Sahihi mkuu lakini hii haitufanye tusizingatie yale meeengi ya uhalisia ambayo yanathibitishwa na milango yetu ya fahamu.
Maadamu milango ya fahamu inathibitisha uhalisia wa mambo mengi basi haina budi tuyazingatie mambo hayo mpaka pale kutakapokuwa na uthibitisho unaopingana na uhalisia tunaouexperience kwa milango yetu ya fahamu,tena uthibitisho ambao hauleti utata kama vile mirage sote tunafahamu kwamba yale sio maji yaani haina utata hiyo hakuna atakayebisha hiyo.
Ni kweli tunapaswa kutumia milango yetu ya fahamu mpaka tutakapo kuwa na uthibitisho vinginevyo.
Mfano wangu wa mirage ulikua na lengo la kuonesha kuwa kuna mambo yanaweza kuonekana kwa macho tukadhani ni kitu fulani, kumbe ni tofauti kabisa na tunachokiona.
Yaani, tunachokiona kwa mbali ni KAMA maji lakini kiuhalisia ni effect ya refraction of lights tu.
Mtu asiyejua mambo ya refraction akiona mirage na ukamwambia yale sio maji atabisha.
Hii ni kwa sababu amategemea milango yake ya fahamu pekee kujua ukweli wa mambo.
Mfano wa kunywa kinywaji chenye flavour ya tunda ulikua na kusudi hilo hilo.
Mkuu kuhusu picha zinazotolewa na satelite tulishazungumza kwamba zina utata,hazina uhalisia mfano hiyo picha ya chini ni ya kutengeneza sio halisi.
Kumbuka kwamba kwa technolojia ilivyo hatuwezi kuamini mambo kwa picha tu maana utaalamu ni mwingi so picha za satelite BADO hazitoshi kuonesha umbo la dunia kwa sababu kuna utata katika hilo na picha za kutengeneza.
Mkuu,
Nilikuuliza awali kama unatambua uwepo wa setelite katika maeneo mbalimbali ya anga la dunia.
Kama unatambua uwepo wake, ningeomba nijue japo kazi moja ya hizo satelite.
Ni kweli kwamba hatuwezi kuamini mambo kwa picha tu.
Lakini picha iliyo halisi inaweza kuwa kithibitisho tosha cha ukweli wa jambo.
Ningependa pia kujua kwanini unasema kuna utata au kukosa uhalisia kwa hizo picha.
Je, umeangalia features gani ukatambua kuwa hizo picha si za uhalisia bali ni za kutengeneza tu?
Je, unadhani waliozitengeneza wanapata faida gani kwa kufanya hiyo kazi ya kutengeneza picha za uongo kuhusu dunia?
Je, kunapicha zozote(zisizo za kutengenezwa) zimewahi pigwa na satelite?
Tutajuaje kama si za kutengenezwa tu?
Kama umewaza hivi mkuu kwa kudhani kwamba dunia tambarare itakuwa ni ndogo tu basi sivyo,dunia tambarare nao husema kwamba dunia ni kuuuubwaaa saaana licha ya utambarare wake.
Hivyo dunia tambarare nayo ni kuuuubwaaa pia kiasi kwamba haiwezekani satelite moja ikamulika sehemu yooote ya dunia.
Umeongelea satelite.
Unatambua uwepo wa picha za setelite katika maeneo mbalimbali ya anga la dunia?
Nisaidie kazi mojawapo ya hizo satelite.
hii hoja mkuu nitaijadili peke yake katika comment moja alafu tuone kama maelezo yangu yatamake sense kwako ama laa.
Kwa sababu tunajadili idea na uwezekano na wala hatujadili mambo ambayo tayari yana uhakika.
So nakuahidi mkuu suala hili la kipindi kifupi cha jua nitalielezea katika comment ya peke yake.
Sawa mkuu.
Nasubiri.
Mkuu nasema kwamba "FORCE ZAIDI INAHITAJIKA ILI KITU KILICHO KWENYE MWENDO KIENDELEE KUWA KWENYE MWENDO"
Tunaporusha jiwe angani maana yake lile jiwe linasukumwa na force ya mkono force tuliyotumia kurisha jiwe.
Hivyo basi kadri muda unavyozidi kwenda ile force inapungua ns jiwe litarudi chini(sio kwa sababu ya gravit.force) bali kwa sababu force imepungua.
HIvyo basi tungekuwa constant force kwenye lile jiwe ambalo tumerusha basi jiwe lisingerudi chini tena lingeenda juu tu,lakini kwa kuwa force inapungua na jiwe litarudi chini.
Ni kweli tunaporusha jiwe angani maana yake lile jiwe linasukumwa na force ya mkono yaani force tuliyotumia kurusha jiwe.
Nilichoshindwa kuelewa ni namna hiyo force itakavyo potea kadri muda unavyozidi kwenda.
Itapotea kwenda wapi mkuu?
Hewani?
Nini kinafanya isiendelee kudumu tu bali ipotee?
Hapa kweli nimetoka kapa.
Fafanua nipate kuelewa.
Kwa ninivyojua, jiwe litarudi chini kwa sababu ya grivitational force inayolivuta kuja chini.
Jiwe linapo rushwa mwanzoni, huwa na kasi kubwa kutakana force iliyotumika kulirusha.
Lakini gravitational force uact kwenye hilo jiwe kwenye kwa mwelekeo(kwenda chini) ulio kinyume na mwelekeo jiwe lilipo rushwa(kama limerushwa juu).
Ni kama unapojaribu kukimbia then mtu anakuvuta shati kukurudisha nyuma.
Hivyo basi, baada ya muda jiwe lile hupunguza kasi yake ya kuelekea juu, then husimama, na kisha kubadilisha mwelekeo wake na kuanza kuja chini(towards gravity).
Kumbe, ile force iliyotumiwaa kurusha imebaki "constant" kabisa, ila tu kuna force nyingine, iliyo kinyume na ya awali imetenda kazi(gravitational force)
Hovyo basi kama tunahitaji jiwe liendelee kutembea kwenda juu maana yake tunahitaji force zaidi ili jiwe liendelee kutembea,lakini kama hakuna force zaidi jiwe litarudi chini.
Assume umerusha jiwe limeenda mita 10 juu,then kabla halijaanza kushuka mtu mwingine akalirusha likaenda 10m juu trna ,then akalidaka mwingine akarusha 10m juu na kuendelea, UNADHANI NINI KIMESSABABISHA JIWE LISIRUDI CHINI ?
bila shaka ni kwa sababu ya force mpya ambayo tumeiapply katika jiwe baada ya kila 10m ambazo jiwe lilitaka kurudi.
Kama nilivyoeleza;
force iliyotumiwa kurusha imebaki "constant" kabisa, ila tu kuna force nyingine, iliyo kinyume na ya awali imetenda kazi(gravitational force).
Tukitaka jiwe lisirudi chini, hatuna budi kulirusha kutumia force itakayo lifanya jiwe hilo lipate kasi isiyopungua escape velocity, 11.2km/s.
Hii force ita overcome gravitatinal force na jiwe halitarudi.
Mfano uliutoa hapo sijweza kuuelewa vizuri. Pengine ungeurudia kwa maneno mengine ili twende sawa.
NA mimi hapa naweza kuuliza "UNAPOSEMA VITU VIKIRUKA VINARUDI KWA SABABU YA GRAVITY FORCE,JE HIYO GRAVITY FORCE KWA NINI ISIVISHIKILIE VITU HIVYO PALE VINAPORUKA TU ANGANI ??
Nimerudisha swali kwa sababu swali lako linaweza kuwa dhidi yako juu ya gravitational force.
Ni vizuri ukitumia neno "kuvuta" na si "kushikilia".
Maana unaweza kuvuta kitu pasipo kukishikilia.
Mf. Sumaku huweza kuvuta vitu vilivyo mbali kidogo pasipo hata kuvishikilia.
Gravitational force inavuta, haishikilii.
Kwa sababu nikirusha jiwe juu mbona gravitational force haifanyi kazi pale pale badala yake inasubiri jiwe lieendee mbali kisha likiishiwa nguvu ndio gravity anakuja kuJITAPA KWAMBA yeye ndio kafanya jiww lirudi.
Mkuu,
Ukirusha jiwe juu, gravitatinal force ina act palepale.
Lakini kwa kipindi kifupi baada ya kulitupa, jiwe linakua na initial momentum.
Momentum ni ile hali ya kitu kuendeleza hali yake ya kasi au utulivi.
Hapa momentum huathiriwa na ukubwa wa jiwe hilo, pamoja na kasi ambayo jiwe lilitupwa awali kabisa.
Hivyo,kutokana na momentum, kwa kipindi fulani jiwe litaenda juu kwa kasi japo force of gravity ipo, na inaendelea kuvuta.
Gravity hii ndio hupelelekea kupungua kwa kasi ya kwenda juu(kadri muda unavyoenda, tangu liliporusha awali).
Hii ni kutakana na kwamba force hupelekea change in momentum(i.e kupungua kwa momentum).
Kupunguakwa momentum huku hupelekea kupungua kwa kasi(momentum=uzito×kasi)
Baadae jiwe hufikia kwenye hiyo hali unayoitambua kama "kuishiwa nguvu" (kasi ya kwenda juu imepungua kabisa) na huanza kuja chini, towards gravity.
Hivyo tulitarajia pia kuona gravitationa force inaact soon tu baada ya kurusha jiwe,lakini hatuoni hilo,sasa ni sawa na kusema gravitationa force anatuibia,yaani anajificha then jiwe linapopoteza ile force yake then gravitation force anatokea anatuzuga kwamba yeye ndio anarudishs vitu chini ?
Kama kweli yeye gravitation force anafanya kazi hiyo kwa haki na uzalendo basi tuliratajia kuona kwamba hakuna kitu kiende juu hata point moja kwa sababu gravitational force always yupo.
Sijui umeyaoata maelezo yangu mkuu ?
Nimekuelewa na nimetoa maelekezo juu hapo.
Hapa mkuu nikupe mfano.
Mimi nasema kazi ya mlango ni kufanya mtu asiingie,kwa hiyo kama lango haupo maana yake watu wataingia.
Hovyo hatuwezi kusema kwamba mlango haujafanya kazi yake wakati haupo pale,lazima uwepo mlango kisha ndio mlango huo utafanya kwzi yake.
Nirudi kwenye point.
ARDHI NDIO HUSHIKILIA VITU kwa maana ardhi inakazi ya kushikilia vitu viwe juu yake.
Hivyo ardhi ikitoboka maana yake hapo palipotoboka hapana ardhi tena,na kama ardhi haipo basi tusitegemee ile kazi ya kushikilia kitu hicho ipatikane wakati huyo mfsnyaji(ardhi) hayupo (katoboka).
Hivyo ardhi ikitoboka maana yake haipo na kama haipo na kazi yake pia haitokuwepo yaani ileeèeee kazi ya kushikilia ardhi,hivyo hapo hatuwezi kuilaumu ardhi kwamba haijafanya kazi yake wakati ardhi yenyewe haikuwepo.
Nakubaliana na wewe kwamba ardhi inashika vitu vilivyo juu yake. Na ukiiondoa utadondoka.
Nilicho ongezea tu ni kwamba;
gravitational force yenyewe inavuta vitu kuelekea chini(haivishiki).
Na kwamba pasipo kuvishikilia na ardhi iliyopo juu(mf. Chini pakitoboka) basi hivyo vitu vitashuka chini kwa sababu ya gravity.
Zaidi, gravitational force ipo tu, vitu vikiwa either vimeshikiliwa au havijashikiliwa.
Lakini matokeo yake yameonekana baada ya vitu hivyo kuacha kushikiliwa(na ardhi).
Ni kama unaposhikilia kitu chepesi kwenye upepo mkali.
Ukikiachia kitapeperuka.
Hakitapeperuaka ukiwa umekishika vizuri.
Haimaanishi nguvu ya upepo ilikua haipo kilipo kua kimeshikwa.
lakini kama tunakubali kwamba grav.force ndio inavuta vitu chini basi tukubali kwamba haya majumba yote na binadamu wote wapo hapa sio kwa ajili ya gravitational force bali kwa ajili ya ardhi,kwa sababu ardhi ikitoboka tu sote tunaenda chini,so why now hatuendi ? Kwa sababu mwamba ardhi yupo anatushikilia na gravitationa force(kama ipo) kawekwa pembeni kwanza.
Nimejaribu kulezea hapo juu mkuu.
Utanisamea sana kwani ninapata ugumu kukueleza vitu vingine in details as ni masomo marefu na yanahitaji muda mwingi.
Mfano. Mambo ya momentum, laws of motion n.k ni msingi mkubwa wa maswali unayoweza kupata.
Nilichojaribu kueleza ni kidogo sana kati ya mengi.
Hivyo sitashangaa kama bado utakua na maswali zaidi na zaidi.
Pengine itahitajika somo zima la msingi wa maswala ya motion na gravity ili tuelewane kikamilifu.
Kama uko interested na kujua hayo mambo ili uweze kuhitimisha kama ni ya kweli au uongo, unaweza pitia link nilizo ziweka hapo awali.
Uneweza ongeza na hii.
Want to see an object accelerate? Drop it. If it is allowed to fall freely it will fall with an acceleration due to gravity. On Earth that's 9.8 m/s².
physics.info
Kama utahitaji info zaidi niko tayari kushare na wewe source mbalimbali ili tujifunze.
Ukiwa na maswali, niko hapa kujibu.