OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 5,315
- 13,269
Wakuu salama!
Kuna ukweli mmoja mkubwa sana ambao mahasla wengi huwa tunaufeli. Mara nyingi tunakimbilia kusoma historia za biashara zilizofanikiwa (kama akina Mo Dewji au GSM). Lakini ukweli ni kwamba, ukitaka kujua changamoto halisi za soko, usisome waliofanikiwa nenda kasome biashara zilizofeli na kufungwa!
Hebu tuchukue mfano wa madaktari wa MBBS (Bachelor of Medicine and Bachelor of Surgery). Katika mwaka wao wa kwanza chuo, kabla hawajaruhusiwa kumgusa au kumtibu binadamu aliye hai, wanatakiwa kwenda maabara na kusoma mwili wa mtu aliyekufa (Cadaver/Maiti).
Kwanini wanafanya hivi?
1. Kujua viungo vilivyoaribika: Mwanafunzi wa MBBS anakata maiti ili aone mishipa, nyama, na jinsi ugonjwa ulivyoharibu mwili. Hawawezi kukata mtu mzima aliye hai kujifunzia!
2. Kujifunza kuzuia kifo: Ukijua kilichomua yule wa kwanza, inakuwa rahisi kumuokoa yule aliye hai wodini.
Hii ndio Anatomy ya Biashara. Ukisoma biashara iliyokufa, utajua wapi walikosea
Kusoma biashara iliyofanikiwa pekee kunakupa upofu (Survivorship Bias). Unaona utajiri lakini huoni mitego ya njiani. Kujifunza kutoka kwa biashara zilizofeli ni kupata darasa la bure kutoka kwa "Mwalimu Aliyenyamaza" (The Silent Teacher).
Bill Gates, Marc zuckerberg, Elon musk, Bakhresa mtu yeyote akitaka kujifunza biashara hukimbilia kusoma historia za hawa watu ambao hawawezi kukuonyesha rangi halisi ya biashara.
Ktk sekta yeyote jambo lolote mtaani ukitaka kulifanya vyema jifunze kwa waliofeli na sio waliotoboa.
Pinga kwa hoja
Nawasilisha.