Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?

  • Total voters
    710
Ndiyo Dunia ni flat,...anga haina shape as it's intangible object,. Au hujui maana ya intangible ndugu yangu?

Kitu ambacho hakiwezi kushikika utasema kina shape gani?
Kitu ambacho hakiwezi kushikika na nini? Kila kitu kinaexist kwenye kitu. Mambo ya Infinity hayo.

Kwa concept yako ya kutokushikika, gesi inashikika? Gesi Ikiwa imejazwa kwenye chupa inakuwa na shape ya chupa na kushikiliwa na chupa au inakuwa haina shape sababu haishikiki kama unavyosema?
 
Direction ya Jua lilipo,
Kwenye Dunia Tufe,..ni Direction ipi napaswa kuelekea towards Jua ikiwa ni Saa 2:30 usiku Tanzania,... Assume Dunia ina umbo hili ➡️🌍

Jua ni sehemu ya anga au anga ni sehemu ya jua? Usisahau kwa anga kwako ni sehemu ya dunia na si dunia sehemu ya anga.
1. Jua lipo kwenye anga ya Dunia....
2. Jua ni sehemu ya anga ya Dunia.
 
Kwenye Dunia Tufe,..ni Direction ipi napaswa kuelekea towards Jua ikiwa ni Saa 2:30 usiku Tanzania,... Assume Dunia ina umbo hili ➡️🌍
Haijalishi ulipo au muda, utaelekea direction ya jua lilipo bila kujali kwa muda huo linaonekana kwa macho au la maana huendi kwa kutazama na kulifata, unatumia hesabu na hapo kuna hesabu za kutosha kutegemeana na kifaa utakacho tumia kwenda kwenye jua.
 
Kitu ambacho hakiwezi kushikika na nini? Kila kitu kinaexist kwenye kitu. Mambo ya Infinity hayo.

Kwani gesi inashikika? Gesi Ikiwa imejazwa kwenye chupa inakuwa na shape ya chupa na kushikiliwa na chupa au inakuwa haina shape sababu haishikiki kama unavyosema?
Ndiyo gesi Kwa kuwa haishikiki huwezi kusema ina shape., kama ilivyo Kwa maji hayana shape.

Kuweka simple, jiulize gas ina shape gani? achana na shape ya container unayowekea hiyo Gas,..
 
Haijalishi ulipo au muda, utaelekea direction ya jua lilipo bila kujali kwa muda huo linaonekana kwa macho au la maana huendi kwa kutazama na kulifata, unatumia hesabu na hapo kuna hesabu za kutosha kutegemeana na kifaa utakacho tumia kwenda kwenye jua.
Lengo la swali langu ni kwamba,...ikiwa mnasema Jua linazama that means at 2:30 nikiwa Tanzania ili niende lilipo Jua....itabidi niende downward (as if nazama) kama jinsi Jua lilivyoonekana kufuata muelekeo huo?
 
Tunaoshughulisha akili ni sisi ambao pamoja na mionekano wa hayo magimba huko juu kuwa midogo, haijatosha kutufanya tuamini kuwa ni size ndogo..
Wewe umeshughulisha vipi akili sasa?

Au NASA walivyokuambia Dunia ni Tufe linalozunguka ndiyo tayari ushashughulisha akili yako?
 
Ndiyo gesi Kwa kuwa haishikiki huwezi kusema ina shape., kama ilivyo Kwa maji hayana shape.

Kila kitu kina shape. Shape inatokana na container. Hayo unayoyaita maji yapo somewhere, yameshikiliwa na something, na yamechukua shape ya hiyo something.

Hata wewe unashape sababu kuna container limekushikilia likatengeneza hilo umbile ulilo nalo. Otherwise mambo yaliyokuunda yakisha sambaa huwi wewe tena.

Kila kitu kinashikiliwa na kitu ndo shape inapatikana. Na shape hutokana na kishikio au container na kila kitu ni kishikio au container ya kitu kingine.

Kuweka simple, jiulize gas ina shape gani? achana na shape ya container unayowekea hiyo Gas,..

Huwezi ondoa container unayoiweka hiyo gasi kwa sababu shape inatokana na hiyo container na ukiondoa container hii inafata nyingine hivyo hivyo. Yaani lazima kitu kiwe kwenye kitu na kitu kwenye kitu na kitu kwenye kitu to infinity na hicho kitu kinachoshikilia kitu ndo kinatengeneza shape Sijui kama unanielewa.

NADHANI KAZI IPO ILI TUELEWANE.
 
Lengo la swali langu ni kwamba,...ikiwa mnasema Jua linazama that means at 2:30 nikiwa Tanzania ili niende lilipo Jua....itabidi niende downward (as if nazama) kama jinsi Jua lilivyoonekana kufuata muelekeo huo?
Hapana. Jua kuzama ni lugha inayomaanisha usiku unaingia. Hiyo lugha haina uhusiano na jua kwenda chini.
 
Kila kitu kina shape. Shape inatokana na container. Hayo unayoyaita maji yapo somewhere, yameshikiliwa na something, na yamechukua shape ya hiyo something.
Sawa...,hivi kwa mfano Maji tukiyaweka kwenye sponge,.yanakua na shape gani?
 
Hapana. Jua kuzama ni lugha inayomaanisha usiku unaingia. Hiyo lugha haina uhusiano na jua kwenda chini.
Sawa na Mimi nakubaliana na wewe kwamba Jua actually halizami wala kwenda chini..
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Wewe umeshughulisha vipi akili sasa?

Au NASA walivyokuambia Dunia ni Tufe linalozunguka ndiyo tayari ushashughulisha akili yako?
Mbona unaleta utoto,

Nini maana ya kujifunza ?

kila tunachokisoma tunakipokea kwa kukipitisha kwanza kwenye tafakuri ili ubongo uchakate na kufanya tafiti zinazowezekana ili kukubaliana na tulichokisoma.

Hiki unachokisema wewe ni akili za watu wa flat Earth ( Hao/nyinyi mnategemea youtuber wanaopinga sayansi na kazi zake )

Siamini mtu mwenye akili timamu, ambae kichwa chake kina uwezo mzuri wa kudadavua mambo na kuyachakata ili kuchuja na kuelewa facts kama anaweza akasema Dunia ni flat, Siamini.
 
Kwa hiyo maji ili yakae kwenye vitundu inabidi yawe na shape ya hivyo vitundu.
Kwa ufupi ni kwamba maji on it's own hayana shape,.na ndiyo maana yanaweza ku fit kila sehemu......kitu chenye fixed shape hakiwezi kukaa kwenye kila container.
... Bruce Lee alishawahi kusema kwamba "When you put water into a cup it becomes a cup, you put it into a teapot it becomes a teapot, the water can flow or it can crush, be formless, shapeless like Water,..akamalizia kwa kusema "Be water my friend"!
 
Mbona unaleta utoto,

Nini maana ya kujifunza ?

kila tunachokisoma tunakipokea kwa kukipitisha kwanza kwenye tafakuri ili ubongo uchakate na kufanya tafiti zinazowezekana ili kukubaliana na tulichokisoma.

Hiki unachokisema wewe ni akili za watu wa flat Earth ( Hao/nyinyi mnategemea youtuber wanaopinga sayansi na kazi zake )

Siamini mtu mwenye akili timamu, ambae kichwa chake kina uwezo mzuri wa kudadavua mambo na kuyachakata ili kuchuja na kuelewa facts kama anaweza akasema Dunia ni flat, Siamini.
Yes upo sahihi,. Kama usingefundishwa na kujifunza nadharia za Dunia Tufe linalozunguka,.on your own usingeweza kujua wala hata kuhisi kwamba Dunia ni Tufe linalozunguka.

Kuhusu flatness ya Dunia haihitaji YouTubers ili ujue Dunia ni flat-plane,.inahitaji macho na akili Tu.
 
Kwa ufupi ni kwamba maji on it's own hayana shape,.na ndiyo maana yanaweza ku fit kila sehemu......kitu chenye fixed shape hakiwezi kukaa kwenye kila container.
... Bruce Lee alishawahi kusema kwamba "When you put water into a cup it becomes a cup, you put it into a teapot it becomes a teapot, the water can flow or it can crush, be formless, shapeless like Water,..akamalizia kwa kusema "Be water my friend"!
Maji on it's own unamaanisha nini boss? Hakuna kitu ambacho kipo on its own, kila kitu ni muunganiko wa vitu vilivyoshikiliwa na kitu na kishikio ndo hutengeneza shape.
 
Anhaa kumbe,..basi tusaidie maji yana shape gani?
 
We jamaa ni mgumu sana kuelewa. Nimekuambia, hiyo shape yako uliyo nayo inatokana na mfumo wa container lililokushikilia usitapanyike into space, huna shape nje ya hicho kishikio, same to water, itachukua shape ya kishikio. Tofauti yako wewe na maji ni kuwa maji yanaweza fit kwenye vitu vingine vya aina nyingi na kuendelea kuexist kwa shape ya hivyo vitu.
 
Back
Top Bottom