Nimezunguka siku 32 Tanzania nzima kwenye miji mikuu na midogo inayofikika kwa lami kasoro Kigoma na Kagera
Nilikuwa na Kampuni moja hivi ya nje kwenye reaserch flani
Na nikafanya reaserch ya siri mimi nilitaka nione kama ni kweli wachaga wamesambaa Kila mahali na wanafanya vizuri kuliko watu wengine Nikakuta sio kweli
1. Kariakoo. Nilikuta wamekutana na upinzani mkali wamezidiwa na Wakinga
2. Tanga , Lushoto na Handeni ...ni mchanganyiko Kila mtu anapambana
Kama lushoto wenyeji wako moto sana ndio wakulima wakubwa wa Matunda na mboga mboga na wasafirishaji pia.
3. Handeni ..Mchanganyiko kidogo ila nimeona mchaga mmoja ni Mama mwenye duka kubwa la agrovet ndio aliyechangamka pale wengine ni Mchanganyiko
3. Lindi. Kondeboys wanafanya vizuri na wabena ingawa huu mji nao sijakuelewa vizuri
Pamepoa sana.
4.Masasi. Pako vizuri sana. Wafanyabiasha wakubwa hapa ni wabena na Wakinga na Kondeboys kidogo wanajitahidi.
5. Mtwara yote hii Wakinga / Wabena
6. SONGEA. Wakinga/ wabena
Labda huyu mwenye La chazz night club
Sijamjua Challes Hilary ni kabila gani
7. Njombe. Wenyeji wako very active Wakinga / Wabena
Mahotel mazuri, lodges nzuri wanatawala vizuri
8. Makambako . Wahehe/ Wakinga
9. Iringa. Vile vile ila niliingia kwenye bar moja ya mchaga inafanya vizuri
10.Mafinga. Wakinga. Na ndio Fredy vunja bei amekita mzizi kama home na kuweka Chachu kwa vijana wengi
11. Mbeya . Changanyikeni wachaga wapo, wanyakyusa wapo wahehe , wabena, Kila mtu yupo huko
12. Tunduma. Wakinga / Wabena na Mchanganyiko
13. Sumbawanga. Hakuna bingwa biashara kubwa zimeshikwa na waarabu wa Tawakall
Hawa wenye Dew Drop Kampuni ya maji
14. Mpanda. Pamechangamka sana ila hakuna bingwa Kila mtu anagusa kidogo kidogo maendeleo yanakuja
15. Tabora. Mji mkongwe ....sijaona chochote kilichonivutia
16. Nzega. Lodge nyingi tu ..Na vijana wengi kutoka singida wanyaturu na wanyiramba ndio wapambanaji hapa
17. Kahama. Hapa ni amazing. Kila kabila lipo na Kila mchunguli fursa.
Nililala submarine hotel nikafeel kama Niko Arusha uchumi ni kunyang'anyana hakuja shujaa
18.Singida. Wachaga wamevamia kidogo kwa Kasi hata manyoni hapo wapo Nililala Narumu hotel ni ya mchaga
19.Dodoma.
Ngoma droo Kila mtu anazama pango jipya
20.Moro. Changanyikeni
Wacha nipumzuke kidogo nitarudi tumalizie ziwani.