Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Msaada mara nyingi sana naota nakemea pepo,wachawi,..Yani nasali na kukemea ndotoni ..hii inamaana gani?
Inamaanisha uko thabiti kiroho na moyoni mwako unamcha Mungu kuliko unavyojionesha kwa nje na katu usiwaambie watu wabaya juu ya ndoto kama hizi maana watataka kukudhuru, ushauri kama mazingira unayoishi siyo mazuri(yana inshu za kishirikina) vumilia tu maana huwezi dhurika au unaweza hama kuepuka kero nakwenda pengine.
 
Je, una jambo lolote ambalo limekufanya ukwame kimaisha au uhisi kaugumu fulani kutimiza ama kulitekeleza?
Je, huna kazi, umetingwa na pressure za majukumu au mafanikio ya kazini, unaandamwa na changamoto ngumu kuzitatua au unahisi siku hizi umekaa idle sana?
Chanzo cha ndoto zako kipo ndani ya hayo maswali endapo ukijitathimini vyema kuhusu hali yako kwa sasa ilivyo. Suluhisho lake ni subra na uvumilivu kama kipindi hiko ulivyoweza kuhimili mikikimikiki ya shule na majaribu yake hasa pressure ya mitihani na adhabu, kwan soon yatapita na hali ikishaimarika utashangaa utokaa uote tena ndoto za namna hiyo.
 

Ndoto yako inakulenga wewe kama kikwazo au chanzo cha matatizo yako mwenyewe hivyo angalia unapokosea narekebisha fikra juu ya mambo yanayokukwamisha kupiga hatua.
 
Nikumbukumbu tu za kawaida haina maana yeyote zaidi ya ubongo kurelax unless ikijirudia rudia
 
Mkuu mtarimbo umekula kona ya wapi tena?Tafsiri yako inaeleweka vizuri sana sio ya kubabaisha haina makando makando.

Majibu yako yanarandana na uhalisia kabisa na unajibu vizuri mnoo..yaani unajikuta majibu unayatafuta Mwenyewe sababu unafundisha namna ya kutafsiri rudi tafadhali sisi wanafunzi wako tuko hapa tunakusubiri kwa hamu kubwa naona umetutelekeza.

Kama kuna watu wanakukosoa na kukukasirisha embu wapuuze tafadhali,wana wivu wa kike tu unawasumbua kama wangekuwa wanajua si tungeona hapa wakileta tafsiri nzuri zaidi zinazoeleweka kuliko wewe??

Njoo tafadhali Mkuu Mtarimbo.
 
Ndoto za maji zinajirudia sana kwangu, nimeota nimesimama Nataka kuvuka mto ghafla nikaanza kuona maji yanaongezeka yanajaa.
 
Ndoto za maji zinajirudia sana kwangu, nimeota nimesimama Nataka kuvuka mto ghafla nikaanza kuona maji yanaongezeka yanajaa.
Unaonywa usivuke mto kwa daraja au kuruka (wana wa israel waliyafes maji kwa uwezo wa Mungu)maana neema yako ya mafanikio umefunguka pita kwenye kile unachohofia sijui wewe una plan gan ila unaloliogopa kufanya ndio mafanikio yako yalipo.Mwisho unahitaji msaada wa Mungu sana omba sana
 
Mkuu nami nisaidie kutafsiri ndoto hizi:
1. Juzi kati niliota nimekutana na watu zaidi ya watatu niliosoma nao miaka 15 iliyopita, sura na majina yao havijapotea bado. Tukafurahi na kupiga picha ya pamoja.

2. Rafiki yangu alimpoteza mama yake mwaka jana mwishoni, baada ya miezi 2 kaota ndoto mama yake (marehemu) amepita akiwa ndani ya bus, rafiki yangu kaanza kumuita mama yake amsubiri waondoke nae, mama yake kamkatalia, bus likaondoka.

Asubuhi na mapema kanisimulia, na asubuhi ile alikuwa anasafiri hivyo kapanda gari mwendo wa kama km 1 gari likataka kupata ajali, Mungu ni mkubwa likajikita mahali, wote wakapona[emoji1431]

Je, ndoto hii iliashiria nini??
mtarimbo
 
[mention]mtarimbo [/mention] nina ndugu yangu (baba mkubwa) aliyenilea toka utotoni mpaka ukubwani lakini alifariki toka 2013.

1.Cha ajabu ni miaka imepita sasa lakini mara nyingi nimekuwa nikimuota kwenye ndoto zangu hata usiku wa kuamkia leo nimemuota na mara nyingi naota nipo kwenye nyumba yake ambayo tumekuwa tukiishi na familia yake japo kwa sasa nimeshahama nipo kwangu.

2. kuna kipindi nafikiri mwaka umepita sasa niliota kwamba amerudi licha ya kwamba kwenye hiyo hiyo ndoto ilikuwa inaonesha tulimzika hiyo 2013.

Naomba tafsiri mkuu.
 
Mkuu ukiota huko na marafiki zako wa shule inaleta tafsiri ya kuna watu wako wa karibu ambao umewasahau inabid uanze kujenga nao mahusiano ya karibu maana wamebeba furaha yako ,huwez jua watakupa msaada gani kwenye matatizo yako
 
Kumuona mama ndotoni inamaana gani mkuu


Na kuonana na viongozi wa juu wa taifa inamaana gani mkuu
 
Mkuu ukiota huko na marafiki zako wa shule inaleta tafsiri ya kuna watu wako wa karibu ambao umewasahau inabid uanze kujenga nao mahusiano ya karibu maana wamebeba furaha yako ,huwez jua watakupa msaada gani kwenye matatizo yako

Asante sana, na hiyo ndoto ya 2?
 
AENDE MBELE ZA MUNGU KWANI MUNGU ANAKAA WAPI. TAFSIRI NDOTO SIO MNAVAMIA SIREDI HALAFU MNALETA INJILI HAPA. KWANI MAKANISA HAYAWATOSHI.
 
Kumuona mama ndotoni inamaana gani mkuu


Na kuonana na viongozi wa juu wa taifa inamaana gani mkuu
Kumuona mama ndotoni ina maana kila utakalopanga litanyooka. Kama ni marehemu kuna ujumbe mwema anakujulisha.
 
Safari ni maisha kuna mtu anakuhusu anafanya au anaandamwa na Jambo lisilo jema unashauriwa kumwonya au kumshauri. Japo yaonekana ulishajaribu ukashindwa. Si lazima awe uliyemwona ndotoni ila mna ukaribu.
 
Asante mkuu na vipi kuona viongozi ndotoni mfano rais au pm
Kuona raisi maana yake kuna watu watakumbwa na dhoruba au madhara fulani kama hukumu ya mabaya waliyoyatenda. Wanakuhusu kwa namna moja au nyingine.
 
Kuota moto unaunguza kanzu uliyoivaa kisha unaamua kuivua na unabaki na pensi maana yake nini? ......Na hali ya kuwa wala huwa siyo mpenzi wa kuvaa kanzu
 
Naota Mara nyingi Sana nipo juu ya jengo refu,mnara au mti..,wakati wa kushuka nashindwa ,nilitaka kudondoka tu nastuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…