Mwanzo ulisema unaweza kuona mpaka space station iliyopo km 400 kutokea Duniani.....
Au sio wewe uliyedai hivyo?
NB:- Macho yana limitation ya kuona, limitation ambayo inatokana na factors mbalimbali ikiwemo distance, obstacles na kadhalika.
Mkuu, mbona hata vitu rahisi kuvielewa ni ngumu kwako?
Ngoja twende kama darasa la kwanza:
KM 60 ni ndogo kuliko km 400.
Kama unaweza kuona kitu kilicho km 400, basi kilichopo km 60 unatakiwa pia uweze kukiona maana hapa ni dhairi macho yako hayajafikia limit yake.
Sasa wewe unaiona international space station iliyopo km 400 angani alafu taa za Zanzibar zilizopo km 60 kutokea pwani ya dar huzioni alafu unafikiri umefika limit ya uwezo wako wa kuona???
Pia macho pekee hayawezi kukupa uhalisia wa kila kitu.
1. Mbingu ina onekana ni ya blue, unafikiri na ublue huko angani?
2. Upinde wa mvua, unafikiri ukipaa utaupata huo upinde?
3. Sunset, unafiki kuna mawingu mekundu kila jioni?
4. Mirage, yale maji unayoona mbele ukiwa kwenye gari mchana, ulishawahi kuyafikia???
Unajifungia kwenye box na kulimit fikira zako, ukitoka nje ya hiyo jela yako utaona jinsi dunia ilivyokubwa na maajabu yake.
Asilimia kubwa ya vitu unavyotumia vimetokana na nadharia hizi hizi unazozipinga, kama unahisi nadharia zako ni sahihi tengeneza simulations alafu angalia kama hizo simulation zitakupa majibu sawa na unavyoona dunia inavyofanya. Ukiona hupati majibu jaribu kusimulate nadharia unazozipinga na kisha angalia kama nazo hazitoi majibu sahihi.
Bajeti ya kumpeleka kila anayezaliwa space ilikujihakikishia dunia ni duara kwa kweli hatuna (ukizingatia wanaweza sema kioo cha vessel ilitumikia sio real ni cgi).
Na ndo sababu tunapokua na ukakasi tunatafuta experiments zinazoweza prove au disprove fikira zetu.