Sisi ambao hatutekwi na Wahubiri Waongo wa Miujiza ndiyo hatuna Akili au waliotekwa nao ndiyo hawana kabisa Akili?

Unataka RC wawape fedha? RC wana huduma nyingi bota haya vyuo na shuke nzuri. Kama umeshindwa kutumia hizo huduma shauri lako. Umaskini sio kulalamikia kanisa, ni ww binafsi au mtu binafsi tu.
 
Na kinachotuunganisha na Mungu ni Roho zetu hivyo ilitakiwa roho ya aliyepona imushukuru Mungu na siyo kwenda kupeleka pesa kumlipa Mungu.
 
Unataka RC wawape fedha? RC wana huduma nyingi bota haya vyuo na shuke nzuri. Kama umeshindwa kutumia hizo huduma shauri lako. Umaskini sio kulalamikia kanisa, ni ww binafsi au mtu binafsi tu.
Niambie wewe ukienda Kwenye hizo huduma huwa unaenda Kama Muumini wa RC au unaenda Kama Mpagani tu mwingine. Je unatambulika Hapo kama Muumini wao !?

Unaambiwa hii shule imejengwa kwa Sadaka na Michango ya Waumini wa Kanisa. Je huduma gani huwa unazipata kama Muumini wao au wanaku treat kama Mpagani tu
 
Wewe habari ya Sodoma na Gomora unaiamini, lakini habari za Biblia huziamini, wala Maandiko huyaamini. Kigezo gani unatumia kuchuja kwamba hili uliamini na haya mengine si ya kweli? Unamwamini Bwana Yesu Kristo?


 
Nilikuwa najiona kuwa labda nipo peke yangu mwenye ufahamu huu na kujitambua, kumbe tupo wengi. Ukiwaangalia watu wanavyopurukushwa sadaka hadi unawahurumia na kujazwa matango pori vichwani.
Tunaojielewa tupo.

Tofauti ya mlokole na mkatoliki ni moja tu:mmoja anampelekea mtanzania mwenzake hela na jasho lake hapa hapa bongo,wakati mwingine anampeleka hela na jasho lake mzungu aliyepo kule vatican anayeitwa Papa.
 
We jamaa una hoja dhaifu sana. Kwanza nikuulize kama ulishawahi kusali RC?? Na kujua taratibu zao walau kidogo.

Kama hujawahi kusali wala kujua taratibu za RC basi ni kheri ukakaa kimya upate kujua.
Kwanza unapotoa sadaka pale haiwi ya padre wala katekista!! Ile ni moja kwa moja jimboni kupangiwa matumizi.
Na matumizi yenyewe ni pamoja na kuwatunza hao wanaowalisha neno, hata ukiwa mbwinde huko basi parokia iliyo karibu na nyie itajitahidi iwezavyo padri walau awe anafika kila wiki kigangoni kwenu kusalisha.

Anapoondoka wala hamumlipi kwa huduma yake, wala hamumjazii mafuta kwwnye gari yake hata kama sadaka yenu mmetoa buku hiyo ndo itaenda jimboni kuungana na nyingine ili Neno liendelee kuhubiriwa.

Hiyo michango ya kujenga kanisa sio ya mtu mmoja, hatokei mtu akataka gari basi achangiwe, sijui mtu kaamka na wazo mchungaji anahitaji nyumba basi mnachanga tu.

Kubali kataa kuna utofauti mkubwa sana juu ya uendeshaji wa makanisa ya kilokole na katoliki yani utofauti mkubwa mno.
 
Wewe ndio ujiulize hapo kuna Mifumo miwili.

Mmoja Unataratibu wa kufuata System -RC
Mmoja hauna Utaratibu wa kufuata System-Walokole

Ila Wote wanachuma Sadaka na Kuziweka mahali kwa Matumizi yao Binafsi. Mmoja anarudisha Kidogo kukuadaa akili ili uzidi kumwamini ila mmoja Anafanya Moja Kwa Moja Bila Kukuaadaa sana.

RC lina Miaka Mingi Kwahiyo Linajua Akili yako vizuri ni kama Vile Benki zilivyoanzishwa. Usidhani zilianzishwa ili zikutunzie Pesa tu ww umekaa Nyumbani eti pesa zangu zipo salama. Unajidanganya Kama unavyojidanganya Mifumo ya RC inavyofanyia kazi sadaka zako na Michango yako.

Nenda Jimbo lolote uone michango ya Kununulia Magari Ma Paroko zinatoka Wapi. Kama si waumini wanachanga mil 30 ya kununua Prado ya Paroko
 
Hivi ukiacha ahadi ya kwenda mbinguni ukifa na kuombewa maombi ambayo nayo ni lazima uyasindikize kwa sadaka yako,kuna kipi kingine ambacho kanisa linakupa?
 
Wana huduma nzuri sana kuliko za dhehebu la SDA nililokulia kwalo mimi. Huduma mara nyingi ni five stars kabisa. Na mimi sio member wao, ila wako vizuri sababu hawabagui. Madhehebu mengu yanabagua sana. Ww acha kutegemea dhehebu likutoe katika umaskini. Binafsi nilizaliwa maskini sana ila sasa nina kila kitu nilichokitaka maishani. Ila hakuna serikali wala dhehebu imenipatia. Nimepambana. Acha mambo ya ajabu mkuu wangu.
 
Tunaojielewa tupo.

Tofauti ya mlokole na mkatoliki ni moja tu:mmoja anampelekea mtanzania mwenzake hela na jasho lake hapa hapa bongo,wakati mwingine anampeleka hela na jasho lake mzungu aliyepo kule vatican anayeitwa Papa.
Umeeleweka sentensi yako short and clear, direct to the point hakuna kupepesa macho
 
Inabidi wengine waende kuwaungisha tu tusipoenda wote.. hapatanoga wakuu.. waacheni wainjoy
 
Msikilize huyu jamaa then nenda you tube umtafute ndipo utajua Mwomposa ni nani
 

Attachments

  • VID-20220119-WA0000.mp4
    8.9 MB
Umeenda nje ya swali nililokuuliza
 
Najiuliza kwa nn hawa wanaojiita "manabii" wamejazana mujini daslam tu??? Mbona huku kwetu mwanza kijiji cha nsumbugu hakuna hata nabii mmoja au watu wa dar ndo wanahtaji kuhubiriwa ila sisi huku kijjn hatufai kuletewa hlo neno?

[emoji3][emoji3]Anyway nahs daslamu ndo kunawalipa zaidi maana wanaume wa dar ukiwaambia utawaombea ili wapate nguv za kiume bas watajazana kanisan mpaka wakanyagane

Wanawake wanajazana kuombewa waolewe
 
Hivi we jamaa umenielewa kweli??
Hilo prado paroko akistaafu ataondoka nalo??
Hilo prado limeandikwa jina/linamilikiwa na nani??
Hilo prado unalosema huyo paroko hawezi kulitumia kwa matumizi binafsi nje ya yale yalioanishwa na kanisa.

Tatizo lako unataka kuweka usawa mahali pasipo sawa, na kubwa zaidi huijui RC na naamini we si muumini wa RC.

Hizo gari hutumika kufikia vigango mbalimbali vilivyo mbali na parokia ili hao maparoko watoe huduma.

Na unaposema hizo sadaka wanazila wao maparoko bado pia ni sawa kwani wale hwafanyi biashara nyingine zaidi ya kula kunywa na kuzunguka kuhubiri baasi, kila kitu wanahudumiwa na kanisa mavazi,makazi na chakula. Sasa sijui huo ufanano wake na walokole unauwekaje hapo ilhali wao hawana parokia wala jimbo wala watawa wala mapadre na mashemasi, wala masista. Na hao wote hapo wanategemea sadaka yako ili huduma za kiroho ziendelee kutolewa sasa hapo muumini unapigwaje ilhali hao watu ni kweli wapo na wameacha familia zao makwao kuja kuhudumu kanisani tuu maisha yao yote.
 
Hivi ukiacha ahadi ya kwenda mbinguni ukifa na kuombewa maombi ambayo nayo ni lazima uyasindikize kwa sadaka yako,kuna kipi kingine ambacho kanisa linakupa?
Kanisa kwa imani yangu linakupa mwanga, si ajabu kama nisingewahi kwenda kanisani toka mdogo basi mambo ya Mungu yangenipita kushoto.

Kanisa ni mwanzo wa karibu kila mtu kujijua na kujua kweli ni ipi, hata wasioamini uwepo wa Mungu walianza kwanza kwenda kanisani.

Achana na mambo ya kiroho tu pia kanisa ni jamii, inakuunganisha na watu kirahisi zaidi.

Na nikusahihishe jambo ndgu yangu, kwenda mbinguni ni matendo yako, unaweza kua muumini mzuri lakini mchawi hapo hata ulale kanisani si rahisi kupenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…