Sisi ndio watekaji na wauaji, tunawasingizia tu wasiojulikana

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
SISI NDIO WATEKAJI NA WAUAJI TUNAWASINGIZIA TUU WASIOJULIKANA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Wasiojulikana! Kivipi yaani? Hawajulikani kwa namna ipi? Watekaji na wauaji ni sisi sisi Watanzania. Alafu tunajitia hawajulikani. Hawajulikani?

2. Mwaka wa kumi huu! Mnakimbizana na jambo moja kisa unafiki na ubinafsi.

3. Wenye jukumu la kulinda wananchi na mali zao wanajulikana. Na wanalipwa miaka nenda rudi. Miaka yote kumi ya utekaji na mauaji. Wao wanajulikana lakini wanaoteka watu hawajulikani. Miaka kumi! Miaka kumi! Alafu mnasema wasiojulikana wamefanya blah! Mara bleh! Really!!!

4. Ni sawa na kule uswahilini wale panya road au vibaka. Wanajifanya hawawajui lakini wanawajua.

5. Wanawalea vibaka na panya road kwa sababu ni watoto wao, waume zao, na ndio wanawapa hela za matumizi. Alafu ukiyakuta yanalalamika, panya road, sijui vibaka wamezidi. Kana kwamba hawajui nini cha kufanya.

6. Ndugu zangu, bila jamii kuamua kuacha uuaji na utekaji haya mambo yataendelea sana. Sisi kama jamii ndio tunaua na kuteka ndugu zetu alafu tunakuja kujiliza kinafiki nafiki kama wachawi. Maana mchawi ndio anaua alafu analia kwa kujifanya anauchungu.

7. Wewe mumeo au mkeo ni Polisi. Miaka kumi utekaji na mauaji yanafanywa kwenye jamii. Hujawahi hata kumuuliza nani anayeua watanzania wenzako kwani mumeo au mkeo hilo ndilo jukumu lake la kulinda jamii. Upo kimya unasubiri unachojua ni kupokea mishahara na kuomba matumizi. Really!

8. Muumini wako au muumini mwenzako ametekwa au kuuawa. Kanisa au msikiti mpo mpo tuu! Kila siku mnaenda kuswali na kuabudu. Mnamuita Mungu. Yupi? Nauliza Mungu yupi?
Yaani muumini mwenzenu hajulikani alipo lakini nyie mnaamani kabisa mnaswali na kujifanya waomba Mola. Really?
Nasema muumini kwa sababu huenda utaumia kidogo japokuwa najua wengi wenu hamuumii zaidi ya unafiki.

9. Mchungaji anazuga zuga tuu kujifanya anasema na kukemea utekaji na mauaji ilimradi naye aonekane alikemea. Lakini hana consistency yoyote ila kwenye sadaka ndio ana consistency.

10. Hivi amri ya kumpenda jirani yako kama nafsi yako ilivyo mnaitafsiri vipi?

11. Sisi ndio wauaji na watekaji wa ndugu zetu wenyewe alafu tunaleta unafiki nafiki wa kipumbavu.
Unakemea mauaji na utekaji umejificha kama hao mnaowaita wasiojulikana. Wewe na wao mnatofauti gani?

12. Kama angeuliwa mtoto wako au ndugu yako ungejificha kumtetea? Ungejificha nakuuliza wewe mnafiki na mbinafsi mkubwa!

13. Nakupa Mfano, ujasiri wa kaka wa Polepole umetoka wapi? Au mama Polepole kujitokeza kumdai mwanae umetoka wapi kama sio hayahaya ninayoyasema hapa.
Akitekwa au kuuliwa wa mwenzako unajificha kwa sababu sio wako.
Yakitokea kwako unajitokeza ili nini? Ili nani akusaidie.
Ili uonekane una uchungu au unazuga?

14. Unaenda Kanisani kila siku na unatoa sadaka kila leo kwa kanisa na mchungaji ambaye hayupo mstari wa mbele kutetea haki za watanzania hasa walionyimwa haki zile za msingi kabisa ikiwemo haki ya kuishi.
Unatoa sadaka ili hao wachungaji na mashehe wasifie serikali badala ya kuiambia serikali iwalete waliofanya utekaji na mauaji.

15. Wachungaji wako, kanisa lako na huyo mungu wako wote unawatolea sadaka wakasifie viongozi ambao wanashindwa kutekeleza wajibu wa kulinda maisha ya watu.
Hata kama ni mtu mmoja. Maisha ya mtu yana thamani.

16. Wewe kwa vile ni muuaji na mtekaji unasapoti kwa kwenda kanisa au msikitini unatoa Sadaka ili kuwapa nguvu hao watumishi waendelee kuwatia moyo watu wasiofanya wajibu wao. Wewe kama sio mtekaji au muuaji ni nani?
Unajifanya ati unamtolea Mungu, yupi? Nani alikuambia Mungu anataka sadaka yako ya kikafiri unayotoa kwa watu wasiostahili.
Sadaka na zaka zinakanuni zake. Sadaka na zaka sio za Mungu bali watumishi wa Mungu.

17. Watumishi wa Mungu ni wale wanaotetea HAKI, wanaofundisha maadili sio tuu kwa mdomo na kuhubiri bali kwa vitendo. Sio leo taikonmaster nimejiita mchungaji fulani lakini sitendi sawasawa na haki na kweli alafu wewe inanipa sadaka na zaka.

18. Hawa wanaoteka na kuuawa watu ni watu wetu wenyewe. Sisi ndio tunawaendekeza na sio ajabu tukawa tunawapa nguvu kwa kuwapa hela kwa njia mbalimbali.

19. Watu wanatekwa na kuuawa. Polisi wapo, jeshi lipo, usalama wa taifa wapo, mawaziri wapo, Rais yupo zaidi wananchi walioweka hao wote nao wapo na wanaendelea kuwalipa. Seriously??

20. Damu za watu hawa zipo juu yetu ndugu zangu. Hatuwezi kukwepa hili. Tumeshiriki kwa namna moja ama nyingine.

21. Hivi kweli Mwenzako anauawa hapo, au kutekwa hapo. Unashindwa hata kuongea. Kuongea tuu! Yaani kuongea tuu! Kupiga kelele tuu!
Jamani kuongea tuu! Unaogopa! Hutaki kufa si ndio?

22. Alafu unasema unamuabudu Mungu. Yupi?
Hivi utaweza kweli kukataa kumuabudu mtu akikuambia umsujudie na bila hivyo unakula chuma ya kichwa? Utaweza?
Jibu ni kuwa hutoweza. Utamsujudia huyu aliyekushikia silaha.

23. Kama sasa tuu hujashikiwa bunduki, hujatishiwa popote lakini unaogopa kupaza sauti kukemea mauaji na utekaji.

24. Hakuna wa kukusaidia. Hakuna!
Wewe ni muovu tuu! Wewe ni muuaji tuu! Unajifanya hujashiriki na haujawahi kuuawa lakini wewe ndiye muuaji mwenyewe.

25. Hao wanaoua moja kwa moja wao wakiomba toba Lazima ipokelewe.
Sio ajabu mtu aliyeua wote waliopotea ukamkuta kwa Mungu muumbaji. Sio ajabu kabisa hasa akiomba toba. Na lazima iwe toba ya kweli kwa sababu wauaji na makahaba wengi wao wana ujasiri na sio wanafiki nafiki.

26. Lakini wewe uliyeshindwa hata kupaza sauti yako kukemea maovu yakifanyika kwa uwoga hakika hutoweza kumuona Mungu. Hutoweza! Nakuhakikishia wewe sio mwema! Wewe ni vuguvugu!

27. Utawezaje kuomba msamaha. Kwamba utasema niliogopa kukemea maovu au? Utasemaje?
Uliogopa na uliwasapoti.

28. Nataka niwahikikishie hao wauaji na watekaji ni bora mara elfu kumi kuliko watu wanaonyamaza. Wanafiki!

29. Unaulizwa kwenye kamera, unazungumziaje kuhusu utekaji na mauaji. Ulivyo mnafiki unajifanya hujui kuwa kuna utekaji na mauaji. Unajibu oooh! Hakuna ushahidi wa kuwa kuna mtu kateka mara blah! Blah! Really?

30. Mpaka wauaji wenyewe wakikusikiliza wanapandisha hasira. Linafiki hili jamaa.
Mkeo nyumbani naye alivyomnafiki ana kupokea nyumbani. Shit..!

31. Wauaji wanasema, tumeua kweli lakini ni bora tungeliua hili jamaa huenda tungepata thawabu!

32. Hakuna kitu kinawauma wauaji kama kuua mtu asiye na hatia. Inawauma sana. Inawasumbua sana. Lakini kuuawa majitu manafiki nafiki kwao ni sherehe kubwa.

33. Nataka kusema nini baada ya andiko hili refu.
Ni hivi; Unapoishi kwenye jamii, ukatokea uovu na huo uovu ukakithiri alafu ukaa kimya nawe unakuwa sehemu ya huo uovu. Yaani nawe ni miongoni mwa watu hao.

34. Ni jukumu letu kupambana kila mtu katika eneo lake. Kwa nafasi yake. Na sio kwa woga. Kupinga maovu.
Kwa sababu kutokupinga maovu ni kushiriki maovu.

Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Utafikiwa
 
Haya matukio ya utekaji na mauaji yaliyokithiri nchini kwa sasa yanafanywa na watu wanaojifanya wanamsaidia mtawala aliyeko madarakani, na ambaye hataki kukosolewa/hataki mawazo tofauti na yale ya kwake.

Bahati mbaya haya matukio yanaharibu taswira ya nchi na pia ya huyu mtawala ambaye hasikiki akikemea, au kukomesha! Na hivyo wananchi wengi kuamini ya kwamba huyu mtawala anawaunga mkono hawa wahuni.
 
Tunawajua watekaji ni Samia, Abdul, Mchengerwa, Rostam, Kikwete, Mombo na Mafwele.

Siku tukiikomboa nchi tutawawajibisha watuambie wamewaficha wapi ndugu zetu.
 
Wanafiki na wabinafsi hawawezi kukomboa kitu chochote achilia mbali level ya kupambana na serikali
 
Back
Top Bottom