Siri ya Pinda kuongezwa kwenye ‘Kikosi Kazi’ ni wajumbe kuelemewa na hoja ya Katiba Mpya

Upo sahihi, kwanini asiwaingize watu kama Pro Assad na Jaji Warioba kama kweli ana nia ya dhati?
Hawawezi kuwaweka watu ambao ni free thinkers. Makamu wa Kwanza wa Rais ZNZ alikuwa Attorney General wa SMZ wakati wa mchakato wa Katiba Mpya ya Warioba, aliwaumbua SMZ kwenye Bunge la Katiba mpaka akafukuzwa na kazi! Wanajua, ukiweka radicals utapata radical ideas.
 
Kazi ya kikosi kazi ni kukusanya maoni sasa wanaelemewa vipi na hoja wakati hakuna wa kuwauliza maswali.
Hahaaa, labda Kikosi Kazi kiliingia na majibu yake kimekuta paper imebadilishwa.
 
Kama hivyo basi mama kafanya vyema kabisa. Kapeleka ataekwamua walipokwama.

Tatizo ni nini kwa pinda kuongezwa kwa hekima zake?
 
Kama hivyo basi mama kafanya vyema kabisa. Kapeleka ataekwamua walipokwama.

Tatizo ni nini kwa pinda kuongezwa kwa hekima zake?
Huyu ndiye aliyesema Zanzibar siyo nchi je alikwamua au aliongeza matatizo zaidi na je ulikubaliana naye kuwa Zanzibar siyo nchi?
 
Sasa mtu kama Pinda anaushawishi gani huyu kwa jamii?
Kwa wanaomjua vizuri wanajua yeye ni nani na ushawishi wake ni mkubwa Kwa kiwango gani.Ushawishi ni zaidi ya kuwashawishi tu watu.
 
Suala la KATIBA MPYA hata Aje Rais Mstaafu haliepukiki PINDA hawezi kuzuia Matakwa ya Wananchi Pinda atake asitake Maoni yetu lazima Yaheshimiwe

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Wewe umeshahojiwa na hicho kikosi shikizi?
 
Kwa Pinda watakua wamekosea Sana kwa Sababu yeye mwenyewe anataka katiba mpya kwa nguvu Zote.
 
Kwa wanaomjua vizuri wanajua yeye ni nani na ushawishi wake ni mkubwa Kwa kiwango gani.Ushawishi ni zaidi ya kuwashawishi tu watu.
Asiposhawishi watu atakuwa anashawishi kitu gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…