Sisi ambao hatutekwi na Wahubiri Waongo wa Miujiza ndiyo hatuna Akili au waliotekwa nao ndiyo hawana kabisa Akili?

Wale tuliowahi kuchangia ujenzi wa Cathedral sent Teresa Arusha kisha kabla ya ujenzi pesa ikachukuliwa kununua shule ya Secondary na ada ya shule hiyo hatumudu walalahoi wanetu kusoma hapo tunacoment wapi mkuu? Kuna tofauti gani ya kiwizi na hao unaowasema?
 
Pole kwa kuingizwa chaka kuwa kuna Mungu baba, mungu mwana na mungu roho na kuwa yesu alichukua dhambi za walimwengu wote pale msalabani
 
Kuku ni Kiumbe cha Mungu kama Wewe ulivyo na Chenyewe kiliumbwa Kabla Hata Ya Wewe. Wewe ni Kiumbe Cha Mwisho Kuumbwa. Usidharau [emoji215]

Kikubwa ww Umepewa kitu tofauti na Yeye tu ambacho ni Akili ingawa si Binadamu wote Wana Akili Timamu
Una matatizo ww. Japo hauyaoni.. na madhara ya matatizo uliyo nayo hayataonekana leo wala kesho.. yataonekana baadaye sana na utajuta kwamba fikra ulizo nazo sasa zilikupotosha.. ndio tatizo la haya mambo.. unapotea taratibu.. na majuto ni baadae sana kama vile mjukuu anavyokuja baadae sana
 
Waliotekwa na dini hawana akili timamu.
Waliotuletea dini(Wazungu na Waarabu) hawajatekwa na dini kuliko tulioletewa hio dini.
Mbona mwalimu wako wa shule ya msingi unamzidi elimu?.
Kumjua Mungu ni jambo la mtu binafsi.
Mbona unakataa ushoga ambao wazungu wanaukubali?
 
Wahubiri waongo wana sifa gani, au niseme wanahubiri mahubiri gani?
 
Sadaka siyo mali ya padri inakwenda jimboni na kutolewa kwa utaratibu maalum tofaut na walokole sadaka anachukua mchungaji anafanya anavotaka
Ni lini hiyo sadaka ilirudi kwa muumini mmoja moja?.
Tena RC ndo wanakula pesa za washirika kuliko hata makanisa mengine. RC ilikuwa inapokea pesa ya wafadhili sana ila nyingi ziliishia kwa viongozi
 
We jamaa una makasiriko na RC sio bure aisee.
Au labda nikuulize kitu ndgu, wewe unataka sadaka yako ikunufaishe kwa 100%?? Sasa hiyo ni kodi na sio sadaka.

Hapa mleta mada anachozungumzia ni ile kumtajirisha mtu mmoja, angalia mifano ya makanosa haya ya kilokole mwenye nguvu kubwa hapo kanisani ni huyo mchungaji mwenye upako, kwanza huyo anaweza kua tajiri kuliko hata waumini wote, huyo ndo mpanga mipango ya pesa za kanisa zitumikaje, huyo ndo mponyaji, masihi, ukiwa na shida basi peleka sadaka kwake.

Mfano leo hii kuna hao wanajiita manabii kuwaona mpaka utoe pesa, ukitaka kuponywa basi nunua maji, sabuni, mafuta au udongo wa upako.

Sasa utofauti nnaousemea mimi ni huu, wao nguvu zote anazo hiyo mmoja ilhali RC haiko hivyo.

Umekaza ubongo eti kisa mapadre hawaondoki na gari basi mm roho yangu kwatu eti hilo gari mm halinisaidii kitu😁😁, ndio maana nikasema wewe una makasiriko na RC, ushaambiwa gari linatumika na parokia kufikia vigango mbalimbali sasa na mm si ni muumini wa ivyo vigango au ulitaka wanipe mm kisa natoa sadaka.

Kijana hiyo gari ni ya kusafiria, sasa kuna uajabu gani kulikuta mahali tofauti na kigangoni(hapa mkuu ulishindwa kujiongeza).

Masister na mapadre huwa wanasoma, na ndio huwa na profession kadha wa kadha lakini hao wote huudumu kanisani au kwenye mahospital/ mashule ya kanisa, na ndio hulipwa kwani hifanya kazi. Na hata mapadri pia naskia kuna namna huwa wanapata posho(japo sina hakika sana na hili).

Umeelewa.
 
Wote akili.mnazo happy lina kuja swala la imani, wale imani zao ni kali ila ww bil shaka imani yako ni habaaa mboo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umekosa mbivu unaamua kujifariji na mbichi
 
Endelea kupotoka kote mnapigwa halafu unatetea. Mie sitaki marumbano one day utajua. Sasa hivi Ushawishi wa Makanisa umepungua sana. tofauti na miaka ya Nyuma. Papa na Manabii wa sasa Hawana Nguvu kma zamani.. Jiulize kwanini

Watu washaanza Kushtukia hii michezo
 
Hivi kulikuwa na haja gani ya kumtaja CDF Mabeyo na mkewe? Tanzania bado tuna safari ndefu sana ya kulikomboa Taifa letu dhidi ya fikra za namna hii.
Mleta mada ana inferiority complex tatizo hili huwapata hasa watu waliotoka familia na koo maskini na wenye maisha duni ambao hawajatoboa akienda hata msibani akatokea Mabeyo utasikia ahh tulihudhuria msiba mkubwa na Mabeyo!! Utafikiri walitoka naye nyumbani kwake!!! Au akipita Mabeyo na gari yeye akiwa muuza genge la Nyanya utasikia jana tulikuwa naye msibani huyo mimi nimekaa hapa yeye kakaa hapa jirani kabisa huku akijichekesha kibwege bwege kujionyesha super

Ni umaskini wa kuanzia mawazo ,maisha nk anakuwa anajiona kidogo kama ka steam out frustration zake za maisha akiongea hivyo kuwa ohh msinione nauza genge hili jana nililkaa na Mabeyo!!!! Ukimuuliza hilo lime add value gani kwenye maisha yake au kubadili status ya uchoka mbaya wa maisha yake ? Hamna kitu ni ujinga hewa tu uliojaa kichwani!!
 
Mkuu unayebishana naye aweza kuwa padri mnufaika wa hako kamrija ka kunyonya waumini !!!
 
Kama una moyo na muda kidogo tafuta lecture moja ya Prof Robert Sapolsky inaitwa "Biological Underpinnings of Religiosity"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…