Ok mkuu kwanza pole na misiba.ni hivi ukiota chombo cha usafiri wa ardhini kama gari huwa zamani walikua wakiotaga farasi au punda enzi izo magari yalikua hakuna,that why kama we we ni mkristo ukipitia kitabu cha ufunuo utaona sahemu nyingi wanatumia farasi kapandwa ,ingekua now days yohana angeona gari limepandwa.Sasa turudi kwenye mada gari code yake ni kipind au nyakati flani ambazo zimeamriwa juu ya mtu mpaka utakapokufa mfano kuna wakati wa kulia,kucheka,kupata,kupoteza,furaha,majonzi,kufanikiwa,kufilisika,kuumwa... yaan ni nyingi ,ulipoota una magari mawili mapya na yote yakateketea inamaanisha kuna nyakati mbili unazipitia au utazipitia.kuteketea code yake ni uchafu au ovu au isiyofaa au isiyokua na faida.Hapo sasa ukiunganisha unapata jibu kuwa kuna nyakati mbili zitakujia ambazo zitakuhuzunisha au kukurudisha nyuma au kukupa wakati mgumu lakini tumaini lako litabaki kwenye wakati ulionao kwa sasa ,wakati huu unaoupitia inaonesha ndio wakati uliobora kwako KULIKO nyakati zozote zile hivyo unaonywa usichanganye jambo geni kwenye hali ,imani,mtizamo ulionao kwa sasa maana ndio pona yake,simamia ulichonacho usiyumbishwe la sivyo utapata wakati mgumu sana mkuu.
Ndoto za marehemu ziko za aina mbili ambazo ni kuota marehemu unaowafahamu na pili kuota marehemu usiowafahamu
Ndoto ya kuota watu au wapendwa unaowafahamu ambao walikwishafariki , kwanza ujue asilimia kubwa ya binadamu wana roho chafu (hapa simaanishi tabia namaanisha nafsi nyingine) ambazo mtu huyo akifa hutafuta ndugu wa karibu ili wamwingie hivyo kumwota marehemu huwa ni mchezo ambao anakuletea yule roho chafu ili akuzoee ,wengine hadi hufundishwa uchafu,huambiwa mambo ya mbele,hivyo ukiota mtu ambaye amekwishafariki omba kwa Mungu akuepushie mbali hizi roho kumbuka ni za magonjwa,ajali,kujiua,mikosi,ambayo zilikua zikimwandama marehemu mpaka akafariki.Hivyo huwa zikishamwangamiza marehemu hutafuta wa kurithiwa ili ziendelee kuharibu ukoo au familia yote.
Pili ukiota mtu aliyefariki ambaye humjui huwa inamaanisha kuna mambo ambayo unayawaza au umeyapanga ila hayo mambo kama hujui hayawezekani kabisa yakafanyika ni ngumu mno ,yaani kufanikiwa kwake ni haiwezekani labda kwa muujiza wa Mungu