mpita-njia
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 1,734
- 1,616
Mimi Noah yangu haijafika hadi leo. Sijui meli imepata pancha au.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata Mungu utushangaa hawa wanataka kulia tena safari hii sio mitano ni ishirini katiba ni lzm atabadilishaHuu Uzi natamani tuusambaze kwenye platforms zoote za kijamii ili watu wakumbuke maana Watanzania tuna sifa ya kusahau.
Ndege ya mizigo itabeba raslimali zetu kuzipeleka kwa mabeberuSasa hiyo ndege ya mizigo si ndiyo itakayoleta fedha za kuchimba visima upate maji safi maana huna utamaduni wa kulipa kodi.
Ni heri wataadharishwe pia ili wakiumizwa wasimlilie mtuMkuu pole sana
Kwa uliyotaja yanafikirisha yanaumiza ni wachache watakuelewa
Napata wakati mgumu kujiuliza kwa nini wengine wanaona ni Heri akaendelea kutukanyaga
Usilie kamanda!SISI SIO WAJINGA.
Ulipochukua tu madaraka ukaanza na kubomoa nyumba zetu katika bonde la Msimbazi. Bila huruma ukatuacha tumelala nje na watoto wetu. Ulidhani tutahama mjini lakini sisi bado tupo.
SISI SIO WAJINGA.
Ulipokuwa unapanua barabara ya Ubungo - Kibaha ukabomoa nyumba zetu. Mbunge wetu Mnyika aliomba utulipe fidia ukampinga mbele yetu. Lengo lako tufe masikini lakini kwetu sisi maisha yanaendelea.
SISI SIO WAJINGA.
Hukutaka tuwaone wawakirishi wetu, wakiwakirisha matatizo yetu Bungeni. Ulisema gharama za kurusha matangazo Live ni kubwa. Lakini leo hii unatuomba tufungue TBC tukuangalie ukikata mitaa kuomba kura.
SISI SIO WAJINGA.
Baada ya kuwa tumefanya kazi kwa miaka 40 na tumebakiza miezi 3 tustaafu ukatufukuza kazi kwa kisingizio cha vyeti feki. Ulidhani tutakufa kwa njaa lakini Mungu anatupigani bado tunaishi.
SISI SIO WAJINGA.
Tulipopata tetemeko la ardhi Watanzania wenzetu walituchangia pesa nyingi lakini wajanja wakatafuna. Ulipokuja Bukoba tulidhani utatutetea wanyonge badala yake ukatusimanga na kutukumbusha majanga ya Ukimwi, MV Bukoba kwamba yote yanatupiga sisi. Sasa nasikia unakuja kuomba kura kwetu! Je, ni kweli wewe utakanyaga Bukoba?
SISI SIO WAJINGA.
Tulipokuwa tuna njaa. Njaa iliyotokana na ukame. Tukakuomba msahada wa chakula. Hii sio kwako tu, hata Serikali zilizopita zilitusaidia tulipokumbwa na ukame. Lakini ulitujibu kwa kejeli na kiburi cha hali ya juu. Eti tusikuombe chakula, Serikali haina shamba. Leo hii unakuja tena kuomba kura?
SISI SIO WAJINGA.
Tukaenda Mtwara kulima korosho. Ukatuma askari wako wakatunyang'anya korosho halafu wakadai tuwaonyeshe mashamba yetu. Mbona wanaolima Mahindi, Pamba, Mpunga, n.k. hamuwaulizi mashamba yao? Ukasema hao askari watabangua korosho kwa meno ili kila Mtanzania atapata kilo 2, lakini hatujapata mgao.
Sasa nasikia unakuja kuomba kura! Labda uishie Nangurukuru kwa sababu.
SISI SIO WAJINGA.
Tumeitumikia nchi yetu kwa bidii kubwa. Tumefanya kazi kwa uzalendo mkubwa, huku tukipokea mishahara kidogo. Leo hii tumestaafu, tupo nyumbani miaka ikikatika. Lakini hutaki kutulipa mafao yetu. Bila aibu unakuja kutuomba kura tena?
#SISI_SIO_WAJINGA.
Kweli kamanda.Come 28 Oktoba
Chagua
Rais Chadema
Mbunge Chadema au ACT
Diwani Chadema au ACT
Usifanye makosa tena ya kuchagua matapeli.
Halafu sijui kwa nini havai barakoa kama wenzake Wakenya?Amesahau Lissu ana damu ya wakenya, wakenya hawakubali ujinga wanakinukisha.
Kweli kamanda!Siko tayari kuona tunanunua ndege za mizigo angali kuna watanzania hawana uhakika wa maji safi.
Sisi sio wajinga, kura kwa Tundu Lissu
Yes!Inafikirisha
Hao waliofanya kosa la jinai miaka yote mbona products walizozitoa mlizpokea na mnaendelea kuzitumia?Wewe na wenzako wanaoshabikia huu upuuzi ulioandika ni wajinga na wapuuzi kabisa. Ulitaka uachwe unaishi bonde la msimbazi kama chura? Ili mafuriko yawe yanafunika nyumba yako ili upige mbizi ukiwa umelala! Ulitaka watu waliojenga kwenye hifadhi ya barabara walipwe? Huku walishaenda mahakamani na kushindwa kesi?..
Yeye na bwana ake mkuu..wazee wa kupumuliwa visogoni hawa shida tupu.Ungesema wewe siyo mjinga. Badala ya kuongelea nafsi ya mtu.
Mimi sipo hapo kwenye “Sisi”