Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Papaa Muu
Hebu pitia comment kwenye mitandao ya kijamii habari inayomuhusu CAG asilimia zaidi ya 80 watu hawajapendezwa na hichi alichofanya Magufuli hadi wajinga wameamka kwa sasa Rais haaminiki kwa wananchi
This is very very true...!!!
Akili ya kawaid tu haikubaliani na hichi alichofanya Magufuli kwa CAG Prof. Assad. Kumwondoa CAG mwenye kiwango cha elimu ya u-Profesa na kumweka mtu ambaye hana hata Udaktari wa Mahesabu ya Uhasibu/Uchumi unategemea nini kama siyo janja-janja ya kutaka kuendelea kula fedha za walipa kodi wa Tanzania. Rais gani anayepanga Bajeti za mifukoni badala ya kutokana na Bajeti ya Bunge....???!!!Maswali ya kujiuliza ni Ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege Chato na Mbuga ya Burigi vilikuwa kwenye Bajeti gani?Ununuzi wa Bombadier, Dreamliner na Airbus tena kwa Cash zilitengewa Fedha Bunge gani?
Rais anayeamka asubuhi na kuagiza Fedha ya Bajeti iliyotengwa kwa ajili ya Sherehe za Uhuru au chochote yeye anaagiza zikajenge barabara,,,,!!Rais anayetamka kumpa RC Makonda 1.5 B ya kujenga hospitali ya Wilaya ilhali kuna Wizara ya Afya iliyotengewa Bajeti ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha husika....Rais anayetembea na Maburungutu ya Noti akifika mahali anaanza kukagaa mamilioni kwa wahitaji kana kwamba hizo hela zinatoka mfukoni..!!How do you account for that monie? Je, hayo siyo matumizi mabaya ya Fedha na ukiukwaji wa matumizi ya Fedha kulingana na taratibu za kifedha? CAG kama Prof. Assad anapokuja kuhoji madudu kama haya anaambiwa anajifanya muhimili na anaingilia mihimili mingine...nonsense!!!