winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 379
- 603
Fikiria hili: unapomtegemea mtu kwa kila jambo bila kufanya juhudi za kujitegemea, ipo siku utakuta umegeuka mtumwa wake. Hali hii inadhihirika wazi kupitia uhusiano wetu na China, ambapo nchi yetu na nyingine nyingi za Afrika zimewekwa katika hali ya utegemezi mkubwa. Sekta zetu muhimu kama viwanda, biashara, na ajira zimelegezwa au kudumaa, na nafasi ya kujenga msingi wa utaifa imetatizika kwa kiasi kikubwa.
Kwa wale wasioangalia kwa mapana na vipindi virefu, huenda wasione mtego ambao China imeuweka kwa mataifa yanayoendelea kama Tanzania. Kinachotia uchungu zaidi ni kwamba, kama taifa, tumekosa utamaduni wa kutumia busara na mikakati ya muda mrefu, tukiegemea zaidi kwenye siasa na mara nyingine ubabe. Viongozi waliopita wengi hawakutoa dira ya kweli ya maendeleo ya muda mrefu kwa manufaa ya taifa.
Tanzania, kama taifa lenye rasilimali nyingi na nafasi nzuri ya kujitegemea, tunapaswa kuwa na mifumo madhubuti ya ulinzi wa kitaifa katika kila sekta. Tunahitaji vitengo vya usalama wa taifa vinavyolinda uchumi wetu, kuimarisha uongozi bora, kusimamia biashara, na kuhakikisha usalama wa kitaifa katika kila wizara na idara. Mifumo hii inapaswa kusimamiwa na watu wenye uzalendo wa kweli na uwezo mkubwa wa kufikiri kimkakati, badala ya uteuzi wa watu wasiokuwa na weledi wa kutosha.
Intelijensia ya TANZANIA toka awali imekuwa chini sana lakini kwa kipindi hiki ipo kwenye kiwa cha chini zaidi kuwa kutokea. Miradi mingi na yenye kuingizia hasara trilioni za fedha imesimama na hakuna waziri wala mtendaji wa serikali aneshituka. Mipango mingi inalenga kipindi cha unyangányi wa kura kifike ndipo serikali itumwe na kundi la wachache kwenda kuhadaa wananchi.
Inasikitisha na kuudhi kuona nchi yetu ikikosa mwelekeo kama jogoo aliyechinjwa kichwa na kuachwa akikimbia bila kujua anakokwenda. Tunahitaji mabadiliko ya dhati kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu.
TUNA WATU WENYE UTASHI, AKILI, UADILIFU NA MAWAZO CHANYA LAKINI MFUMO WA UTAWALA UMENGÁTA NDIMI ZAO WASIWEZE KUSEMA NA KUKOSOA WAZIWAZI MWENENDO WA NCHI YETU ULIYOKOSA DIRA.