Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Mambo ya kuendekeza ndoto naonaga ni upuuzi tu unaweza hata kuugua wazimu ukiyaendekeza hata nikiota nazikwa I dont give a fu**
 
Kuna jambo la aibu linakukabili katika maisha yako mostly ni kukosa kazi au kujihisi umekwama kimaisha at the moment nakuishia kulala au kuwaza muda wote ukiwa na uwalakini maisha yataendeleaje please usiumize sana ndonga mitihani yote utaishinda.
 
Mkuu habari Mimi huwa naota nimekunja miguu napaa hewani kunakundi lawatu linanikimbiza hao watu siwa jui.huwa wananikimbiza hawanikamati Ila wao hawapai angani Mimi tuu ndo huwa napaa nikiwa nimekunja miguu.
Kuna jambo unalikwepa na utaki kuliweka wazi hivyo katika fikra zako unajaribu kutoroka japo linasumbua saikolojia yako tafakari ni kipi kinakupa wakati mgumu nafunguka usaidiwe
 
Kuota unakula nyama yeyote kwenye ndoto ni ishara ya mikosi nakulingana na ndoto yako kuna mazingira ya usaliti hivyo kuwa makini
 
Ndoto zote ulizoota hazina maana yeyote kubwa zaidi ya kuna mambo unatamani ungekuwa na uwezo yangefanyika lakini ndo hivyo haiwezekani
 
Niliota tunachimba Kaburi pembeni ya kaburi la Ndugu yangu, halafu nikakutana na Mifupa ya Ndugu yangu inaporomokea kwenye Kaburi tunalochimba la karibu.
Naomba tafsiri yake Mkuu!

Mpaka leo inanitesa maana ilinistua saana.
Lengo la kuchimba nikuzika, nakuzika jambo lolote nikulisahau hivyo wakati huko mzima sasa usisahau kuwa kuna mema wapaswa kumtendea marehemu mf. kama alikuwa na familia tafadhali ijali na utoe msaada au kama akuwa na familia mtembelee japo kaburini kwake kumjulia hali.
 
Niliota nimepata ajali ya gari nikatoka salama,nikaona gari inaendelea kunguruma ikiwa chini nikaenda kuizima nilipo lizima hapo hapo likawaka moto hii inamaana gani.maana kweli natumia gari kila siku.
Inaweza isiwe na maana kubwa zaidi ya kuota mawazo au hisia zako mwenyew juu ya hofu uliyonayo kila siku kuhusiana na ajali au chombo chako
 
Bliss ni ishara ya kipindi cha amani ya nafsi na huna kinachokukwaza moyoni kwa sasa hivyo endelea kufurahia kile ambacho maisha yanakuzawadia.
 
Vipi na ndoto za kupanda milima Hadi juu, au kuota mlima mrefu na theluji yake?
Unapitia kipindi cha mpito wa sintofahamu ya kimaisha/ugumu ila bahati nzuri una-ambitions kubwa na hakika utakwea na kufikia kwenye kilele cha mafanikio
 
Mimi nimeota mwanamke niliyeachana nae ndio mpenzi wangu kwa kipindI hiki lakini ana mwanaume mwingine ikafikia kipindi akaniacha akapata nae mtoto je hii ina maana gani
Inamaanisha achana na mambo yaliopita hayatokusaidia zaidi ya kukusababishia machungu, hivyo ishi maisha yako
 

Unakumbushwa kuwa kila unachokifanya kiwe kizuri au kibaya ukurudia vilevile hivyo ishi kwa upendo na epuka ubaya
 
Tafsiri ya madini ni thamani na nyoka huwa ni adui hivyo kuokota madini nikupata thamani au kibali mbele ya watesi wako ambao hawali walikuchukulia ndivyo sivyo na pia ni ishara ya mambo yako kukunyookea au kufanikiwa.
 

Kuna mambo marehemu anahisi hatia kuwa akuyatenda ipasavyo kipindi cha uhai wake na hivyo angetamani kama angepewa nafasi angeyarekebisha, huu ni ujumbe kwako kuwa mission yake anataka uikamilishe wewe na siyo kumuhukumu, ebu jaribu kuangalia maeneo haliyofeli marehemu kudeliver iwe nikutoa msaada, kusimamia majukumu yakifamilia n.k hili wewe uweze kuyarekebisha hayo katika maisha yako ya sasa.
 

Kumwota ng'ombe kibiblical ni ishara ya kipindi cha neema hasa akiwa kanawiri au mwenye maziwa mengi yaani ishara ya shibe, kwa tafsiri ya ndoto zako ni kuwa utapata utajiri mbeleni ambao bado ujajiandaa vyema kuwa nao ndiyo maana unajiuliza na huyu ndama umweke wapi, hivyo andaa uelekeo au palilia vyema njia yako kama ni kazi fanya kwa bidii nawe mbeleni utakula mema ya nchi.
 
Maji ni ishara ya hisia zako mwenyewe hivyo jaribu kuzikabili hisia zako ambazo pengine ukutia woga au hofu au huzuni nakuwa kikwazo cha kufanikiwa mambo mengi maishani mwako hivyo jiamini na uishi kwa furaha.
 
Habari wakuu,

Kabla sijalala nilimuomba MUNGU anifunulie jambo fulani kupitia ndoto, sasa nilipolala nimeota Niko na kaka yangu namsindikiza safari akanipa dumu/galoni limejaa divai/whine nikawa nakunywa kwa kulimiminia mdomoni huku tukiendelea kupiga story. Itakuwa na maana gani?
 
Unaroho wa kufeli kimaisha in whatever you are doing is doomed to fail, hivyo ushauri wangu zidisha maombi na acha dhambi au kiri tokea moyoni kwa kutubu na kujivua roho chafu ulizojivika au kuvikwa na watu waovu na utokaa ukwame tena kimaisha na wala kuota ndoto hizo
 
Una upendo pure kwa familia yenu na wao pia wanakupenda hivyo mnatakiana mafanikio au mnaombeana mema kila siku kwa Mungu hivyo ni ishara njema.
 
Ukiota unaendesha gari
Tafsiri yake ni kuwa ukiota safari yeyote uwakilisha maisha, barabara ikionekana ni ishara ya njia utakayopitia au unayopitia na gari ni wewe hivyo kama wewe ndo dereva ina maana nzuri kuwa wewe ndiye kiongozi au mwenye maamuzi juu ya maisha yako mwenyewe kama mshika usukani, lakini ukijiona ni abiria jua kuna mtu ndiye anayecontrol maisha yako.

Lakini kama huwa unatamani kuendesha gari na hujui kuendesha katika maisha ya kawaida pengine ni roho inajaribu kukupa ishara ya matumaini kuwa siyo muda mrefu katika maisha yako utapata nafasi hiyo.
 
Hapo kwa Magu nadhani umechomekea kutest kina cha maji!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…