Sitakula kwa mama nitilie labda nione nataka kufa na hakuna namna nyingine

Sitakula kwa mama nitilie labda nione nataka kufa na hakuna namna nyingine

Hi!
Naweza nikaonekana nakufuru au naringa. Hapana, huo ni msimamo wangu tu kama wewe msomaji ulivyojiapiza kwenye baadhi ya mambo.
Mimi sili kwa mama nitilie.
Kila jambo linalokataliwa basi ni tatizo, na hilo tatizo limesababishwa na jambo lingine (cause and effect). Tuambie ni tatizo gani hilo na limesababishwa na nini ili na wengine tuwe aware, pengine tunaweza kusaidia kuondoa kisababisho (cause), na hivyo kurejesha hali ya kawaida. Nadhani hiyo ni busara zaidi.
 
Kusema kwamba hautakula chakula cha mama ntilie Hadi unakufa hapo utakuwa unakosea sn

Kwa maisha ya kibongobongo,kuna wakati mama ntilie hawakwepeki,vinginevyo uwe unatembea na gari lenye mgahawa ndani Kila unapoenda

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Lunch box zimejaa madukani
Snacks zipo
Coffee bottles zipo

Plan B hizo…
 
Kimsingi mama ntilie wa bongo wachafu sana..vyakula vyao ukila huwezi maliza wiki hujaendesha..

Wanatia kinyaa sana..hasa wale wa vyakula vya buku jero buku 2.

Daah..shida hata uelewa wa usafi na usalama wa chakula hawana.

Unakuta beseni la kuoshea kaoshea vyombo toka asbuha hadi jioni habadilishi maji.

Sponji la kuoshea vyombo hilo hilo anafutia meza na viti baada ya wateja kula.

Maji ya kunywa wanakinga ya bombani au kisimani hawachemshi.

Hata kama ni umasikini hawa watu wawe controlled wanaumiza wengi sana kwa huduma zao mbovu.

*n.b.:wengi wana misambwanda hatari na ni vipezo vya wateja wao wanauza chakula na wanaliwa sana pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zile ndoo za maji asilimia kubwa huwa ni za chooni au usiku huwa zinawekwa chumbani kwa ajili ya kukojolea maana si unajua wanawake hawatokagi nje au kuchuchumaa chooni muda wa usiku hata kama choo kipo chumbani.
 
Huwa nawashangaa wale wanaokula vyakula vya mtaani, hasa chapati, sijui kachumbali, mimi huwa nazungukaga au naenda mbali kutafuta hotel, na wengine huwa wananishangaa.
Mi hata nikiwa nasafiri mkoani, ni mwendo wa soda na biscuits/korosho au karanga nilizotengeneza nyumbani, au maziwa ya pakti au chupa.
 
Kila jambo linalokataliwa basi ni tatizo, na hilo tatizo limesababishwa na jambo lingine (cause and effect). Tuambie ni tatizo gani hilo na limesababishwa na nini ili na wengine tuwe aware, pengine tunaweza kusaidia kuondoa kisababisho (cause), na hivyo kurejesha hali ya kawaida. Nadhani hiyo ni busara zaidi.
Wachawi sana
 
Ila hawa wamama wanapika vyakula hovyo hovyo mpka sio poa...si kwanini hawajiongezi angalau basi waweke mazingira masafi.
Kuna mama mmoja ye anapikiaga soko fulani, mji fulani, kitongoji fulani kikubwa tu, kwa macho yangu, nilimshuhudia anapopika maharage yanayotakiwa kutumika kesho yake asubuhi, basi anachochea moto, anaongeza maji, halafu anafunika sufuria na anaweka jiwe juu, anakwenda kulala, siku hiyo katika mishemishe zangu za usiku, nikakuta mbwa kama 7 hivi, wamesukuma sufuria, wametipa kule mfuniko, na moto ulishapoa, mbwa wakawa wanarambaramba maharage, yule mama asubuhi akawahi, nikamwambia usiuze hayo maharage akasema sawa khee! huku nyuma nimetoka, mwenzie akaniambia eti alinichukia sana, na akaamua kuyaosha na kuyapasha akawauzia wananchi!! Dah!
 
Back
Top Bottom