Huu uzi unanihuzunisha sana kuona kiwango cha ukosefu wa exposure kiasi hiki. Jamani kutembea nako ni kuona. Tembeeni, someni, jifunzeni mtajua.
Nianze nawe nkumbi, ulifundishwa dunia ni tufe kwa kuwa ni tufe, sio kwa sababu ya picha zinazoonyeshwa, ni kwa sababu ya fact zilizopo na zinazoendelea. Ukiangalia ramani ya dunia kama kitambaa kilichotandikwa itakwambia mji wa Tokyo uko mashariki ya mji wa San Francisco. Ungetegemea chombo cha usafiri wa angani kama ndege kinachotoka Tokyo kwenda Sanfrancisco kielekee magharibi ili kifike safari yake. Lakini sivyo, huelekea mashariki ndipo kinapofika haraka zaidi kuliko ile njia ya mwanzo. Huu ni mfano mmoja wa utufe wa dunia na faida moja ya kufahamu elimu ya utufe wa dunia. utafakari kwa ajili ndogo tu ya kawaida.
Kuna mtu kwenye huu uzi ameeleza kuwa ndani ya masaa 24 ya siku wakati eneo moja linapokuwa usiku lingine linakuwa mchana. Ninapoandika haya ni saa 12 asubuhi just linatokeza. Lakini ndugu yangu Yuko Florida sasa hivi ananiambia ametoka kazini ndio anaingia kitandani, usiku. Sasa elezea hili kwa hiyo theory ya tambarare.
Hizo theory za mleta uzi zimejikita Sana kwenye conspiracy theories ambazo nyingi zinajibika kirahisi sana ukipata exposure ya kinachoendelea duniani fizikali