Sisi Wakristo masikini tunanufaika vipi na shule za Kanisa?

Sisi Wakristo masikini tunanufaika vipi na shule za Kanisa?

Kwanza ungejiuliza umekuwaje masikini wakati Bibilia inasema uliumbwa utawale? Ungejiuliza Kwanini huyo Mungu awanague? Wachache wawe matajiri huku nyie wengi ndo masikini?
Hata Yesu alikuja kwa ajiili Yetu 😁😁masikini....ila tanueni tu,tumeshashtuka ...tutapindua meza!
 
Shule za dini zinazofaulisha vizuri ada ni kubwa hivyohivyo, za kiislamu nazo ni hivyo ila tofauti ni kwamba hazijengwi kwa michango ya waumini. Taasisi inayoanzishwa ndiyo inajenga, huku Tanga zipo zilianza kama madrassa, wanafundisha kwa ada na baadaye wakaja kufikia kuanzisha chekechea na kisha msingi mtaji ulipopanuka. Hatimaur wakaja kuleta sekondari zao.

Pia zipo taasisi zingine zilianzishwa na waislamu wanaojiweza, zikaja kumiliki shule zao.

Mfano Tanga kuna shule ya sekondari ada ni Sh Mil 5, na sijawahi kusikia imetoa div 4 au zero. Mwaka huu ina div 1 53, 2 zipo 19 na 3 zipo 5 tu.

Shule za kidini kuwa na ada kubwa si tatizo balo tatizo ikiwa inaendeshwa kwa michango na wanaotoa kiwa hawanufaiki. Ila kama iliundwa kwa nguvu za taasisi wakawekeza pesa ya kutosha si jambo baya hilo. Maana taasisi ni watu na hao watu wana maisha pia, inabidi wapate riziki kupitia huko.
...hao wanaoan zisha kibiashara Kwa Mgongo wa Dini nao ni wahuni kama wahuni wengine!
Afrika tuamke!
 
Hata Yesu alikuja kwa ajiili Yetu [emoji16][emoji16]masikini....ila tanueni tu,tumeshashtuka ...tutapindua meza!

Hayo mahubiri ni ya kukupumbaza uukubali umasikini na kujiona mtakatifu wakati ukweli ni kwamba dini ni uduwanzi
 
Huwaga najiuliza hili swali kama kkkt tuna mchango kabisa wa mfuko wa elimu unachangia kila jumapili kwenye bahasha yako ya ahadi na jengo

Wangeweka utaratibu wa kila msharika akiwa anajaza form ya shule kuwe na kipengele cha dhehebu unalotokea na no ya ahadi na kuwe na unafuu wa ada
 
Wakisomesha bure masikini elimu yao itashuka. Kanisa linafanya biashara na halipo tayari kupata hasara nendeni huko kayumba
Shida linafanya biashara kwa mgongo wa Masikini. Maana hao ndo wanaozijenga hizo shule but hawawezi kuzimudu ni wizi ambayo hata Yesu atawakataa.
 
Kweli kabisa! Hiyo sadaka tutunze tupeleke watoto shule zao.

Wao wajenge kwa vyanzo vingine!

Niliumia sana binti mmoja alikuwa analalamika anakatwa mshahara LAKI 2,Kuchangia ujenzi was kitega Uchumi wcha Kanisa Fulani jijini Dodoma!
Huu ni wizi!
Round about ya whimpy
 
Huwaga najiuliza hili swali kama kkkt tuna mchango kabisa wa mfuko wa elimu unachangia kila jumapili kwenye bahasha yako ya ahadi na jengo

Wangeweka utaratibu wa kila msharika akiwa anajaza form ya shule kuwe na kipengele cha dhehebu unalotokea na no ya ahadi na kuwe na unafuu wa ada
Thubutuuuuuu
 
Leo matokeo ya Mitihani ya Darasa la nne na Form Four yametoka!

Kama kawaida shule zinazoongoza nyingi ni zile zenye Uhusiano na Kanisa, iwe kwa umiliki au kwa njia nyingine! Hii bila shaka inatoka na misingi Bora iliyowekwa!

Pamoja na mafanikio haya, Shule nyingi za Kanisa gharama zake za masomo ni ghali sana! Pengine kuliko hata shule za watu binafsi!

Hali hii huwafanya Wakristo wengi masikini wasinufaike na hizi shule! Kwangu mimi nafikiri hiki ni kinyume na misingi ya Ukristo na hata ubinadamu!. Ilitarajiwa basi wenye shule nao wanufaike!

Wote ni mashahidi Kwa mfano, upande wa KKKT kumekuwa na michango ya kuchangia Seminary kadhaa hapa nchini! Lakini ni vipi hawa masikini Wananufaika ambao ndio wanaochanga kuku na mbuzi wao na wengine huchangia kwa maombi ilhali ada za shule hizi ni sawa na kipato Cha familia masikini kwa mwaka mzima!

Je, hao hawana haki ya hii Elimu Bora!
Je, Kanisa linaona hii hali!?

Hali haipo tofauti pia ktk Hospitali za Kanisa,Waumini wengi hawana ubavu wa kuingia hospitali kadhaa za ambazo ni ghali.

Ni vipi Msharika Maskini wa Loita Dayasisi ya Meru anaweza kupata huduma Bora za afya ktk Hospitali ya Selian aliyaoichangia kwa miaka mingi!

Nafikiri kuna kitu hakipo SAWA! Ndani ya Kanisa na Sisi Waumini pia!

Tutafakari!
Nyie endeleeni kutoa sadaka na fungu la kumi tuu,thwawabu mtazikuta mbinguni.
 
Huwezi kuwa na Kanisa ambalo Kazi yake ni kufanya biashara harafu hata faida za hizo biashara hatuoni zikiwaridia waumini,matokeo yake wanajinufaisha wachache.

Nini faida ya kuwa na vitega uchumi vya Kanisa ambavyo mwisho wa siku haviwanufaishi waumini wala michango haipungui.

Binafsi nilishaachaga kwenda makanisani.
 
ikibidi wewe jitoe sadaka, fanya kazi kama mtumwa mtoto wako asome huko unakolalamika ni bei.
kuna wazazi wanasomesha watoto wao hizo shule, wanajinyima sana aisee.
uwe unaamka hata saa kumi alfajiri unapambbana hadi saa nne usiku, osha magari, uza mifuko, uza uji, n.k.
Pale mwishoni mwa uzi wake kaandika:

"TUTAFAKARI"
 
...hao wanaoan zisha kibiashara Kwa Mgongo wa Dini nao ni wahuni kama wahuni wengine!
Afrika tuamke!
Shule hizo ni biashara aisee na taasisi huwa zinaendeshwa kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake, ambao wanazitumikia. Zinatumia falsafa ya kidini kwenye utendaji na maadili yake, tofauti na nyingine za kiraia. Yaani wao mfumo wao, maisha yao ndano ya taasisi ndiyo yanaendeshwa kwa kufuata dini. Ila bado wanasimamia biashara, hata misikiti kwa taasisi za kiislamu imewekwa kwa kufanya ibada tu. Wakimaliza wanafunzi wanarudi kusoma, wafanyakazi ni ofisini.

Kisichoruhusiwa na ni kibaya ni hicho kuendesha michango ya kulipa wafanyakazi wa taasisi, au ujenzi wa mradi husika huku wachangiaji hawanifaiki. Ila kama taasisi ilianza kusimama yenyewe, basi hakuna baya hapo. Mungu karuhusu tujitafutie mkate wa siku, nao wanatimiza hilo.
 
Back
Top Bottom