vipi kama dunia ni tambarare? kwa maana tumeambiwa kuwa kuna ukingo!!! kama ndivyo, likienda halirudi linakuja jipya!
 
Kuna conspiracy nyingi sana kuhusu dunia yetu.
Kuna flat earth theory na pia kuna hollow earth theory.

Flat earth conspiracy ina uzito wake ambao unaweza ukaduwaa wanaamini kwanza milima yote tunayoiona ni miti mikubwa iliyokuwa zamani.
Wanaamini pia dunia haizunguki jua, bali jua na mwezi huizunguka dunia.
Wanaamini kuwa siku zote dunia inapaa kwenda juu (wakimaanisha gravity tuliyonayo inatokana na dunia kupaa juu to infinity)
Katika hivyo vichache huibua maswali mengi.....

Haya, na kuna hii conspiracy ya hollow earth. Ambayo huzungumzia kuwa katika poles za dunia yetu, yani south na north poles zina shimo ambalo huko kuna inner earth ambayo kuna viumbe huishi ambao wako very advanced wanaitwa AGATHA.
Kuna imani ya kibudha ambao wanaamini kuna sehemu ndani ya dunia ambayo huitwa SHAMBALA ambayo hufanania na story ambayo aliitoa pilot wa marekani miaka ya 1950s ambaye alipita karibu na North pole na kuona mazingira ambayo imani ya kibudha ya china huamini hivyo.
Pia kuna issue ya Ujerumani kufanya ziara katika bara la antrantica lililopo karibia na south pole kipind cha adolf hitler. Hii ilileta maswali mengi sana kukaribia vita kuu ya pili ambapo ujerumani ilionekana ilikuwa advanced katika silaha zake za vita na kuwa na technology kubwa sana. Wamepata wapi utaalamu huo??
Hivyo inasemekana mpaka leo south pole kuna basement ambayo ni gate la kwenda huko inner earth na bado ujeruman na mataifa mengine makubwa wanalinda maeneo hayo. Na inasemekana hata hitler alikimbilia huko na hakujiua kama tunavyoambiwa..

Guys kuna lots of informations ambazo zinaweza zikapeleka mbali na ukweli... kueni makini pindi mnatafuta ukweli.. Mungu awatangulie
Dah,dunia hii hii lakini mambo ni mazito Sana
 
Mada yako ipo kisayansi zaidi nami Naomba nikuulize kisayansi zaidi
Kama dunia iko flat na haizunguki inakuwaje jua likizamia magharibi lisichomozee huko huko badala yake linachomozea mashariki na kuzama magharibi,na mwezi je si ungekuwa ukionekana marekani Leo kuja kuonekana huku ni baada ya siku za kutosha?
 
Jibu lake rahisi sana dunia Kuna mabonde, milima, mitelemko kama Kuna bonde, mlima, miinuko na mitelemko katika utawezaje kuona zanzibar.
Alafu kitu kingine kuwa uwezo wa macho yetu kuona ndo inasababisha zanzibar isionekane. Mfano nzuri angalia Anga utaona Kuna blue lakin hakuna mawingu ya blue, blue tunayoiona angani Mwisho wa upeo wa macho yetu kuona. Ukipanda mlima kilimanjaro kwa kutumia macho yetu Mji wa Nairobi huwezi kuona lakin ukitumia vifaa maaluma Mji wa Nairobi unaona bila shida.
Sio jibu sahihi hata kidogo. Hata ukiwa na darubini kali ukiwa dar zenji huioni na hayo mabonde na milima huioni. Imewahi enda bichi hapa dar na kuiona boat toka zenji inavyotokea ikiwa inatoka zanzibar?? Inatokea kwa chini kama inaibuka. Zenji iko kwa "chini"!
 
Hii theory ndiyo ilikuwa inatumika miaka dahari kabla Galileo hajapingana nao kwa ushahidi ambao ulithibitisha madai yake kuwa dunia ni duara na ina umbo la tufe.
Sasa huyu jamaa anataka kuturudisha enzi zileeeee!!!!
Tuacheni jamani mvurugo wa ccm unatosha.
Hapa kueleweshana kwa njia ya maandishi itakuw ngumu, cz wengi bado hawajaipata logic hasa ya utambarare au uduara wa hyo dunia.

Kwa nielewavyo mimi, sifa za uduara zipo kote kote kati ya dunia mviringo na wanaoamini dunia tambarare.
Uduara wa Dunia tambarare ni wa kama sahani, disk, au mfuniko wa ndoo, na uduara wa dunia mviringo ndio huu ambao wote tunaujua, big ball.
Kwenye kueleweshan kwanza tusipingane juu ya uduara mana wote tunaongelea dunia ya duara ila katika utofauti wa maumbo.

Tangu mwanzo nasisitiza, mtoa post hajaoteshwa, ila elimu hyo ameitafutwa haifundishwi katika mitaala kama elimu ya dunia duara/mviringo ambayo wengi tunayo.
So ktk kupingana ni lazima wote tujifunze kwanza mtazamo wa wanaosema dunia ni tambarare bila hivyo, hamtapata uelewa nakubaki na uelewa wa kile mlichokuwa mnafundiswa tangu class mimi nikiwa ni mmoja wao.

Mtoa post source yake ni www.theflatearthsociety.org tembeleeni kwnza huku mjibiwe maswali yenu bila kujaribu kumuua mjumbe.
 
Sio jibu sahihi hata kidogo. Hata ukiwa na darubini kali ukiwa dar zenji huioni na hayo mabonde na milima huioni. Imewahi enda bichi hapa dar na kuiona boat toka zenji inavyotokea ikiwa inatoka zanzibar?? Inatokea kwa chini kama inaibuka. Zenji iko kwa "chini"!
Hawa jamaa masakala kweli!!!
 
Mkuu,nianze kusema tu kuwa nasikitika sana baada ya kusoma uzi huu kwa namna watu walivyochangia na wanavyochangia......

Mtoa mada amekuja na kuandika mambo mengi sana namna anavyosema juu ya umbo la dunia na ushahidi ameweka.Ameelezea kuwa yeye anaamini kuwa umbo la dunia ni flat,lakini akasema ni flat ya namna ipi anayoizungumzia.Shida ya kwanza ya watu inaanzia hapa...

Kuna watu wanapoona neno flat basi wanakimbilia kwenye fikra zao namna wanavyofikiria flat,wanafikiria flat kama ya meza tu,hapa ndipo panaponisikitisha kuliko mahala pengine popote pale.Mtoa mada ameelezea kuwa dunia ni flat duara yaani kama cd na michoro ameweka,watu wanakuja kujenga hoja kutoka na fikra za flat ya meza au umbo ambalo soyo duara kabisa.

Kwa kukuthibitishia hili angalia watu wanaojenga hoja kwa kuonesha kuwa mtu anaweza kutoka Dar hadi Sydney kisha akaenda Marekani kisha akarudi Accra na baadaye kurudi Dar.Ukiangalia hoja hii imelalia kwenye fikra za dunia isiyokuwa duara ya namna mleta mada aliyoizungumzia kwenye mada yake maana ukiangalia kwenye hoja za mtoa mada utaona kuwa mtoa mada naye anasema kuwa dunia ni duara lakini siyo mviringo kama tufe bali ni mviringo kama CD.Kwa mviringo huu unaweza kabisa kufanya safari hizo nilizotaja hapo juu bila kuhitajika kurudi nyuma.

Hoja ya watu kuzunguka dunia na kujikuta wamerudia pale pale,hoja hii nayo haishindikani kwenye hoja ya dunia duara ya kama sahani.Ukiangalia utaweza kuona kuwa inawezekana kabisa kuwa mtu akatoka Afrika ya kusini,akapitia Australia kisha akafika Amerika ya kusini kisha akarudi tena alipotoka maana atakuwa amezunguka duara inayosemwa na mtoa mada.Kwa maana hii bado hii haithibitishi kabisa kuwa dunia ni duara kwa maana ya tufe.....

Ameelezea mambo mengi sana pia,miongoni mwa mambo aliyozungumzia ni namna usiku na mchana unavyopatikana,watu hawasomi kabisa majibu na thread yote na unakuta mtu anakuja kurudia hoja ambazo zimeshajibiwa kwa uwazi kabisa na hili ni tatizo jingine,uviovu.Huwezi kujifunza mambo mazito kama haya huku ukiwa mvivu,huwezi na hutaweza kabisa kamwe......

Hoja nyingine ni route za ndege.Mtoa hoja amesema kuhusu hili,watu badala ya kujibu sababu ya ndege kutokuwa na rout hizi wameongeza swali kuwa vipi kuhusu ndege binafsi.Kwanza nafahamu kuwa kuna maswali ambayo ukiulizwa unaweza kuuliza aina fulani ya swali ambalo ukilijibu linaweza kukupa jibu la swali lako,lakini swali hili linaweza kujibu au kutokujibu swali kuu la mtoa mada kwasababu zifuatazo....

1;Hakuna uthibitisho ambao umetolewa hadi sasa wa uwepo wa ndege binafsi zinazokatiza north pole au south pole...

2;Kama kuna huo uwezekano wa ndege binasi kukatiza hapo,ni kwaninio ndege za kibiashara zisipite hapo ili kupunguza umbali mrefu? Kutoka South Afrika hadi Urusi kupitoa Siuth pole na kupitia katikati ya bara la Afrika hadi Geneva kisha Moscow wapi ni karibu?

Kimsingi hoja zote hizi ni mfu na zinaongeza maswali zaidi.Hakuna aliyejisumbua kujibu kuhusu ukweli wa binadamu kwenda mwezini.Hakuna ushahidi wa bibadamu kwenda mwezini....

Suala la meli kitoonekana kwa macho inapokuwa mbali ya macho yako hili mtoa mada amelijibu na ndiyo jibu bora kabisa linaloenezea suala hili.Watu walikuwa wanachukulia suala hili la meli kuzama kuwa ni moja ya ushahidi wa duara ya dunia,hii ikiwa na maana kuwa meli ile inakuwa imeshafika kwenye upande mwingine wa duara ya dunia.Mtoa mada amesema kuwa,kama inakuwa hivyo basi ukichukua kifaa maalum cha kuonea mbali usingeiona meli maana itakuwa iko kwenye upande mwingine wa duara ya dunia.

Mfano mzuri wa jambo hili ni kuchukua kijiti kifupi na ukakichoma kwenye chungwa kwenye upande mmoja kisha ukaligeuza chungwa lile upande mwingine kisha ukaanza kutazama,hutaweza kukiona kijiti kile kwakuwa kitakuwa kwenye upande ambao unazuiwa na muinuko wa chungwa lile hata kama utachukua kifaa cha kuonea mbali.Lakini ukichukua mti ukauchoma chini kwenye barabara iliyonyooka kisha ukaenda umbali wa kilomota 10 ukatazama mti ule hautauona bado lakini hii haimaanishi kuwa huuoni kwakuwa upo kwenye upande wa pili wa dunia bali ni kwasababu macho yako hayaoni tu,ukichukua kifaa utaweza kuuona mti huu.....

Kwa mfano huu ni dhahiri kuwa hoja za dunia duara bado zimegaragazwa kwenye mada hii,leteni nyingine......

Sisi tunajifunza na kuhoji pale ambapo tunaona kuna haja ya kufanya hivyo.......
Hapo kwenye meli na chungwa umejikanyaga sana. Unaongelea dunia kuwa flat ya cd alafu tena upande wa pili wa duara ambao unafanye meli isionekane??????!!!!! Hapa umechemka.
 
Mi kinachoniumiza kichwa ni hili la dunia kujizunguusha yenyewe kwenye muhimili wake "ROTATION" kwamba hiyo gravitation force ni hadi kwenye atmosphere? coz Kwa mfano ikitokea something labda ndege kikaganda hewani kwa maana ya atmosphere kwa masaa kadhaa kikitua chini c kitajikuta kipo America!!
 
Sio jibu sahihi hata kidogo. Hata ukiwa na darubini kali ukiwa dar zenji huioni na hayo mabonde na milima huioni. Imewahi enda bichi hapa dar na kuiona boat toka zenji inavyotokea ikiwa inatoka zanzibar?? Inatokea kwa chini kama inaibuka. Zenji iko kwa "chini"!
Kama unakubali kuwa boat inatokea kwa chini inapotoka zanzibar, sifa kubwa ya mabonde, milima, mitelemko na miinuko. Ninapo pandisha mlimani mimi siwezi kuonekana wote.
Hata mtu aliyeko zanzibar atakuambia kuwa dar Ipo kwa chini, sababu gani boat ukitokea dar inaelekea zanzibar inatokea kwa chini kama inaibuka.
Utata unazidi kuongezeka kila mtu yeyote aliyeko pwana katika nchi yeyote Ile kitu chochote kitakaho tokea baharin kinaibuka.
 
Back
Top Bottom