Sisi ndio watekaji na wauaji, tunawasingizia tu wasiojulikana

Wewe bwana una matatizo kichwani kwako?
Tofauti ya ulaya na afrika au TANZANIA ni nini? Ujinga uliopo afrika umesababishwa na watu wa aina yako msio na uwezo, mnaotegemea vimemo. Laiti mngekuwa mnafahami purpose za kuwa viongozi msingefanya ujinga. Isitoshe wanaoishi ulaya ni binadamu kama wewe, mimi na yule nothing special there.

Nimekwambia hivi serikali, viongozi au watawala wakipewa space wakashindwa kujitafakari basi ile jamii au watu wao watawalazimisha kwa nguvu ili warekebishe sehemu wanazolalamikiwa.

Mfano suala la utekaji halijaanza zungumzwa leo, kila mahali na tangu kitambo abduction inazungumza watu wanapotea na kuumizwa vyombo vya dola vinaleta sanaa kwenye maisha ya watu. Jamil imeongea, ikakaa kimya na kuvumilia sasa imechoka wacha ifanye kuwalazimisha sasa hata kwa kafara ya damu.

Usirudie kuniuliza vitu vidogo vidogo kama hivyo. Use your brain 🧠 properly.
 

Mkuu hayo unayoyaeleza yote wetu wote wanayajua.

Shida yako niliyoyaandika ndio hunipati kwa sababu tayari unaongozwa na mihemko. Ipe akili yako nafasi.

Jiulize kama utekaji haujaanza leo why mpaka leo unaendelea? Jibu lake lipo kwenye hii post.

Kwa nini hutaki kukubali ukweli kubwa mimi na wewe ni sehemu ya wanaoteka na kuua watu. Huoni ushiriki wako katika jambo hilo?
 
Sasa unapata faida gani kuwakejeli watu ambao wengine wamepotelewa na wapendwa wao, wanahangaika kulisha familia zao, ndugu zao wamepigwa, kuvunjwa viungo na kuwa vilema? Wanaona kila siku rasilimali, kodi zao zinaibiwa na kutumika hovyo, viongozi wao wanafungwa, kuuwawa na kupotezwa?

Waelimishe kwa staha, waonyeshe wanapokosea, namna bora zaidi kufanya harakati zao kupata matokeo chanya kwa familia zao na Taifa kwa ujumla. Taifa likipata uongozi bora, unaojali haki kwa wote, sote tutanufaika.

Kwa wengi hii sio abstract, philosophical, ego driven discussion. Sehemu ya kutafuta kiki. Uhuni unaoendelea unaathiri maisha, uhai, haki za msingi za watu. Hizi ni serious issues, require serious discussion. Sio kubeza watu. Mimi ni hivi,vile, mimi ni mjanja sana, mimi nina akili sana, mimi natumia jina langu halisi. Hii issue, discussion siyo kwa ajili yako, kukujua wewe ni nani bali kujaribu kutatua matatizo makubwa ya kitaifa.
 

Je ww hapa umepinga au Umeongea?.

Kwa kuongea tu hivi unaona kuwa umepinga?.

Maneno hayavunji mfupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…