Na siyo hivyo tu Malkia Elizabeth anayemchanganya huyu mwandishi mzushi ni wa kanisa la Anglikan, au ndiyo amemchomekea hiyo Uskochi kulazimisha uhusiano na ukatoliki?.
Soma historia fupi ya uasi wa jeshi wa mwaka 1964 ili upevuke kiakili na kimwili ewe kizazi cha nyoka,
Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say
Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi...Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo,hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia.Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona....Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha,inasemekana Maficho yao yalikuwa Kigamboni.Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.
Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu,askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.
Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta. Walifanikiwa kutuliza maasi yale, na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi, ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wananuheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.
Ukitaka kupata mambo mengi kuhusu maasi yale pitia kitabu "Dar Mutiny Of 1964" by Christopher MacRae