Siri niliyoipata katika kufunga siku 21 kila mwanzo wa mwaka

Siri niliyoipata katika kufunga siku 21 kila mwanzo wa mwaka

ULIMWENGU WA ROHO

Pale utakapofunga, utaufanya mwili uwe dhaifu. Mwili utaanza ku regulate namna ya kutuzakisha energy kwenye mwili kwa matumizi madogo ya chakula kilichopo kwenye mwili wako.

Kwakuwa unatumia asali na sukari huku ukiwa umevichanganya na maji, mwili utakuwa unapata kiwango kidogo cha chakula, kwahiyo mwili utaacha ku process unnecessary activities. Ndipo hapo milango ya fahamu na thought zitapunguza utendaji wake wa kazi. Ndipo hapo ulimwengu wa roho utakapoanza kuchukua nafasi.

Unaweza usiingie katika ulimwengu wa roho at the first week, lakini utakapoendelea kutenga muda wa faragha utaanza kuingia taratibu. Nakuhakikishia kabla ya siku hizo 21 kuisha utakuwa umekutana na mambo mengi.

Katika ulimwengu wa roho level one. Kuna vurugu za kila aina. Utakutana na kuzungumza na kila aina ya roho. Hakikisha lengo lako lililokufanya ufunge unalizingatia. Chanting inakuwa kama gateway ya kuingia huko.

Ni kwambie ukweli, usipo kuwa makini na kuwa mwangalifu, baada ya siku hizo utarukwa na akili. Utagudua mambo mengi ikiwamo kwamba uhalisia wetu ni ulimwengu wa roho. Utaweza kukutana na watu waliokufa na kuongea nao ana kwa ana. Na ukiwauliza wakupe evidences ya hayo wanayo yaongea watakupatia, na uta prove.

Utaweza kutembea (utaweza hata kuwasiliana na nafsi ya mtu aliyehai na kufanya jambo fulani). Hapa sasa baada ya mfungo wengine hugeuka na kuwa wachawi, wasoma nyota na waonaji.

Kumeibuka na kundi kubwa la walokole wanaojiita manabii. Ukweli ni kwamba hao ni waonaji sawa na wapiga ramli. Hao watu wanauwezo wa kukuelezea matukio yako yote yaliyopita.

Hata wewe ukifika katika ulimwengu wa roho jicho lako la tatu(spiritual eye) litaanza kufunguka. Lakini my WARNING tafuta kwenda mbali zaidi katika ulimwengu wa roho, usiishie hapo tu. Go to the most higher ili uweze kuwa enlighten. Katika level ya kwanza utakuwa na uwezo wa kuwasiliana na watu waliokufa na kuwa muonaji. Hii siyo enlightenment, enlightenment ni kujua siri kuu za spiritual world.

Utakapoanza kuona, unakutana waliokufa zamani na kuongea nao; USIOGOPE upo katika safari ya kuelekea ulimwengu wa roho level ya juu zaidi.

USIWAPE MBWA CHAKULA CHA WATOTO.

Nitatoa summary but not details.

NITAENDELEA.....
Umesema Utaweza Kuzungumza na Waliokufa...Sasa mbona Maandiko yanasema hakuana ushirika Kati ya walio hai na Wafu....
Na Ni Jambo gani hasa unazungumza na Wafu...?
 
Umesema Utaweza Kuzungumza na Waliokufa...Sasa mbona Maandiko yanasema hakuana ushirika Kati ya walio hai na Wafu....
Na Ni Jambo gani hasa unazungumza na Wafu...?
Ngoja nianze kwa kusema.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.

Kisha niongezee kwa kusema Andiko linaua bali Roho anahuisha.

Sasa hebu soma katika biblia upate kujua mzimu wa Samweli ulivyopandishwa.
11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.
1 Samweli 28:11

13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13

14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14
 
Tunaendelea...

Kama nilivyosema kufunga ni hatua ya kuutiisha mwili. Watu huweza kufanya mambo ya mwili wanapokuwa wamekula.

Lakini ninataka mpate kujua ya kwamba kufunga na kujinyima chakula pekee haitoshi. Unatakiwa unapofunga utenge muda kwa ajili ya Sala na Maombi.

SALA NI NINI
SALA ni neno la ujumla linalojumuisha maombi yote, iwe ya shukrani, mahitaji, ibada, sifa, toba,ulinzi, Baraka n.k…Kwamfano yale maombi ya Baba yetu uliye mbinguni Yesu aliyowafundisha wanafunzi wake….Ni mfano wa SALA.

KUSIFU
Unapoanza sala ni vyema ukaanza kwa kusifu. Kusifu ni pamoja na kukubali mazingira mazuri yanayokuzunguka. Nyota, wanyama, ndege na vitu vingine kuwa wewe huna uwezo wa kuvitengeneza. Unaweza kusifu kwa kuongea au kuimba. Kubali kushuka kwa kuna mambo mengi yapo juu ya uwezo wako. Hivi vyote tunavifanya ni vitendo vya kiimani. Unaweza ukataja masuala kadha wa kadha kulingana na imani yako. Lengo kuu ni kuweza kuhamisha hisia kutoka katika mwili na kuelekeza katika roho.

TOBA
Kitu kinachoweza kukukwamisha kuingia kwenye ulimwengu wa roho ni kuwa na ila ndani yako. Ile hali ya kujikataa na kuona kwamba wewe upo na makosa kadha wa kadha. Inaweza ikawa kikwazo kwako kuingia katika ulimwengu wa roho.

Kama kuna mtu amekukosea au umemkosea, tamka maneno ya toba na weka katika imani kuwa jambo hilo limekwisha. Kuna namna nyingine ya kujikataa mwenyewe. Jaribu kuongea maneno "NIPO SAFI" kwa kurudia rudia (Chanting) mpaka akili itakapo amini kuwa huna ila tena.

MAOMBI
Tamka maneno ya kutaka unachokihitaji. Iwe ni kutaka baraka, iwe ni kutaka ulinzi au kuomba kitu.

Inakuwa ni vizuri sana kama ukiwa umeandika na kuyaweka kichwani maombi yako. Yatamke hayo maombi kwa kurudia rudia. Ukiweza tengeneza wimbo wa hayo maombi yako.

Unajua mtu anaweza kukulaani au kukubariki kama atayaandika maneno fulani na kuyaongea kwa kurudia rudia kila kwa muda mrefu.
NENO HUUMBA

Ongea maneno hayo, iache hisia ivume, kama ni maneno ya kusikitisha iruhusu hisia ifanye hivyo. Ruhusu hisia itawale.
Ukiendelea hivyo kwa muda utajikuta midomo inaanza kutetemeka tu, wakati mwingine mwili utaanza kutetemeka. Wengine huwa wanahisi umeme unapita kwenye mwili wao. Mwili utakuwa haufanyi kazi tena, huwezi kusikia, huwezi kuona, huwezi kuhisi chochote katika mwili.

Ndipo sasa utaanza kuona, kusikia na kuhisi kupitia viungo vya ulimwengu wa roho. Acha ububunije.

TUTAENDELEA.....
 
NGUVU YA KUTAMKA MANENO

Baada ya kuingia katika ulimwengu wa roho, kile kitakacho kufanya uwe focused ni ile nguvu ya maneno uliyokuwa unayatamka kwa kurudia rudia. Kwamba unapokuwa unafanya chanting "waisrael walikuwa wakitumia neno "ABRACADABRA" yaani "I create as say".

Hata mambo yapo. Ni vyema sasa utakapofika katika hatua hii ujielejeze katika kitu unachokitaka. Maana kuna wengine wanajikuta wameingia katika ulimwengu wa roho hawana hata cha kufanya. Wanaonge tu " laba shanda la bu" Ni kweli umefanya chanting na umeingia katika ulimwengu wa roho, but you don't have mission.

Wengi wanajikuta wanakutana na vitu tofauti tofauti na vinawefanya wafanya vitu vya ajabu. Wengine wanakuwa na uwezo wa utambuzi. Kama nilivyosema hapo awali, WAMEIBUKA WANAOJIITA MANABII ukweli ni kwamba siyo manabii wao ni sawa na wale wapiga RAMLI, kwamba wanauwezo wa utambuzi.

Haya mambo ni kama antenna, pale utakapoamua ku search channel, kulingana na uwezo na aina ya antenna utapata unachokipata. Kuna wengine accidentally wanafungua channel nzuri.

But inakuwa vizuri unaingia katika spiritual world ukiwa na mission.
 
SPELLS NA UCHAWI

Ulimwengu wa roho tunaouingia ni uleule. Wachawi nao wanaingia katika ulimwengu huo. Na unaweza ukaamua, kama unataka kuwa mchawi unaweza kufanya hivyo.

SPELLS
Hapa ni kutamka maneno kwa lengo la kumdhuru mwingine au kumlaani. Watu wadini wanaojua kutembea katika ulimwengu wa roho wanaweza kutumia njia hii kwaajili ya kuwadhuru wengine.

Tunaposema MANENO HUUMBA, hii ni kweli. Wakati MATAKWA NA HISIA vinapoungana katika jambo unalolitamka hutokea kweli kweli.

Soma Book of the Gospel of Thomas
(106) Jesus says:

(1) “When you make the two into one, you will become sons of man.
(2) And when you say ‘Mountain, move away,’ it will move away.”


Anaposema when you make two one, anamaanisha matakwa na hisia vifanye jambo moja.

SIWAFUNDISHI UCHAWI, lakini ndio ukweli ulivyo katika ulimwengu wa roho. Ni uamuzi wako kuamua kuwa mchawi au sio. Wengine ni wale wanaojiita watumishi wa Mungu hutumia njia hizi hizi kuweza kumlaani mtu.

Level ya kuweza kufanya hivi unaweza ukaifikia.
 
Mfungo wa tatu kavu unaendaje nidadavulie tafadhali mkuu
Kwa mfungo mzuri usioweza kuathiri afya nivyema ukawa unachemsha maji asubuhi na jioni na kuweka asali na sukari. Unatumia kikombe kimoja cha chai.

Tenga muda wa kufanya sala na maombi.
Mimi nashauri uweze kuamka saa nane za usiku. Muda huo utakuwa umetulia.
 
Kwa mfungo mzuri usioweza kuathiri afya nivyema ukawa unachemsha maji asubuhi na jioni na kuweka asali na sukari. Unatumia kikombe kimoja cha chai.

Tenga muda wa kufanya sala na maombi.
Mimi nashauri uweze kuamka saa nane za usiku. Muda huo utakuwa umetulia.
Asante mkuu
 
Kwa mfungo mzuri usioweza kuathiri afya nivyema ukawa unachemsha maji asubuhi na jioni na kuweka asali na sukari. Unatumia kikombe kimoja cha chai.

Tenga muda wa kufanya sala na maombi.
Mimi nashauri uweze kuamka saa nane za usiku. Muda huo utakuwa umetulia.
Na SAA Tisa ndo mida ya mkuu wa anga
 
Back
Top Bottom