Sirro: Sitosahau Askari walipopigwa risasi Kibiti

Sirro: Sitosahau Askari walipopigwa risasi Kibiti

IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro baada ya kuagwa rasmi na Jeshi la Polisi leo Dar es salaam amesimulia tukio ambalo hatolisahau akiwa kazini ambalo amesema ni la Askari Polisi kupigwa risasi na Majambazi baada ya kushambulia kwa risasi gari la Polisi katika Kijiji cha Uchembe, Kata ya Mjawa Wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani.

Sirro amesema “Tuliwapata Wahusika na bahati mbaya na wao walishatangulia mbele ya haki, hili ni tukio ambalo sitolisahau, ukienda ukakuta Askari tisa wote wamepigwa risasi wamelala sio jambo dogo”
Mnafiq na muuaji mkubwa huyu
 
Askari walikuwa wanaenda/wanatoka kwenye lindo walikuwa kwenye difenda la polisi ndipo mdunguaji akampiga risasi dereva wakati gari lipo kwenye mwendo likapinduka askari wakajeruhiwa ndipo walipovamiwa pale na kuanza kupigwa risasi kwa ukaribu zaidi ila kuna askari mmoja alipona baada ya kujifanya amefariki baada ya wale wadunguaji kuwafikia pale chini, hii ilikuwa kibiti miaka ya nyuma kidogo.
Nafikiri askari aliyepona alikuwa mwanamke na wale majamaa yalikuwa yanauwa askari wanaume tu, yule wa kike walimuacha makusudi kwa maelezo ya yule askari wa kike kama kumbukumbu zangu zipo sawa
 
Pongezi kwake siro kwa kuzima ugaidi kibiti.hakuna hata mmoja aliyemuuliza kuhusu kuibiwa billioni 4 za mfuko wa kufa na kuzikana wa polisi?maana yeye atakuwa anajua zaid.
 
Asili ya kupigwa risasi kwa mkupuo ilikuwa ninini?
Ina maana wote tisa walikuwa off guard?
Waliowaua hao askari nao walikufaje wote?
Maswali ni mengi
Hata kama siwapendi Polisi lakini unyama uliofanywa na kundi lile la Wapuuzi Kwa kupiga risasi dereva gari likiwa kwenye mwendo na lilipopinduka wakawafuata waliosalimika na kiwapiga risasi hakivumiliki. Kama Polisi nao waliwaua ni halali yao.
 
Na asisahau kwenda kutubu kwa Mola wake, jeshi la police sio mahakama, why hakuwakamata na kuwapeleka kwa court?,IGPsirro umeonyesha ni mtu wa visasi na usiyefuata sheria, unakumbuka ya police wako what's about Azory?,au hujui naye alipotea kwenye mazingira tatanishi wakati wa issue hiyo?,Akwilina naye huna taarifa naye na hujutiii na hujui, kama wewe sio member wa royal families, utakufa kibudu!honestly kodi yangu imetumika vibaya kukununulia wewe gari, peleka hiyo gari kwenye charity
 
Tuliwapata Wahusika na bahati mbaya na wao walishatangulia mbele ya haki
If you can underline those words "bahati mbaya"
Bahati mbaya= risasi za mgongoni!

We tumekusamehe haya kimbia!

Ukikimbia unakula chuma za mgongoni yaani uuwe askari halafu ukamatwe ubaki hai hiyo haipo!

Mbona jibu rahisi tu!

Labda swali ni je waliouwawa ni kweli ndio wale walioua askari?
 
IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro baada ya kuagwa rasmi na Jeshi la Polisi leo Dar es salaam amesimulia tukio ambalo hatolisahau akiwa kazini ambalo amesema ni la Askari Polisi kupigwa risasi na Majambazi baada ya kushambulia kwa risasi gari la Polisi katika Kijiji cha Uchembe, Kata ya Mjawa Wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani.

Sirro amesema “Tuliwapata Wahusika na bahati mbaya na wao walishatangulia mbele ya haki, hili ni tukio ambalo sitolisahau, ukienda ukakuta Askari tisa wote wamepigwa risasi wamelala sio jambo dogo”
Tz kuna majeshi mengi, Jeshi la Ulinzi (JWTZ)/JKT, Jeshi la Magereza, Jeshi la Uhamiaji, Jeshi la Wanyama-pori, n.k., n.k.
Je, Ni kwa nini ambush ya kuuawa iwe kwa Askari Polisi tu pekee?!???
1.Askari Polisi wa Staki Shari Dsm walivamiwa kituoni Kisha wakauawa,
2.Askari Polisi wa Kituo cha Mkuranga walivamiwa kisha waliuawa kadhaa.
3.Hamza Mohamed alivamia kibanda cha Askari Polisi karibu na Ubalozi wa Ufaransa Kisha akaua Askari wote waliokuwapo kwenye kibanda kabla hajauawa. Matukio ya kuvamiwa ni mengi sana kuwahusu Askari Polisi, Why Always Police Officers?? Why???
Tafakari!! Chukua Hatua!!
 
Bahati mbaya= risasi za mgongoni!

We tumekusamehe haya kimbia!

Ukikimbia unakula chuma za mgongoni yaani uuwe askari halafu ukamatwe ubaki hai hiyo haipo!

Mbona jibu rahisi tu!

Labda swali ni je waliouwawa ni kweli ndio wale walioua askari?
Labda swali ni je waliouwawa ni kweli ndio wale walioua askari?[emoji419][emoji375]
 
Back
Top Bottom