Sisi Wakristo masikini tunanufaika vipi na shule za Kanisa?

Sisi Wakristo masikini tunanufaika vipi na shule za Kanisa?

Simple calculation ni kuacha kuchangia maana hakuna matokeo ya moja kwa moja kwa muumini ndio maana nashangaa wanaowasakama akina Gwajina etc.

Wote wanafanya kwa njia tofauti, unatoa pesa ananunua helicopter unatoa sadaka wanajenga shule na hostels lakini manufaa yake yananufaisha wenye “jiko”

Faith Based Orgs hazina tofauti na NGOs au mashirika mengineyo 😃😃
Kumbuka Heri kutoa kuliko kupokea...
Kumbuka kwa kutoa hiyo sadaka basi unaeneza injili kwa watu wote..ambao ndio wito wetu mkuu.
Kwa uchache nikizungumzia hiyo kkkt iliyotajwa, dayosisi ya huku Dar wanakusanya taarifa za wanaotaka kusoma lkn hawana uwezo wanaanzia level ya jumuiya na baadaye wanachambua kupata wahitaji zaidi vs idadi ya nafasi walizotengewa.Hivyo wanazingatiwa vizuri tu, labda kama huendi kanisani au unaenda lkn hufuatilii matangazo vizuri.Shule ni Mbwawa, kiserawe semibary, mkuza nk.
Dayosisi zingine pia wana taratibu zao Muhimu afuate channel sahihi hasa kuanzia usharikani au jimboni.
 
Mi ni KKKT nilishaachaga kutoa sadaka ya mambo ya mfuko wa elimu sijui benk mara hospital maana vikiisha hata siwezi kuvimudu hata mwanangu sitaweza kumsomesha hapo. Hizo ni business na wanaofaidika ni hao waliojuu wanaondesha V8. Na siku ukinyoosha kidole kuuliza Haya mambo watakuparura kila kona maana unawaingilia maakuli yao. We makanisa yana kila ruzuku kutoka serikali ie hawana wakodi kama sekta binafsi but still wanafamya biz kabisa. Huku zikiwa zimejengwa BURE kabisa na waumini Masikini.... Ni WIZI.
Now Kanisa ni Business entity sio tena kueneza Injili na ndio maana mahubiri yao 90% ni pesa... 5% mafanikio 5% ndio injili ya Yeshua.
Ukichangia unaoeleka mbele injili na eventually baraka zitaambatana nawe.Sasa huzitaki Ni uamuzi wako ila ni matamanio nawe usizisikie tu baraka kwa wengine bali uziishi.
Kumbuka hizi kkkt ni 'trust' orgs viongozi ni wadhamini( trustees) Hivyo kwa sehemu kubwa sana sana hela inazunguka kuifanya kazi ya BWANA ( diakonia, afya, elimu, watu kumjua Mungu nk).Ukiwa mkristo uyajue hayo utafurahi na utastawi bila shida katikati ya wanaolalamika.
 
Haya mambo ya dini nishaona bora umwabudu mungu ktk roho nakweli kanisani nikuchoshana tu.
 
Leo matokeo ya Mitihani ya Darasa la nne na Form Four yametoka!

Kama kawaida shule zinazoongoza nyingi ni zile zenye Uhusiano na Kanisa, iwe kwa umiliki au kwa njia nyingine! Hii bila shaka inatoka na misingi Bora iliyowekwa!

Pamoja na mafanikio haya, Shule nyingi za Kanisa gharama zake za masomo ni ghali sana! Pengine kuliko hata shule za watu binafsi!

Hali hii huwafanya Wakristo wengi masikini wasinufaike na hizi shule! Kwangu mimi nafikiri hiki ni kinyume na misingi ya Ukristo na hata ubinadamu!. Ilitarajiwa basi wenye shule nao wanufaike!

Wote ni mashahidi Kwa mfano, upande wa KKKT kumekuwa na michango ya kuchangia Seminary kadhaa hapa nchini! Lakini ni vipi hawa masikini Wananufaika ambao ndio wanaochanga kuku na mbuzi wao na wengine huchangia kwa maombi ilhali ada za shule hizi ni sawa na kipato Cha familia masikini kwa mwaka mzima!

Je, hao hawana haki ya hii Elimu Bora!
Je, Kanisa linaona hii hali!?

Hali haipo tofauti pia ktk Hospitali za Kanisa,Waumini wengi hawana ubavu wa kuingia hospitali kadhaa za ambazo ni ghali.

Ni vipi Msharika Maskini wa Loita Dayasisi ya Meru anaweza kupata huduma Bora za afya ktk Hospitali ya Selian aliyaoichangia kwa miaka mingi!

Nafikiri kuna kitu hakipo SAWA! Ndani ya Kanisa na Sisi Waumini pia!

Tutafakari!
Usiendekeze umasikini wewe
 
Ahaa,kwa hiyo Watanzania maskini ni Waislam,Wapagani na Wahindu😁😁😁subiri waje!
Ndiio Yesu alisema nimekuja kutangazia maskini habari njema kwa maskini ya kukombolewa kwao

Habari njema kwa maskini kukombolewa si kuondokewa na umaskini?

Ukimkuta mkristo maskini huyo sio Mkiristo mwamini Yesu mtangaza habari njema ya kukomboa maskini

Huyo ni mpagani au dini ingine mfuasi wa Kristo kwelikweli hawezi kuwa maskini huyo maskini anajiita Mkristo atakuwa mwabudu mizimu au mashetani au dini hana mshenzi mkubwa
 
Back
Top Bottom