Mimi niliota nimelala na lijoka design kama cobra hivi, yaani sijui niite ndoto au jinamizi mpaka Leo sielewi, nilienda Arusha nikafika usiku saa 7 nikachukua Guest, kwa uchovu wa ku drive nilivua viatu tu nikapanda kwa bed, sikumbuki kama hata nusu saa ilipita au 1hr maana mara tu nilipoanza usngz wangu nikahisi kama kitu kinateleza pembeni yangu , nikagusa na mkono nikahisi huyu nyoka, nikajishtua ili hiyo ndoto ipotee, hata baada ya kujishtua bado nikahisi nyoka ipo, nikajishtua mara ya pili, lakini bado nikahisi ipo tena safari hii nimeota kobra imeelekeza kichwa chake usoni kwangu, hapo sasa sio tu kujishtua, nilipiga yowe nikaruka, kwa wenge la usiku ule nikakimbilia chooni ambako huwa nina kawaida yakutozima taa ya chooni,.maana mlango ulikuwa wazi, kufika chooni nikaanza kujiuliza maswali, akili yangu moja inasema hilo jinamizi tu, akili nyingine inasema ni nyoka halisi, nimekaa chooni mpaka nikasikia adhana ya saa 11, nikaamua kufuata akili ya kwanza kwamba ni jinamizi nikafungua mlango wa chooni taratibu nikaenda kuwasha taa kuangalia kitandani hamna kitu, nikachungulia mvunguni hamna kitu, nikachukua cm yangu ipo kwa charge maana ningekuwa nayo ninggempigia mwenzangu aliyekuwa chumba kingine, sikulala tena, nikamfuata mwenzangu room yake kufika nae ameshaamka amevaa nguo tayari anasubiri tu kukuche tutoke wakati tuliagana tulale mpaka saa 3 coz tumechoka. Mwenzangu yeye kaota kalala na fles meat ,.yaani anaona midamu tu ya nyama za bucha kitandani, tukahama Guest nyenyewe