Sita wasomewa mashtaka ya mauaji ya Milembe Seleman aliyekuwa Afisa wa GGM, akiwemo aliyekuwa "mkewe"

Sita wasomewa mashtaka ya mauaji ya Milembe Seleman aliyekuwa Afisa wa GGM, akiwemo aliyekuwa "mkewe"

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Milembeeeeee.JPG
Watu sita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita wakishtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya madini ya dhahabu (GGM) Milembe Seleman (43).

Watuhumiwa waliopandishwa mahakamani katika kesi namba 12/2023 ni Dayfath Maunga(30), Safari Labingo(54), Genja Lubingo(30), Musa Lubingo (33), Maige Fundikira (37) na Ceslia Macheni (55).


Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Johari Kijuwile, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Scolla Teffe ameieleza Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa la mauji kinyume na kifungu cha 196 & 197 cha kanuni ya adhabu .

Amedai Aprili 26, 2023 Dayfath Maunga na wenzake watano huko katika maeneo ya Mwatulole wakishirikiana kwa pamoja walimuua Milembe Seleman.

Washtakiwa hao hawakupaswa kuzungumza chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 7, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wote wamerudishwa mahabusu.


Pia Soma 1. Afisa Ugavi wa mgodi wa Geita, Milembe Suleiman auawa na viganja vyake kukatwa

2. mzazi wa marehemu Milembe Suleman aongea mazito
 
Watu sita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita wakishtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya madini ya dhahabu (GGM) Milembe Seleman (43).
Tunaomba story behind.

Kuna familia hapa naiona kuna shida sehemu ukute alimrubuni binti ya mzee hapo.

Ndiyo visasi kesi tamu sana 3 yrs to come sio leo hiiii
 
Hii ndio Habari sasa.

Ndugu watatu wa familia moja watakaa jela na pengine mauti yakawakuta huko kabla hata ya hukumu.

Bado ukifikiria vizur wanaweza pigwa kitanzi... na maisha yakaishia hapo.

majuto mjukuu.

Ubaya una kwao.
 
Tunaomba story behind ....Kuna familia hapa naiona kuna shida sehemu ukute alimrubuni binti ya mzee hapo .....ndio visasi kesi tamu sana3 yrs to come sio leo hiiii
Na visas vyao vya kutoa uhai wa mtu, wakitiwa hatiani, watanyongwa hadi kufa kwa mujibu wa sheria, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
 
Waje na humu jf kuna walioshangilia kweli ukute ni ndugu wa hiyo familia hapo juu wakidhani mkono wa serikali ni mfupi,

Natamani Lemutuz angekua hai aone hao wauaji aliokua anawashangilia kwa kumuua msagaji wanavyopigwa mvua ya maisha,

Na hii iwe fundisho kwa wajinga wote hakuna aliye juu ya sheria, ukikoswa na sheria ya Dunia basi Mungu mwenyewe atakuadhibu kwa kujipa majukumu yasiyokua yako (ref, kwa Lemutuz hakuchukua hata mwezi)

Hongera jeshi letu la polisi, hongera serikali ya Mama Samia, naona hata humu nyuzi za Ushoga zimeisha kabisa watu wameufyata kama Mbwa kaona Chatu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom