Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Nawasalimia wana JF wote.
Katika mwendelezo wangu wa kuwafundisha na kuwafungua macho watu, leo nimeonelea nilete siri iliyomo katika kufunga.
Kwanza kabisa nawaomba muelewe kwamba, kuna namna nyingi sana ya kufunga lakini nitaongelea namna tatu:-
1. Kufunga kwa malengo
2. Kufunga kwa mujibu wa utaratibu au sheria
3. Kufunga kwa mkumbo
Sitaelezea kila moja maana lengo la waraka huu ni kuongelea siri iliyomo katika kufunga.
Kuna njia nyingi ambazo hutumika katika kufunga lakini mimi leo ninaongelea njia moja ambayo huwa naitumia katika kufunga siku 21.
Mara ya kwanza kabisa nilifunga siku tatu mfululizo pasipi kula wala kunywa. Nilikuwa nimefunga na nimejifungia sehemu kwa ajili ya kusali na kuomba. Katika mfungo huo niligundua kuwa:-
1. Unapofunga unaufanya mwili uweze kukutii na kuanza kusikiliza kutoka ndani
2. Unapofunga unapata muda wa kuwasiliana na high self.
3. Kufunga holela pasipo utaratibu unaweza ukaathiri afya ya mwili wako.
4. Kufunga pasipo kufundishwa njia zilizomo katika ulimwengu wa roho, unaweza ukajikuta unarukwa na akili baada ya mfungo.
Ikumbukwe unapofunga unaufisha mwili ili uweze kuingia katika ulimwengu wa roho. Katika ulimwengu wa roho kuna levels 6, as I know mpaka sasa. Katika level ya kwanza utakutana na vurugu za kila namna. Hapajatulia, maana ni rahisi kwenda. Level hiyo kwa mara nyingi huwa tunaiita PEPO. Kwahiyo usipofundishwa namna ya kutembea katika ulimwengu huo; unaweza ukajikuta baada ya mfungo unakuwa mtu wa ajabu, au mara nyingine unarukwa na akili.
JINSI YA KUFUNGA UNAINGIA ROHONI PASIPO KUATHIRI AFYA
Niliweza kujifunza namna ya kufanya na kuniwezesha kila mwaka kufunga siku 21 mfululizo. Unatakiwa uwe na asali, sukari na maji.
Kila siku baada kufanya maombi ya asubuhi; chemsha maji, baada ya maji kuchemka kiwango cha chai, tia asali na sukari, kuywa kikombe kimoja mpaka viwili (Kikombe cha chai).
Ikifika jioni kama saa 12 au saa moja fanya hivyo hivyo, yaani chemsha maji tia sukari na asali.
Fanya hivyo kila siku mpaka siku 21. Mwili wako utaendelea kufanya kazi na hapo hapo utaweza kuingia ulimwengu wa Roho.
UWE NA JAMBO(MAMBO) LINALOKUFANYA UFUNGE
Utakapokuwa na jambo lililokufanya ufunge, litakusaidia kwamba utakapokuwa kwenye maombi na sala utajikita katika jambo lililokufanya ufunge. Sasa basi hii itakusaidia utakapikuwa katika level ya kwanza ya ulimwengu wa roho, hutababaika na yale yatakayokuwa yanatokea. Maana ukifunga pasipokuwa na jambo lolote, utajikuta unazagaa tu kwenye huo ulimwengu, kwahiyo chochote kitakachokuwa kinatokea ni halali yako.
Kuna nguvu katika kutamka. Tamka kwa kurudia rudia jambo unalotaka (Chanting). Liongea kwa sauti au ikiwezekana tengeneza wimbo.
Wakati wa kusali na kuomba, tafuta sehemu ya faradha.
NITAENDELEA NA SOMO HILI....