Sisi Wananchi halali wa Tanzania, tunatuma Ujumbe na Maombi yetu kwako Rais Samia

Sisi Wananchi halali wa Tanzania, tunatuma Ujumbe na Maombi yetu kwako Rais Samia

Mkuu wangu
Hata usemeje hakuna hata moja litakalofanyika.

Waliofanya hayo ni CCM na ndo uelewe kwa nini chama kinatumia dola kusalia madarakani kwa gharama yeyote hata kuteka na kuua.

Umeongea point muhimu sana. Mpaka muda huu unapoona hakuna kilichofanyika ni jibu tosha kuwa CCM hususani wanaoiwakilisha kwenye dola ni sehemu ya haya madudu.

Tunza kura yako. Mwaka 2025 apate kura ya watu aina ya Lucas mwashambwa lakini kura zetu Watanzania ziende nje ya CCM
🤣🤣🤣🤣 ama kweli kupenda ni upofu. Ukionacho chongo mwenzio huona kengeza. Yani unamshaur mleta mada atunze kura yake kwa ajili ya kuwachagua hawa wezi wengine!!

Kwanza afadhali zimwi likujualo halikuli ukaisha. Lakini hawa wengine achilia mbali kujaza matumbo yao na ya familia zao, pia watataka walipe fadhila kubwa kwa mabeberu waliohifadhi watoto wao na ndugu zao huko Marekani, Canada na Belgium ambao wengi wao wameshapewa na uraia kabsa, huku wakiwaacha nyie kina kajamba nani muwapiganie wazazi wao. Na hapo hapo wakili Amsterdam atataka awe analipwa ili kusimamia mikataba feki itakayosainiwa serikali ya hawa walafi.

Sabodo alikipa chama M100 za kujenga ofisi ya ksasa, lakini mpaka leo wameshindwa kupaka hata rangi ukuta. Afu unashauri mleta mada awapigie kura!!!

Nafikiri ungemshauri mleta mada aweke kura yake ili kumchagua mgombea ambae hatokuwa wa chama chochote cha siasa, hapo ungeeleweka.

Just imagine watu ambao wanaanza kujiibia wenyewe vyamani, je wakipewa nchi na kumiliki hadhina ya taifa letu hali itakuaje?
 
Attachments

  • Screenshot_20230408-090031.jpg
    Screenshot_20230408-090031.jpg
    67.3 KB · Views: 2
  • Screenshot_20220912-125326.jpg
    Screenshot_20220912-125326.jpg
    62.8 KB · Views: 1
  • images (3).jpeg
    images (3).jpeg
    28.5 KB · Views: 1
  • Screenshot_20230408-090718.jpg
    Screenshot_20230408-090718.jpg
    45.3 KB · Views: 1
🤣🤣🤣🤣 ama kweli kupenda ni upofu. Ukionacho chongo mwenzio huona kengeza. Yani unamshaur mleta mada atunze kura yake kwa ajili ya kuwachagua hawa wezi wengine!!

Kwanza afadhali zimwi likujualo halikuli ukaisha. Lakini hawa wengine achilia mbali kujaza matumbo yao na ya familia zao, pia watataka walipe fadhila kubwa kwa mabeberu waliohifadhi watoto wao na ndugu zao huko Marekani, Canada na Belgium ambao wengi wao wameshapewa na uraia kabsa, huku wakiwaacha nyie kina kajamba nani muwapiganie wazazi wao. Na hapo hapo wakili Amsterdam atataka awe analipwa ili kusimamia mikataba feki itakayosainiwa serikali ya hawa walafi.

Sabodo alikipa chama M100 za kujenga ofisi ya ksasa, lakini mpaka leo wameshindwa kupaka hata rangi ukuta. Afu unashauri mleta mada awapigie kura!!!

Nafikiri ungemshauri mleta mada aweke kura yake ili kumchagua mgombea ambae hatokuwa wa chama chochote cha siasa, hapo ungeeleweka.

Just imagine watu ambao wanaanza kujiibia wenyewe vyamani, je wakipewa nchi na kumiliki hadhina ya taifa letu hali itakuaje?
Zidaini hizo pesa badala ya kuruka ruka kama.mahindi ya bisi.

Ufisadi wowote unaofanywa na wapinzani kwa ujumla wao haufikii uzayuni wa CCM tena kwa mmoja mmoja
 
Mkuu wangu
Hata usemeje hakuna hata moja litakalofanyika.

Waliofanya hayo ni CCM na ndo uelewe kwa nini chama kinatumia dola kusalia madarakani kwa gharama yeyote hata kuteka na kuua.

Umeongea point muhimu sana. Mpaka muda huu unapoona hakuna kilichofanyika ni jibu tosha kuwa CCM hususani wanaoiwakilisha kwenye dola ni sehemu ya haya madudu.

Tunza kura yako. Mwaka 2025 apate kura ya watu aina ya Lucas mwashambwa lakini kura zetu Watanzania ziende nje ya CCM
Hahaha Lucas akisoma hapa hawezi kurudi kuandika chochote kuhusu siasa.
 
Kwanza nianze ujumbe wangu kwa kumtanguliza mwenyezi Mungu alietupa uhai, afya, nguvu na akili ya kusimamia mfumo wa maisha yetu ya kila siku.

Pili nitumie tena nafasi hii kuwasalimu watanzania wenzangu ukiwepo na wewe raisi wetu na Mtanzania namba moja, "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?" (Kazi iendelee)

Tatu nikupongeze kwa kupata ugeni mzito week iliyopita, ugeni ambao nina hakika utaenda kuinufaisha nchi yetu hapo baadae kutokana na ukaribu uliyopo kati ya nchi yetu na ile ya mgeni wetu mama Kamala Harris.

Mheshimiwa raisi, nikiachana na hayo mambo matatu niliyoyatanguliza hapo juu, naomba sasa ruhusa yako ya kuendelea na kile kilichonifanya niandike ujumbe huu kwako.

Mheshimiwa raisi week iliyopita, yani kabla ya ujio wa mgeni wetu mheshimiwa mama Kamala Harris , kulikuwa na upokeaji wa ripoti mbili. Yani ya takukuru na ile iliyohusu ukaguzi wa mali za umma katika ofisi za serikali.
Kitendo kilichosababisha wananchi wengi tufuatilie ripoti ile ili kujua kile kilichojiri katika ripoti ile, lakin pia kufahamu ni hatua gani ambayo serikali itaenda kuchukua kutokana na kile kilichoandikwa katika ripoti ile.

Kweli ripoti ilisomwa, na madudu mengi tuliyasikia kupitia kwako mwenyewe kama kiongozi wa serikali na raisi wa nchi yetu.

Wengi tuliona ni jinsi gani ulivyochukizwa, na kuumizwa na ubadhilifu ule wa mali zetu za umma uliofanywa na watu wachache wanaotumia mianya yenye udhaifu serikalini kuiba, na kulitia hasara taifa. Huku wakijua kwamba endapo itafahamika kwamba wameiba, basi hakuna hatua yoyote ya maana itakayochukuliwa dhidi yao.

Hili la kujiamini kuwa hakuna lolote litakalofanywa dhidi yao linakuja katika akili zao, kutokana na uzoefu waliokuwa nao huko nyuma. Kwamba wizi mwingi ulikuwa ukifanyika na mwisho wa siku wezi waliishia kuhamishwa tu ofisi, au kufukuzwa tu kazi bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kushitakiwa kwa wizi wao unaolitia hasara taifa, na kuifedhehesha serikali iliyopo madarakani kwa kushindwa kufanya lolote juu yao.

Fikiria kama mwizi wa ndala anafikishwa mahakamani, na kufungwa kwa wizi huo ili iwe fundisho kwa wengine kuiba ndala, sasa kwanini hawa wanaotuibia mabilioni yetu ya kodi kila siku inashindikana kuwaadabisha ili liwe funzo pia kwa watumishi wengine wa serikali?

Wengi tunakumbuka wakati ulipoanza kukalia kiti cha uraisi, ulitoa onyo kwa mafisadi na wabadhilifu wa mali za umma.

Uliwataka wezi hao wasijaribu kupima kina cha maji kwa kutumia ugoko, na pia wale ambao wangekuzingua na wewe ungewazingua zaidi.

Sasa kulikoni mheshimiwa raisi mpaka leo ni miaka miwili sasa mafisadi washapima kina na kuvuka kabisa mto bila kuzama au kushikwa miguu!

Wengine washazingua bila na wao pia kuzinguliwa!

Je zile kauli zako ulizotoa kipindi kile zilikuwa ni za kisiasa tu au za utekelezaje?

Kama ni za utekelezaji, je ni lipi ambalo ushatekeleza kwa wabadhilifu hao wa kodi zetu?

Mheshimiwa raisi, mimi mwananchi wa kawaida ambae nina watu nyuma yangu walionituma nilete ujumbe huu kwako kupitia jukwaa letu hili pendwa, ambalo na wewe huwa unapitia pitia mara moja moja kuchungulia na kusoma maoni ya wananchi wako. Ikikupendeza tulikuwa tunashauri mambo haya matatu tu hapo chini.

1. Wewe kama raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na mkuu wa serikali yetu pendwa.
Tunaomba utoe kauli ya kusimamishwa wale wote waliohusika katika kashfa za ubadhilifu wa mali zetu za umma ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yao ufanyike.

Mheshimiwa raisi tunaomba kauli hiyo iwe ya kimamlaka na kiutekelezaji. Na ikionekana kuwa kauli yako imeshindwa kutekelezeka, basi viongozi wanaohusika kuwasimamia wabadhilifu hao waliwe wao vichwa, ili nafasi zao zichukuliwe na watanzania wengine ambao watakuwa wepesi kufuata maagizo yako ambayo ni yenye faida kwa taifa.

2. Ikibainika kwamba wabadhilifu hao hawakuhusika kwa namna moja au nyingine basi wasamehewe ili waendelee na majukumu yao ya kazi.

Lakini ikibainika kuwa wamehusika na ubadhilifu huo, wasiishie tu kupisha ofisi zao, bali tunaomba serikali yako iwachukulie hatua kali ya kisheria kuwafikisha mahakamani, na huko mahakamani ikibainika uhusika wao, basi serikali iiombe mahakama iwachukulie wahusika hatua kali ya kifungo kirefu na adhabu kali, huku mali zao zote zikizuiliwa na serikali, taratibu za kisheria zifuatwe, na hatiame mali hizo zitaifishwe na fedha zitakazopatikana kutoka katika mchakato huo zirudishwe kwa wananchi kwa kutujengea barabara, shule, hospital au chochote chenye manufaa kwetu.

3. Wahusika baada ya kumaliza vifungo vyao wasiruhusiwe kufanya kazi mahali popote ndani ya ardhi yetu ya Tanzania, isipokuwa kazi ya kilimo tu ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza mfumuko wa bei ndani ya nchi yetu.

Kwa hayo machache mheshimiwa raisi naomba niishie hapa. Nina imani kama raisi mwenye upendo na uchungu wa kweli kwa wananchi wako utafata ushauri huu na kuutekeleza kwa 100%

Ukishindwa kufanya haya, basi turuhusu sisi wananchi wa kawaida tuwafuate huko ofisini kwao tukawachomoe mmoja mmoja, maana sikufichi, sisi raia tuna hasira nao sana.

Nakutakia mafanikio mema katika utekelezaji wa majukumu yako.

Asanteni sana.
Kweli,Rais fanyia kazi riport hiyo ya mkaguzi vilevile fuatilia na capitation mashuleni,watu wanakula tu Hanna kinachofayika huku mashuleni yani stupid kabisa

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Mnajisumbua tu,hakuna hatua yoyote ikatayochukuliwa kwa akatayeonekana kafanya ubadhirifu
Taifa/nyie mtaishia kulalamika na kulialia tu...na wahusika washazoea malalamiko yenu,wanajua mtalialia mwisho wa siku itapita na mtasahau

Ova
 
Ya ni kweli mkuu, raisi atupie jicho na mashuleni. Huko kuna wizi mkubwa unafanyika huku elimu wanayopewa watoto wetu ni zero kabisa.
 
Mnajisumbua tu,hakuna hatua yoyote ikatayochukuliwa kwa akatayeonekana kafanya ubadhirifu
Taifa/nyie mtaishia kulalamika na kulialia tu...na wahusika washazoea malalamiko yenu,wanajua mtalialia mwisho wa siku itapita na mtasahau

Ova
Raisi ashaanza kufanyia kazi baadhi ya mambo tuliomshauri. Sasa ngoja tusubiri kuona hatua itakayochukuliwa badala ya kuanza kum judge katika utekelezaji wa majukumu yake.
 
Back
Top Bottom