Binafsi naamini ya kuwa dunia ni duara, nitatoa sababu ambazo kwangu sina kabisa chembe ya shaka kwa hoja zifuatazo:-
Ijulikane kuwa zipo aina nyingi za ramani, wengi tumezoea hii tuliyosoma tangu shule ya msingi. (Sijui kwa jina inaitwaje), ramani ambayo inaanza na bara la America kisha Africa na Europe ikifata Asia na mwisho ni Australia kama sijakosea.
Kama utakua unaifahamu hii tu basi kuna mambo mengi utaona haiwezekani. Nina atlas ya collins-longman ambayo bara la Africa linaanza kisha Asia, Australia na mwisho ni bara la America.
Kwa hiyo nitajikita sana kwenye hii ramani ya pili. Bahari ya Pacific imetenganisha bara la America na bara la Asia. Lakini kwa ramani ya kwanza hili unaweza usilione.
Jibu jepesi ambalo halihitaji hata kuumiza kichwa ni hili:- mnamo tarehe 7/12/1941 kikosi cha anga kutoka japan kilifanya shambulizi la kustukiza katika bandari ya pearl (pearl harbour) iliyokua kambi ya jeshi la maji la marekani. katika jiji la Honolulu kisiwa cha Hawii. Mantiki ya kuandika hili ni kwamba umbali wa japan na hawii ni 6,604km ambayo ni safari ya sasa 8.5. Japan na na San Francisco ni 3,701km. Maana yake mtu aliye japan anaweza kwenda bara la America ama kupitia mashariki ama mahharibi.
Japan aliunda bomu la Fu-Go baloon bomb, mabomu ambayo yalielea kwa upepo kuelekea USA, mengi yalitua katika maeneo mbalimbali ya US ikiwemo Montana na Alaska. Nimeandika nikiwa na lengo la kujifunza, kuna watu wakiangalia ramani hii tuliyozoea kuna mambo yatakua magumu kueleweke.
Matharani; tunaona jinsi korea kaskazini anavyotamba kuwa makombora yake yanauwezo wa kufika USA, lakini wengi tukipiga picha kwa kutumia ramani tuliyo zoea utaona ni ngumu sana... ni kitendo cha kuvuka tu bahari ya Pacific.
Sent using
Jamii Forums mobile app