Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Hii code zake nimejaribu kuziunga zinagoma ,ngoja ntapitia desa moja then ntakupasha see u next week mkuu
 
Kuna mtu ameota yupo chumbani kwake alipolala, mara akaingia kuku kupitia mlango. Alipo amka kumfukuza, ili atoke nje mara paka naye kaingia. Kuku alitoka, ila paka akamtafuta hakumpata. Hiyo ni usiku wa kuamkia jana. Usiku wa kuamkia leo hakumbuki alichoota. Ila mapigo ya moyo yamemwenda mbio sana na kushtuka. Hana amani kabisa. Code ya hiyo ndoto ya kwanza ni ipi mkuu?
 
Ni mwanamke
 
Kuota unavua samaki ni ndoto njema ,samaki anawakilisha pia maarifa ya ulimwengu wa roho that why kama nyota yako ni samaki yaani kama umezaliwa kati ya February 15-march 21 .hivyo ndoto yako inamaanisha katika kutafuta kwako rizki unahitaji umjue sana Mungu,yaani rizki zako zimeunganishwa na ulimwengu wa roho kwa asilimia kubwa sana ,ukijaribu kutumia njia nyingine hutakua salama ndio maana ukaona polis ,ikimaanisha onyo juu yako maana sheria za dunia hazitakuacha salama.Mweke Mungu mbele kwenye kazi au biashara yako la sivyo mkono wa sheria hautakuacha salama mkuu
 
Paka ni mwakilishi wa uchawi na kuku ni tiba ya uchawi so kwenye ndoto inamaanisha kuna mambo mazuri au njia nzuri umeiacha ambayo nilikua vigumu kwa ulimwengu wa Giza kukushambulia sasa umeingia kwenye mambo ambayo yatakuletea shida ,mabalaa na mikosi .Rekebisha ulipokosea mkuu rudi kwenye mstari kabla hawajakuharibia.
 
Mkuu nimejaribu kuchukua muda kukusoma na nimeona kuna sehemu unapitia mule mule hivyo nikakosa cha kukuuliza,kwani niliwahi kuota kusalitiwa na kweli nikafiwa na baba,
Ila Nina ndoto tatu naomba tafsiri zake mbili zimeshajirudia mara nyingi ,ya kwanza:niliwahi kuota nimeunguliwa na magari mawili mapya mpaka yakawa majivu nikabaki na moja la zamani na baadae nikaota tena kuwa nimenunua gari mpya na zoote zikapata ajali na kupoteabkabisa nikarudi to zero ground yaani apeche alolo
Ndoto ya pili huwa naota mara nyingi nachezea kinyesi ktk mitindo tofauti tofauti
Bi mkubwa wangu nilishamzika miaka mingi mno ila nikamuota akiwa hai akaanza kuumwa na kumzika,hii imenitokea Mara moja pekee
Naomba unipe codes zake na nahisi zitanisaidia
 
Shukurani
 
Habari mkuu,
Nina miaka zaidi ya miwili sasa naota ndoto zinazohusiana na maji, either kuna mafuriko napita kwenye hayo maji ila kabla sijavuka ng'ambo ya pili maji yanakuwa yameisha, na ndoto zingine napita sehemu kuna maji mengi sana yanatembea kwa kasi nawaongoza rafikizi zangu au ndugu zangu kuvuka, ndoto nyingine naenda sehemu nakuta hapo napoenda pamezungukwa na maji mengi sana kama bahari. Hizi ndoto huwa zinajirudia sana kwa mwezi naweza kuota hata mara tatu na zaidi. Tafsiri yake nini?
 
Ok mkuu kwanza pole na misiba.ni hivi ukiota chombo cha usafiri wa ardhini kama gari huwa zamani walikua wakiotaga farasi au punda enzi izo magari yalikua hakuna,that why kama we we ni mkristo ukipitia kitabu cha ufunuo utaona sahemu nyingi wanatumia farasi kapandwa ,ingekua now days yohana angeona gari limepandwa.Sasa turudi kwenye mada gari code yake ni kipind au nyakati flani ambazo zimeamriwa juu ya mtu mpaka utakapokufa mfano kuna wakati wa kulia,kucheka,kupata,kupoteza,furaha,majonzi,kufanikiwa,kufilisika,kuumwa... yaan ni nyingi ,ulipoota una magari mawili mapya na yote yakateketea inamaanisha kuna nyakati mbili unazipitia au utazipitia.kuteketea code yake ni uchafu au ovu au isiyofaa au isiyokua na faida.Hapo sasa ukiunganisha unapata jibu kuwa kuna nyakati mbili zitakujia ambazo zitakuhuzunisha au kukurudisha nyuma au kukupa wakati mgumu lakini tumaini lako litabaki kwenye wakati ulionao kwa sasa ,wakati huu unaoupitia inaonesha ndio wakati uliobora kwako KULIKO nyakati zozote zile hivyo unaonywa usichanganye jambo geni kwenye hali ,imani,mtizamo ulionao kwa sasa maana ndio pona yake,simamia ulichonacho usiyumbishwe la sivyo utapata wakati mgumu sana mkuu.

Ndoto za marehemu ziko za aina mbili ambazo ni kuota marehemu unaowafahamu na pili kuota marehemu usiowafahamu

Ndoto ya kuota watu au wapendwa unaowafahamu ambao walikwishafariki , kwanza ujue asilimia kubwa ya binadamu wana roho chafu (hapa simaanishi tabia namaanisha nafsi nyingine) ambazo mtu huyo akifa hutafuta ndugu wa karibu ili wamwingie hivyo kumwota marehemu huwa ni mchezo ambao anakuletea yule roho chafu ili akuzoee ,wengine hadi hufundishwa uchafu,huambiwa mambo ya mbele,hivyo ukiota mtu ambaye amekwishafariki omba kwa Mungu akuepushie mbali hizi roho kumbuka ni za magonjwa,ajali,kujiua,mikosi,ambayo zilikua zikimwandama marehemu mpaka akafariki.Hivyo huwa zikishamwangamiza marehemu hutafuta wa kurithiwa ili ziendelee kuharibu ukoo au familia yote.


Pili ukiota mtu aliyefariki ambaye humjui huwa inamaanisha kuna mambo ambayo unayawaza au umeyapanga ila hayo mambo kama hujui hayawezekani kabisa yakafanyika ni ngumu mno ,yaani kufanikiwa kwake ni haiwezekani labda kwa muujiza wa Mungu
 
Ndoto za maji huwa asilimia kubwa huwa ni za mafanikio,maji code yake ni mafanikio au maarifa au cheo au ukuu inaonesha utapitia kipindi cha mafanikio kwenye mambo yako ,na unatakiwa uwakumbuke ndugu zako pindi ukifanikiwa ,la sivyo ukienda kibinafsi hutafika mbali
 
daah mkuu hii ni kweli kabisa siwezi kusema nimepata mafanikio 100% ila ukilinganisha kipindi cha miaka miwili nyuma na sasa hivi nimepiga hatua na hii ni kutokana na kazi nzuri niliyopata na cheo ambacho ninacho kwa sasa.,,nazidi kuomba Mungu nifanikiwe zaidi
 
Tunashukulu kwa elimu yako ni mawazo yako na hatuwezi kuyapnga .Lakini kwa uhalisia ndoto zimeganyika sehemu kuu mbili.
1.Hisia ya huzuni wakati wakuota
2.Hisia ya furaha wakati wa kuota .

Naomba nitoe ufafanuzi,hisia ya huzuni,Hapa mtu anaota kwa mfano kihisia anakua na huzuni mpaka wengine huamka usingizini wakiwa na machozi kabisa na rohoni wameumia kabisa,kama mtu akiota ndoto hii basi inaashilia Jambo baya litatikea kwake huyo muotaji.

.Hisia ya furaha hapa mtu naota kihisia Hana maumivu kihisia hta kama ni ndoto ya kutisha kiasi gani.mfano waweza ota upo msibani lakini moyoni una amani I mean roho yako Haina huzuni .Hii ndoto manake inaashilia neema .Ni Jambo la heri.

Hitimisho: Ukweli kuhusu ndoto Huwa zipo ndani ya hisia za muotaji na huu ndo ukweli wenyewe msidanganyike ndugu zangu.Je hisia ni za furaha au huzuni basi ndoto itaitafsili kutokana na hisia zikupatazo kipindibunaota.
Asanteni
 
Dah ni kweli. Ndoto zengine unashtuka ukiwa na hofu moyoni, while nyengine unashtuka ukiwa na Furaha ajabu
 
Kuna ndoto huwa zinanitatiza nakujirudia.

Ndoto ya shule(chuo)

Na ndoto miguu kufa ganzi nikitaka kusimama nashindwa. Naona saivi sio miguu miwili tena ni mmoja wakulia najitaidi kusimama unakuwa umekufa ganzi kama umeparalyse napambana mpka nashtuka.
 
Kwa kiasi ninapitia kipindi cha mpito kuliko vipindi vyoote hapo kabla na mengi yamesimama
Je nahii ya kuota kukutanakutana na vinyesi nayo code yake ni nini
 
Em kiongoz na mm nitafsrie hii.. Nliota nko nafanya kaz na marehm baba angu tupo kwenye ofis kama tunatengeneza kitu nn maana ya kuota unaongea na marehm baba ako
 
Hujakosea mkuu ila hujaenda ndani zaidi ,pia inatakiwa ujue kwa nini tunaota ,ni hivi ndoto unazozikumbuka ni asilimia ndogo sana ya ndoto unazoota yaani hazifiki hata 1% ,ni kwamba asilimia 100% ya usingizi hutengenezwa na ndoto.Bila ndoto ubongo utakufa au kuzima hivyo ndoto ni chakula cha ubongo wakati umelala,sasa tuje kwenye ndoto ambazo huleta matokeo,ni hivi ukiona umekumbuka ndoto au umekumbuka uliota ujue kuna signal imenaswa kwenye ulimwengu wa roho kama tahadhari au saa nyingine mwili unatoa signal kwenye ubongo mfano mkojo kujaa kwenye kibofu,kulala vibaya,hizi signal usipozijua inakua tabu zaidi au maradufu unapokumbwa na lile tatizo . ingekua ndoto ni kitu simple kama unavyowaza basi mitume na manabii na vitabu vyote vitakatifu vinatudanganya,haya maisha usiyoyajua ni kwamba yanaendeshwa kwa mahesabu ,hakuna ambalo litakutokea ambalo halikupigiwa mahesabu ,hivyo kwa neema ya Mungu tunanasa mawimbi ya yale yatakayotupata au kutokea mbelen kupitia ndoto ,kama uko advanced unafunuliwa wazi wazi na Mungu,ila sisi wadhambi tunaonyeshwa kupitia ndoto,ni hivi huwezi kuota kitu usichokijua ,au hali usiyoijua material zote zinazotumika kwenye ndoto zinatokana na yale uliyonayo akilini.Mkuu jiongeze acha hulka za kizamani au uzungu mtafute Mungu maadamu uko hai na nguvu iko nyakati utapitia ambazo hutakaa udhanie kama ungekuja kupitia.
 
 
Ndoto ya shule au chuo nimeelezea kwenye mada mkuu.
Kuhusu mguu kufa ganz hayo ni majinamizi kemea tuu ,huwa hawana nguvu ila kama una magonjwa ya moyo,tb,shinikizo hawa majinamiz yanaweza yakakusababishia kifo ,omba kabla hujajipumzisha
 
Nisaidie hii,

Mimi ni mwalimu,

Miaka mitatu iliyopita niliota nimeokota madini ya thamani kubwa njiani wakati narudi kutoka shule ninayofundisha ambayo ipo pembezoni mwa mji. Madini hayo yalikuwa yanalindwa na nyoka mkubwa wa brown lakini sikumbuki kama alinidhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…