Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Code ya kanisani ni kipi huwavuta watu na kukusanyika pamoja na kuimba kwa imani moja?jibu ni michezo mfano mpira ,hivyo punguza kuangalia sana michezo au usiwe miongoni mwa wenye kufuatilia sana michezo itakusaidia
Nimeota nimekua mlinzi wa Rais Samia, je hii ndoto ina maana gani?
 
Risasi ni mshale kwa zamani ,na mshale unamaanisha mikosi magojwa ,umaskini na megineyo yanayofanana na hayo ,hivyo kuwa makini ikiwezekana ongeza maombi maana kwenye goti ni mbaya ,utakwama ,hutasogea endapo hayo yatakupata ,sali sana bwashee
Mimi niliota nimelala na lijoka design kama cobra hivi, yaani sijui niite ndoto au jinamizi mpaka Leo sielewi, nilienda Arusha nikafika usiku saa 7 nikachukua Guest, kwa uchovu wa ku drive nilivua viatu tu nikapanda kwa bed, sikumbuki kama hata nusu saa ilipita au 1hr maana mara tu nilipoanza usngz wangu nikahisi kama kitu kinateleza pembeni yangu , nikagusa na mkono nikahisi huyu nyoka, nikajishtua ili hiyo ndoto ipotee, hata baada ya kujishtua bado nikahisi nyoka ipo, nikajishtua mara ya pili, lakini bado nikahisi ipo tena safari hii nimeota kobra imeelekeza kichwa chake usoni kwangu, hapo sasa sio tu kujishtua, nilipiga yowe nikaruka, kwa wenge la usiku ule nikakimbilia chooni ambako huwa nina kawaida yakutozima taa ya chooni,.maana mlango ulikuwa wazi, kufika chooni nikaanza kujiuliza maswali, akili yangu moja inasema hilo jinamizi tu, akili nyingine inasema ni nyoka halisi, nimekaa chooni mpaka nikasikia adhana ya saa 11, nikaamua kufuata akili ya kwanza kwamba ni jinamizi nikafungua mlango wa chooni taratibu nikaenda kuwasha taa kuangalia kitandani hamna kitu, nikachungulia mvunguni hamna kitu, nikachukua cm yangu ipo kwa charge maana ningekuwa nayo ninggempigia mwenzangu aliyekuwa chumba kingine, sikulala tena, nikamfuata mwenzangu room yake kufika nae ameshaamka amevaa nguo tayari anasubiri tu kukuche tutoke wakati tuliagana tulale mpaka saa 3 coz tumechoka.

Mwenzangu yeye kaota kalala na flesh meat ,.yaani anaona midamu tu ya nyama za bucha kitandani, tukahama Guest nyenyewe
 
Hayo ni majinamiz tuu mkuu,majinamiz ni roho chafu zisizokua na vikao maalumu hupendelea kuwasumbua watu au kuwachezea ,saa nyingine wanakamata mfumo wa hewa,au wanakuparalize kiaina huku wakikuchezea ,kila ukijitahidi kujitoa unashindwa ,ila uzuri ni kwamba hayana madhara kwa mtu mwenye afya nzuri ,huwa wanabahatisha bahatisha wakikukuta afya mbaya mfano una presha,pumu,tb,au shambulio la moyo unaweza ukafa na ndio lengo lao ,ila ni waoga sana na hawana nguvu mpaka wawe wengi sana.unajua mkuu haya mambo huwa tunapuuzia na kudai ni matokeo ya kulala vibaya,hiyo si kweli ukiwa mtu wa sala haitokei mbona,I hope umenisoma mkuu
 
Kuota unaogelea inakuwaje mkuu
 
Kuota unaogelea inakuwaje mkuu
Ukiota unaogelea inamaanisha una karama ya uongoz au mamlaka flan ya kipekee,aisee hii ndoto kama kweli umeota una kismati mkuu.piga goti Mungu akuongoze.
Nb.Rejea roho ya Mungu ilikua juu ya maji
Yesu au isa bin mariam alitembea juu ya maji.
Piga goti una kitu cha kipekee kinafurukuta ndani yako .
 
Amina ,na iwe hivyo
 
Mi kuna ndoto niliota mara ya kwanza nikaidharau nikaota tena ikanistua kidogo maana ilikuwa kama serious.

Niliota nimepanda chombo baharini sasa wakati nikiwa njiani nilkutana na dhoruba alafu nilivyofika mwishoni nikakuta mifupa ya wanadamu imetapakaa.
 
Pls nitafsirie Ndoto yangu..
Nimeota nipo sehem kuna Miti ya Mauwa ya Roses yanavutia mno halaf Mauwa yamechanua sana.
 
Pls nitafsirie Ndoto yangu..
Nimeota nipo sehem kuna Miti ya Mauwa ya Roses yanavutia mno halaf Mauwa yamechanua sana.
Maua ni nyota njema inayon'gara sana na kutoweka ,hivyo kuna mchongo au zari flan au cheo flan utapata lakin kwa mda ila utumie hicho kipindi kwa uangalifu maana ni kwa mda tuu
 
Maua ni nyota njema inayon'gara sana na kutoweka ,hivyo kuna mchongo au zari flan au cheo flan utapata lakin kwa mda ila utumie hicho kipindi kwa uangalifu maana ni kwa mda tuu
Mkuu namie nifasirie apo juu
 
Ukiota mtu unaemfahamu amefariki, na ukiota mtu alikwisha fariki zamani kua amefariki tena hapo inakuaje
 
Ukiota unaendesha gari
 
Nimeshaota, zaidi ya mara moja, nanunua kahaba kwny danguro huku nikifurahia tu hali hiyo. Hii ina maana gani?!!!!!!!!!!
 
Iyo namba nne naona Ina ukweli flani, ivi.
Je kuota napewa password ya benki, na mzee wangu Alishadead akanipa ATM yake nikatoe ela , ila nikapewa password na ndugu zangu kwamba ni 8?09, kiulizo ni namba nimeisahau
 
Mkuu samahani naomba nikuulize swali...
Tafsiri ya Hizi ndoto unapata wapi...
Ili na mimi nijifunze kutafsiri
 
Usiku wa kuamkia leo nimeota tuko watu wawili tuna vua samaki mahali sio mtoni, bwawani,ziwani au baharini na tukapata samaki mchanganyiko kila mmoja wa kwake aina ya samaki niliyoitambua ni sato, mara kuna gari nadhani la police likaja nikaondoka nalo ila zile samaki niliwaachia nyumbani kama mboga, kuhusu yule niliyekuwa navua nae samaki sikumbuki yeye alielekea wapi
 
Mkuu ukiota unaomba na kukemea mapepo maana yake nini?
Juzi kati hapa niliota niko sehemu karibu na kama bwawa hivi niko na mtoto mdogo ila simfahamu, mara yule mtoto akawa anatusha vitu kama vyungu kwenye lile bwawa vikawa vinavujika, nika vile waganga wanvyovunja nazi, kuna chungu hakikuvunjika vizuri mara yule mtoto akajirusha kwenye lile bwana, akawa anaongelea, ghafra nikaona anajinyoosha na kuwa mtu mzima, akatoka nje, nilipoona vile nikaanza kukemea na kuomba huku nikiita Yesu Yesu nikaonga Kama anashindwa nikaanza kuita Mungu Mungu ghafla akadodoka jini nikawa nimeshinda. Hii inamaana gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…