Siri kubwa ya wapemba na wachaga kumpisha Mkinga ni mkinga kuuza kwa faida ndogo, umoja, bidii, kuheshimu wateja na nidhamu ya matumizi ya fedha

Siri kubwa ya wapemba na wachaga kumpisha Mkinga ni mkinga kuuza kwa faida ndogo, umoja, bidii, kuheshimu wateja na nidhamu ya matumizi ya fedha

90% ya Wakinga wajasoma,nadhani wote mnajua hulka za watu ambapo hawajasoma-ushirikina ndio nguzo yao.
 
Vipi pisi za kikinga, na zenyewe zimetanguliza mingo mbele kama pisi za..........
 
Ukweli mchungu.

1. Wakinga wanayo nidhamu kubwa sana ya biashara na kwenye customer care wapo vizuri, ni mara chache sana utakwaruzana na mkinga dukani kwake.

2. Wakinga wanakuwa boosted na mtaji wa mauzo ya miti au ndugu zao ambao tayari wamefanikiwa kwenye biashara. Yaani mkinga akisikia kuna hotel ya mkinga mwenzake atamletea wateja mpaka ashindwe mwenyewe kuwahudumia


3. Stage waliyopo wakinga wachagga walishakuwepo late 90's na early 2000's, sahizi wachagga wengi wamehamia kwenye real estate, lodge/hotels, makampuni ya ujenzi n.k

4. Wakinga na wachagga ni wapambanaji sana kiasili, hawana destruri ya uvivu na kubweteka hovyo hovyo.
 
Hao wakinga 90% waliiteka Tunduma saivi wamehamia kariakoo

Kuna mkinga mwenye mahotel ya "WANYAMA HOTEL" alikuwa tajiri balaaa ana maghorofa zaidi ya 5 hapa kariakoo

Lakini jamaa alipofariki wakasafirisha maiti kupeleka huko kwao walikosa hata pakulaza jeneza, jamaa hana hata kinyumba cha chumba kimoja hapo kwao

Iliwabidi maiti walaze kwenye nyumba ya babaake mdogo
Duh
 
Sio kariakoo tu. Mkinga akiingia sehemu yoyote mchaga hakai,mhindi hakai wala mpemba hakai. Hawa hawachangamani,sababu staili ya mkinga ya ufanyaji biashara ni unique sana.
Mswahili bwana. Wewe unadhani wahindi wamekimbia biashara ya maduka! Hawajakimbia ila wameshapitia hiyo hatua. Hao wakinga ndiyo kwao kunakucha sasa hivi wakati wahindi ni jioni.
 
Mkinga ni kabila linalopatikana mkoa gani?
 
Hao ndio wakinga bwana, hawaishi kukushangaza kwa jinsi walivyoimeza Kariakoo ambalo ndilo soko kubwa Tanzania nzima.

Zamani ilishazoeleka hio sehemu wamejaa wachaga na wapemba na makabila mengine madogo madogo kama waha (hawa huwa wanalazimisha mno waonekane wanalingana na wenzao wakubwa), wapare, n.k.

Kwa sasa hali imebadilika kabisa kwa mapinduzi anayofanga mkinga kwa sulaha yake kuu ya kuuza kwa bei ndogo, yani kwenye swala la bei kwa mkinga uta enjoy sana, faida anayotaka yeye huwa ni ndogo tu wala si kubwa, hata awe peke yake anaeiuza bidhaa, na hili limefanikiwa zaidi kwa wakinga wengi ndugu zao kujazana mji wa Guangzhou huko China na kwa sasa wana meli zao kabisa za kusafirisha mizigo na wana umoja wa kusaidiana.

siri nyingine wanajali sana wateja wao, kila mteja wanamjali.

Kwenye matumizi ya fedha hapa nadhani hawama mpinzani, mkinga anaishi simple sana
Wana meli zao ipi mkuu hiyo mkuu na ni mkinga yupi yupo Guanzhou?
 
Emu anza ubahili baada ya 20 years uje hapa uniambie kama umekuwa tajiri.
Wanajidanganya ivyo awajui yakwamba awa matajiri kupitia biashara zao zinawajngizia faida kubwa ila kwenye matumizi ni watumiaji wazuri wa pesa kuliko hata masikini.
 
Hao wakinga 90% waliiteka Tunduma saivi wamehamia kariakoo

Kuna mkinga mwenye mahotel ya "WANYAMA HOTEL" alikuwa tajiri balaaa ana maghorofa zaidi ya 5 hapa kariakoo

Lakini jamaa alipofariki wakasafirisha maiti kupeleka huko kwao walikosa hata pakulaza jeneza, jamaa hana hata kinyumba cha chumba kimoja hapo kwao

Iliwabidi maiti walaze kwenye nyumba ya babaake mdogo
We utakuwa mchaga hupendi mtu mwingine anayefanya vizuri asifiwe
 
Back
Top Bottom