Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kukatisha uhai wa mtu ni kosa dhidi ya jamhuri.Watu sita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita wakishtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya madini ya dhahabu (GGM) Milembe Seleman (43).
Watuhumiwa waliopandishwa mahakamani katika kesi namba 12/2023 ni Dayfath Maunga(30), Safari Labingo(54), Genja Lubingo(30), Musa Lubingo (33), Maige Fundikira (37) na Ceslia Macheni (55).
Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Johari Kijuwile, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Scolla Teffe ameieleza Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa la mauji kinyume na kifungu cha 196 & 197 cha kanuni ya adhabu .
Amedai Aprili 26, 2023 Dayfath Maunga na wenzake watano huko katika maeneo ya Mwatulole wakishirikiana kwa pamoja walimuua Milembe Seleman.
Washtakiwa hao hawakupaswa kuzungumza chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 7, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wote wamerudishwa mahabusu.
Pia Soma > Afisa Ugavi wa mgodi wa Geita, Milembe Suleiman auawa na viganja vyake kukatwa
mzazi wa marehemu Milembe Suleman aongea mazito
Mahakama itimize wajibu wake muhimu