Siri ya Furaha ya ndoa ni kuishi wanandoa kama marafiki (washkaji) wawili

Ndoa ni unnatural. Ipo against nature ya binadamu lakini acha nikae kimya na upendo feki wa wanandoa utamalaki kwenye hili jukwaa.
Mkuu hapa ni jamii huru,sisi ni watu huru,unaweza kuweka hoja mezani tukaijadili ili tujifunze zaidi.
 
Ni muda ambao mtoto anakamilisha hatua za ukuaji wake kuanzia kulala,kunyonya,kukaa,kutembelea tumbo,kutambaa,kusimama,kutembea mpaka kukimbia na kuongea maneno kadhaa.

Kumbe ni umri wa honeymoon, Hongera lakini. Basi tuombeane uzima tuzidi kujifunza mitano tena😅😅
 

Kwahyo wazaz kuuliza anafanya kazi gani ni kosa?
 
Hiyo sentensi ya mwisho imenichekesha sana...

Kweli kabisa unapoishi na mwenzi wako kirafiki unakuwa huru sana hata kuachia ushuzi mnapokuwa pamoja faraghani wala si issue kabisa.. yani mnaishia kuchekana tu
Mi kunijambia hapana asee[emoji57][emoji57][emoji57]

Ni mojawapo ya tabia chafu
 
Yaani ninavyoishi na mke wangu aisee naomba Mungu asiruhusu ibilisi kupita katikati hakika tutazeeka amoja.

Mtoa mada upo sahihi kabisa,maisha ya ndoa mkiishi kama marafiki maisha yapo simpo sana.
Tunataniana muda mwingi,na wakati wa kuwa serious tukiwa tunaongea pamoja mambo mhimu tunakuwa serious.Mke wangu ni mpole sana,mcheshi sana hajui kubishana na mume,hajui kujibu vibaya akiona una hasira pengine umevurugwa na mtu au kazini anakuuliza kwa upole sana na hupenda kusema "pole mume wangu","msamehe tu mume wangu"

Aisee huyu mwanamke naona Mungu ameamua kunipa kama zawadi,kwa miaka yote 8 niliyoishi naye sijawahi kumtilia mashaka kabisa kuhusu kuchepuka,sijawahi kuona hata sms yenye ukakasi simu zetu zipo huru sana kila mtu anashika simu ya mwenzake bila hiyana.
Maisha yetu ni sawa na mtu na mdogo wake maisha simple tu siyo masheria na masharti sharti yasiyo na umhimu wowote.

Nikisikia watu wanalalamikia mabalaa ya ndoa huwa nasikitika sana.
Hata ikitokea nikapewa nafasi ya kuoa upya mwanamke ninayemta bado nitamuoa tena mke wangu.

"Ngono ni kipengere kidogo sana kwenye ndoa"
 
Mnaposema mwanamke bila hela sijui huwa mna maanisha nini hasa?kwamba utafute pesa ili umpe mwanamke?
Pesa inahitajika siyo ili ikuletee mwanamke au umpe mwanamke umtawale laa hasha.
Pesa inatafutwa kila siku mpaka mwisho wa uhai wako,pesa ni kama chakula yaani unatakiwa kula kila siku,kuvaa kila siku,kunywa kila siku n.k na kutafuta pesa ni hivyo kwa sababu ili ule,unywe,uvae n.k unatakiwa kutoa hela ili upate huduma.

Hivyo pesa siyo mjadala wa kwamba itafutwe au laa ni automatic,ingekuwa pesa ndiyo dawa pekee ya wanawake wenye pesa kiduchu basi wasingekuwa na wanawake kabisa na wenye pesa nyingi basi mahusiano yao yangekuwa na furaha maradufu lakini cha ajabu changamoto za ndoa unazikuta kotekote kwa wenye hela nyingi na kwa wenye hela kidogo(hakuna asiye na hela)
 
Hahahaaa uttoh2002 sasa unawekaje urafiki na mtu kakutoa kwenu unakula vizuri halafu anakuja kukutesa na njaa lakini?

Hapo ndio utajua mahari kabla ya ndoa ni moja ya vipimo vya kujua kama muoaji ana muwezo wa kutunza mke[emoji23][emoji23][emoji23]
Hapo kwenye mahari kuwa kipimo nakupinga dada,mahari mara nyingi huwa ina halalisha utumwa kwa mwanamke yaani mentality inakuwa kana kwamba umemnunua mwanamke,
Kipindi naoa sikuwa na pesa ya kutosha kuweza kugharamia shughuli za harusi,wala mahari mfukoni nilikuwa na laki tano tu na nilihitaji kuoa kwa namna yeyote ile,bahati nzuri mwanamke naye ni kama alihitaji mwanaume aliye serious na maisha (ndoa)
Tulifahamiana kwa wiki mbili tu na ya tatu tukaoana.

Mchanganuoa wa 500k
Sikutoa mahari nilinunua pea mbili za vitenge 70k kwa ajili ya mama,kitambaa cha suti 35k
Kitenge pea moja 25k kwa ajili ya Bibi.
Mama mkwe nilimpa 50k na baba mkwe 50k
Mke wangu nilimshonea gauni la 60k ili apendeze siku ya kunitamburisha kwao.
Mimi nilivaa nguo zangu tu za siku zote.

Nilitafuta jamaa yangu tukaenda kujitamburisha,tulipokelewa vizuri nilipomaliza kujitamburisha nilitoa zawadi zangu kwa wazazi,nikaomba wanipe mke mahari nitatoa baada ya miezi 6,walikubali na wakatubariki kabisa kwamba tukaishi pamoja,binti alikuwa Islamic na alitamani angalau tuoane kwa ndoa japo ya mkeka ili kujihararisha kabisa,tukampanga shekh akakubali na shughuli ikaisha,kwa kuwa huozeshwi bila mahari binti alitaka mahari ya 5k tu hakutaka mambo mengi.

Tunaenda mwaka wa 9 huu maisha mazuri,amani furaha na upendo.

Baada ya miezi 7 ndiyo nilipeleka zawadi kwa wazazi,ni zawadi kwa sababu nilishatoa mahari 5k msikitini.
Sasa wazazi wangetumia kigezo chako cha mahari kama kielelezo cha uwajibikaji si ningekosa mke,na mwanamke wangu angekosa mume bora kbs.
 
Hiyo sentensi ya mwisho imenichekesha sana...

Kweli kabisa unapoishi na mwenzi wako kirafiki unakuwa huru sana hata kuachia ushuzi mnapokuwa pamoja faraghani wala si issue kabisa.. yani mnaishia kuchekana tu
Yes[emoji13][emoji13][emoji119][emoji119]
 
Wow nimewapenda buree, how i wish too🙏 ni raha sana kuwa na mtu mnayependana na ni rafiki, mnakua free hata kukosoana bila kuhofia amani kutoweka, maana ni marafiki mkiongea yanaisha and life goes on.
 
SUPPORTED
GOOD
 
Mkeo ni rafiki yako, swahiba wako, bibi yako, dada yako, daktari(muuguzi) mkeo ni lia kitu, kasoro tu hawezi kuwa MAMA yako.
Ukiishi nae hivyo tegemea mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…