Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 116
- 260
Na Chacha Wangwe Jr
Maelfu ya watanzania wanaojitokeza kumlaki Rais Samia Suluhu Hassan katika ziara yake Mikoani ni jambo la kuvutia lakini inapaswa ieleweke kuwa haya ni matokeo ya uchapakazi wake. Tuangazie mambo machache yanayopelekea Rais Samia kupendwa sana Mkoani Kigoma na Kagera;
1. Katika kipindi cha kuanzia April 2022 hadi Octoba 2022, serikali imeweza kuzindua miradi ya maendeleo ipatayo 1293 inayogharimu fedha za walipa kodi zaidi ya Bilioni 650. Mikoa ya Kagera na Kigoma ni sehemu ya wanafaika wa miradi hii inayolenga kustawisha maisha ya wananchi.
2. Ahadi yake ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa Hospitali ya kanda, Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Burugo, Kituo kikubwa cha Umeme Mpomvu, na kiwanda cha kusafisha dhahabu Geita.
3. Kwa kipekee ahadi yake ya kuhakikisha watanzania wote wanapata umeme wa uhakika kwa kuzindua miradi sita ya umeme na kwa mara ya kwanza kuzima majenerata na kuiunganisha Kigoma katika gridi ya Taifa ambapo wananchi zaidi ya 10,000 watapata umeme wa uhakika.
4. Miradi inayogusa wananchi moja kwa moja kama vile Skimu ya maji Kakonko, Uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya Kakonko, uzinduzi wa Barabara ya Kabingo yenye urefu wa takribani KM 50 iliyojengwa kwa kiwango cha lami na Barabara ya kidahwe yenye urefu wa KM 63 nayo pia ikiwa imejengwa kwa kiwango cha lami.
5. Kwa kipekee Rais Samia ametekeleza ahadi kwa wanakigoma kwa kuzindua Jengo la wagonjwa wa dharura (EMD). Hospitali ya Rufaa ya Maweni Kigoma inaendelea kuboreshwa kwa kasi ambapo mpaka sasa inaweza kutoa huduma za CT SCAN na hivyo kuepusha wagonjwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.
Licha ya mambo mengi yanayowagusa wananchi wa kawaida kama vile ruzuku ya mbolea kwa wakulima, Elimu bure, Mikopo ya wanafunzi, mpango wa BIMA kwa wote, Rais Samia anaendelea kutekeleza miradi muhimu itayo huisha uchumi wa Kigoma na Mikoa ya jirani kwa kutoa fedha za uboreshaji wa Bandari zilizomo Mkoani Kigoma.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU
#SisiTumekubali #MamaYukokazini