We jamaa una hoja dhaifu sana. Kwanza nikuulize kama ulishawahi kusali RC?? Na kujua taratibu zao walau kidogo.
Kama hujawahi kusali wala kujua taratibu za RC basi ni kheri ukakaa kimya upate kujua.
Kwanza unapotoa sadaka pale haiwi ya padre wala katekista!! Ile ni moja kwa moja jimboni kupangiwa matumizi.
Na matumizi yenyewe ni pamoja na kuwatunza hao wanaowalisha neno, hata ukiwa mbwinde huko basi parokia iliyo karibu na nyie itajitahidi iwezavyo padri walau awe anafika kila wiki kigangoni kwenu kusalisha.
Anapoondoka wala hamumlipi kwa huduma yake, wala hamumjazii mafuta kwwnye gari yake hata kama sadaka yenu mmetoa buku hiyo ndo itaenda jimboni kuungana na nyingine ili Neno liendelee kuhubiriwa.
Hiyo michango ya kujenga kanisa sio ya mtu mmoja, hatokei mtu akataka gari basi achangiwe, sijui mtu kaamka na wazo mchungaji anahitaji nyumba basi mnachanga tu.
Kubali kataa kuna utofauti mkubwa sana juu ya uendeshaji wa makanisa ya kilokole na katoliki yani utofauti mkubwa mno.