Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Usiongee sana,....ili uthibitishe kwamba Dunia ni Tufe lete ushahidi usio na shaka.

1. Lete authentic picha, ambayo sio Computer generated (CGI).
2. Au lete video halisia kutoka hizo satellite unazosema zikionyesha, Dunia Tufe inayozunguka.
 

Attachments

  • spaceeves-20240207-0001.mp4
    7.4 MB
Yes sahihi kabisa mjadala huu, utakua na tija endapo tutautumia kuelimishana na sio kubishana.......

Nikija kwenye hoja zako,...nadhani hoja ya kwanza juu ya "SHIP VISIBILITY" nishaijibu hapo juu kwa kuuliza maswali ambayo yanaonyesha weakness kwenye hoja hiyo ya ship visibility with reference to earth's curvature kwenye bahari....
Nikija kwenye hoja hii ya pili,. Unasema kwamba "Dunia ni kubwa sana that's why it's impossible to notice curvature"......
Logically ukishasema hivyo πŸ‘†πŸΌ,....hutakiwi tena kusema kwamba Ships zina descend towards the curve kwenye bahari,...Kwa kuwa ukisema hivyo unakua ume contradict kauli yako ya awali kwamba "Earth is too large to notice the curvature"

Nadhani mpaka hapo hoja ya Ship visibility with reference to the curvature nishaiweka sawa kwamba ni kitu ambacho hakipo.

Naomba nijibu hoja hii ya mwisho kabisa....
Mkuu kwamba unasema maji yanajikunja?,..... Sio kweli Water can't curve/bend... Maji hasa ya kwenye hizi large water bodies hutoyaona yakijikunja bali yame rest kwenye horizontal level........ teknolojia imeendelea siku hizi ili uthibitishe hili unaweza ukatumia hata drones au laser uone jinsi inavyoonyesha straight line kwenye bahari,...ingekua maji yana curve ukitumia laser kwenye bahari ungeweza kuona mwanga hauendi straight badala yake ungeona bending.


Tazama hizo Glass mbili za maji hapo juu,....kisha niambie glass ipi kiuhalisia ina relate na kile ambacho tunakiona kwenye maji ya bahari.

Ahsante,.. naamini nimejitahidi kugusa hoja zote 🀝🏼
 
Sawa ,let's say hii video ni ya kweli..... kwanini video haionyeshi Dunia iki rotate?

Maana tukiwa kwenye earth's surface,... tunaambiwa Dunia ni kubwa sana ndiyo maana hatuhisi rotation na kwamba ina move at a constant rate.....umejaribu Kujiuliza hilo?

Au hata ukiwa kwenye atmosphere pia,. huwezi uka notice rotation? Eti mkuu Experience now
 
Kwanini tukiruka juu tunarudi chini according to flat earthers theory yenu ipoje hapa?
Ukiruka juu lazima urudi chini,... Kwasababu kikanuni ili usirudi chini inabidi "upae" na sio "uruke"

Kwa kuwa akili yako ishaamini gravity ndiyo inafanya hivyo,.. ngoja nikuulize swali:-

Kama gravity ndiyo inafanya Mtu arudi chini,..... kwanini force ya gravity ishindwe kumzuia Nyuki na udogo wake asipae, iweze kumzuia Binadamu ????! Ukipata jibu tafakari.


Kukuongezea zaidi, ili upae na usirudi chini kadri ya muda utakaoutaka inabidi ujiulize:-
1. Ni vitu gani vinawezesha viumbe wengine kupaa wanavyotaka,.na wanarudi chini wanavyotaka bila kuzuiwa na the so called gravity.....ukishajua vitu hivyo hautorudia "kuruka" tena bali 'utapaa" ili usirudi chini mpaka muda unaoutaka.

2. Ukishamaliza hapo chunguza tena umuhimu wa hewa "air" + Wind kwenye kupaa,..ukikariri gravity hutoweza kufikiria beyond., utaishia kusema Papai linaanguka chini kwa kuwa linavutwa na gravity.

"Bird and insect flight: The principles of lift and drag apply to all flying creatures, not just airplanes. Birds and insects use their wings or other body parts to manipulate air and generate lift in similar ways."

zingatia hapo kwenye neno
"generate lift "

NB: ELIMU NI BAHARI....
 
Ndo shida yenu mkuu, mimi nimeuliza logic ama ile framework au mechanism yote ya kuruka na kurudi kwa ground according to nyie mnavoamini.

Ghafla umeirukia gravity na kuikosoa. Acahana na gravity kaka maana hii nyi mmekataa haipo wewe elezea nyinyi mechanism kwa upande wenu zipo vipi, maana gravity na yenyewe ina kanuni zake katika uwasilishaji wewe huwezi elewa kwa sababu hauitambui, na mimi sina shida na hilo ,


Elezea tu kwa theory mnazotumia nyinyi epuka mambo ya kuprove point by elimination kila muda
 
Inachukua masaa 23 na dk 56 (24 hours ) kukamilisha rotation,
Na clip ina sec 25 tu.

Bro are you serious unataka uuone huo mzunguko unavyofanyika kwenye sec 25 ya hii clip ???

Hili swali ungejiuliza hata kwa nadharia yako hiyo hiyo ya jua kuizunguka dunia, Je umewahi kunotice jua linavyofanya huo mzunguko ?? Na unaweza ukanionyesha clip jua likiwa linazunguka ?

Kuna umuhimu wa wewe kujifunza kuhusu muda,Kasi na umbali ( Time, Speed and Distance )

Angalau utakua makini kwenye maswali unayoyauliza.
 
Hapo unaamini umetetea hoja yako lakini kumbe umezidi kujiweka kwenye angle ngumu......

Hivi unafahamu kwamba, Earth is in constant movement according to those who claimed that the earth is moving?

Kiasi kwamba hata kwenye hiyo video yenye 25 seconds still Dunia ipo kwenye rotation,.?

Earth is in constant movement kama unavyoamini, so logically even in 25 seconds, We should notice/see about 75 meters (246 feet) of earth's movement.

Nakupa mfano wa kawaida tu,.... let's say Treni linachukua masaa 10 kufika Kigoma,...na Treni hilo lipo kwenye constant movement hakuna kuchimba dawa muda wote lipo kwenye mwendo....Nikirekodi video yenye japo 15 seconds zitatosha kabisa kuonyesha kwamba hiyo Treni ina move na sio mpaka safari ya kufika Kigoma ikamilike ndiyo tujue kwamba Treni ina move.... Naamini umeelewa.


NB:- Kwa upande wa Jua unaweza ukachukua video na ukaeleweka hata kama video hiyo ikionyesha Jua limesimama,... Kwasababu hakuna Mtu anaesema Jua lina move constantly kama isemwavyo kwa Dunia,...may be Jua lina move Kwa vituo with
some rests, who knows ?πŸ’­.
 
POROJO
Mfano ulioutoa tu unathibitisha wewe ni mtu mwenye kiwango gani cha ufikiri, Ngoja nkuache mkuu.
 
Binafsi naamini ya kuwa dunia ni duara, nitatoa sababu ambazo kwangu sina kabisa chembe ya shaka kwa hoja zifuatazo:-
Ijulikane kuwa zipo aina nyingi za ramani, wengi tumezoea hii tuliyosoma tangu shule ya msingi. (Sijui kwa jina inaitwaje), ramani ambayo inaanza na bara la America kisha Africa na Europe ikifata Asia na mwisho ni Australia kama sijakosea.
Kama utakua unaifahamu hii tu basi kuna mambo mengi utaona haiwezekani. Nina atlas ya collins-longman ambayo bara la Africa linaanza kisha Asia, Australia na mwisho ni bara la America.
Kwa hiyo nitajikita sana kwenye hii ramani ya pili. Bahari ya Pacific imetenganisha bara la America na bara la Asia. Lakini kwa ramani ya kwanza hili unaweza usilione.
Jibu jepesi ambalo halihitaji hata kuumiza kichwa ni hili:- mnamo tarehe 7/12/1941 kikosi cha anga kutoka japan kilifanya shambulizi la kustukiza katika bandari ya pearl (pearl harbour) iliyokua kambi ya jeshi la maji la marekani. katika jiji la Honolulu kisiwa cha Hawii. Mantiki ya kuandika hili ni kwamba umbali wa japan na hawii ni 6,604km ambayo ni safari ya sasa 8.5. Japan na na San Francisco ni 3,701km. Maana yake mtu aliye japan anaweza kwenda bara la America ama kupitia mashariki ama mahharibi.
Japan aliunda bomu la Fu-Go baloon bomb, mabomu ambayo yalielea kwa upepo kuelekea USA, mengi yalitua katika maeneo mbalimbali ya US ikiwemo Montana na Alaska. Nimeandika nikiwa na lengo la kujifunza, kuna watu wakiangalia ramani hii tuliyozoea kuna mambo yatakua magumu kueleweke.

Matharani; tunaona jinsi korea kaskazini anavyotamba kuwa makombora yake yanauwezo wa kufika USA, lakini wengi tukipiga picha kwa kutumia ramani tuliyo zoea utaona ni ngumu sana... ni kitendo cha kuvuka tu bahari ya Pacific.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo hizo ndiyo hoja zisizo na shaka,...? Acha masihara mkuu
 
Reply post #1445 mkuu
Sawa,,.. kwenye post #1444 kuna majibu ya swali lako endapo utasoma Kwa makini... Kumbuka uliuliza kwamba πŸ‘‰πŸΌ "Kwanini tukiruka juu tunarudi chini according to flat earthers theory yenu ipoje hapa?"

Nikakujibu kwamba ili usirudi chini, unatakiwa "upae" na sio "kuruka"

Kabla hatujaenda mbali,..mpaka hapo umeelewa kwamba kwanini ukiruka unarudi chini?
 
Kupaa ni nini, na vitu gani vikiwepo kitu kinapaa, na je kwenye kuruka viyu gani vinasababisha kurudi chini au vitu gani, kwamba kukiwa na condition hii kitu kitakua kimeruka na kurudi chini

NB: tafadhali sana usitaje concept yoyote ambayo utasema kitu flani mnadanganywa,
 
1. Kupaa ni kitendo cha kufanya mwendo(movement ) kwenye hewa (air) kwa kutumia either wings, like birds, or through the use of aircraft such as airplanes, helicopters, or other flying machines.

2. Miongoni mwa kitu cha muhimu ili kitu kuweza kupaa ni LIFT (NGAZI)..... kwenye kupaa hewa (air) ndiyo inatumika kama ngazi...na ndiyo maana utaona hata Ndege(birds) wakipiga mbawa zao ili kutengeneza lift ya kuwafanya wapae,...


Birds flap their wings in a specific way called the wing beat, which creates a difference in pressure between the top and bottom of the wing. Above the wing, the pressure is lower than below the wing.....This creates lift, which raises the bird into the air!

3. Kitu kitarudi chini endapo:-
kitapoteza uwezo wa Ku generate lift,. Ambapo hapo zinaweza kutokea sababu tofauti tofauti,.mfano Ndege (bird) akipata shida kwenye mbawa yake moja hatoweza Ku generate lift kitu ambacho kitamfanya arudi chini.
(a) sababu nyingine ni kukosa umbo sahihi,.Kwa mfano mnyama kama Tembo hana umbo sahihi la kumfanya apae.

(b) Hali ya hewa, mf. Upepo mkali,..Upepo ukizidi sana huweza kupelekea kurudi chini kwa kiumbe au objects iliyopaa.
 
Ikiwa mtu aliye japan, korea, Australia philippine n.k anaweza kwenda USA kupitia route ya magharibi ama mashariki iweje dunia isiwe duara?
Hiyo sio sababu ya kusema Dunia ni Tufe la namna hii ➑️🌍,..... Kwasababu hiyo scenario ya Mtu aliye Japan, Korea n.k kwende USA kupitia route ya Mashariki au Magharibi ina apply vizuri tu hata kwenye flat earth yenye umbo duara....

Lakini pia jaribuni kutumia akili zenu vizuri wadau,...Kwa mfano:-

Kama unaweza kufika point "C" Kwa kupitia point "B"...Kitu gani kikufanye ushindwe kufika Point "C' kwa kupitia point "A",..Tena kukiwa hakuna barrier yoyote kwenye points zote??!
 
Brother ushawahi kurusha coin kutoka mkononi mwako wakati gari ipo speed? Je coin iliangukia nyuma yako au iliangukia mkononi mwako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…