Dunia ni duara ambalo kwenye ncha zake ni flat. Kipenyo kutoka ncha ya kaskazini ni kifupi kidogo kuliko kipenyo cha ikweta kwa tofauti ya km 44 hivi.Zipo sababu nyingi zinazothibitisha kuwa Dunia Ni duara. Asemaye vinginevyo huyo anachangamsha kundi Hana hoja ya kisayansi au kijiografia. Haya ni mawazo ya watu wa zamani ambayo Ni dhahiri leo yalitokana na ujinga tu. Kama Dunia ni tambarare maana yake lazima iwe na sura ya mstatili, upande mmoja ungekuwa mchana Dunia nzima na upande mwingine ni giza, kwenye ncha kungekuwa giza daima, satellite zisingeweza kuzunguka Dunia, watu tungeona mpaka ulaya kutoka Africa kwa sababu macho yetu hayana mwisho wa kuona.