Sitakula kwa mama nitilie labda nione nataka kufa na hakuna namna nyingine

Sitakula kwa mama nitilie labda nione nataka kufa na hakuna namna nyingine

Ila hawa wamama wanapika vyakula hovyo hovyo mpka sio poa...si kwanini hawajiongezi angalau basi waweke mazingira masafi.
Kuna mama mmoja ye anapikiaga soko fulani, mji fulani, kitongoji fulani kikubwa tu, kwa macho yangu, nilimshuhudia anapopika maharage yanayotakiwa kutumika kesho yake asubuhi, basi anachochea moto, anaongeza maji, halafu anafunika sufuria na anaweka jiwe juu, anakwenda kulala, siku hiyo katika mishemishe zangu za usiku, nikakuta mbwa kama 7 hivi, wamesukuma sufuria, wametipa kule mfuniko, na moto ulishapoa, mbwa wakawa wanarambaramba maharage, yule mama asubuhi akawahi, nikamwambia usiuze hayo maharage akasema sawa khee! huku nyuma nimetoka, mwenzie akaniambia eti alinichukia sana, na akaamua kuyaosha na kuyapasha akawauzia wananchi!! Dah!
 
Kula mgahawani haikwepeki fanya ufanyavyo utakula tuuu , unless ule kwenye mahoteli makubwa , ya Kati , tatizo hzo huduma zinakuwa kwenye miji mikubwa , kama we ni mwanaharakati wa kitaa , utakula Tu vyakula vya mgahawani ...ni kweli wale wa mana ni wachafu Sana , na wanatia kinyaaa, lakini bado hawakwepeki
 
Lunch box zimejaa madukani
Snacks zipo
Coffee bottles zipo

Plan B hizo…
Hayo uliyoyaongea yote yanapatikana mijini..

nenda kanunue mpunga Morogoro ndanindani huko ,kilosa,dakawa na mahenge au kafanye manununuzi ya mafuta ya mawese huko kazura mimba kigoma au kanunue magunia ya mahindi huko msamala Ruvuma ili ulete mjini

Huko kote uwe unakaa zaidi ya wiki kufanya manunuzi alafu ukiwa na njaa ingia madukani kaulizie lunch box...mdogo wangu mama ntilie siyo bongo Tu,Kwa nchi zetu hizi za kimasikini ahepukiki
 
Hi!
Naweza nikaonekana nakufuru au naringa. Hapana, huo ni msimamo wangu tu kama wewe msomaji ulivyojiapiza kwenye baadhi ya mambo.
Mimi sili kwa mama nitilie.
Nimeshakuelewa sana....!Unachoogopa!/sometimes nyama zinakuwa zimelainika kweli kweli unameza uku unaomba Allah.
 
Kula mgahawani haikwepeki fanya ufanyavyo utakula tuuu , unless ule kwenye mahoteli makubwa , ya Kati , tatizo hzo huduma zinakuwa kwenye miji mikubwa , kama we ni mwanaharakati wa kitaa , utakula Tu vyakula vya mgahawani ...ni kweli wale wa mana ni wachafu Sana , na wanatia kinyaaa, lakini bado hawakwepeki
Kuna kwepeka sana tu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi mama ntilie wa bongo wachafu sana..vyakula vyao ukila huwezi maliza wiki hujaendesha..

Wanatia kinyaa sana..hasa wale wa vyakula vya buku jero buku 2.

Daah..shida hata uelewa wa usafi na usalama wa chakula hawana.

Unakuta beseni la kuoshea kaoshea vyombo toka asbuha hadi jioni habadilishi maji.

Sponji la kuoshea vyombo hilo hilo anafutia meza na viti baada ya wateja kula.

Maji ya kunywa wanakinga ya bombani au kisimani hawachemshi.

Hata kama ni umasikini hawa watu wawe controlled wanaumiza wengi sana kwa huduma zao mbovu.

*n.b.:wengi wana misambwanda hatari na ni vipezo vya wateja wao wanauza chakula na wanaliwa sana pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
1.nimewahi kula ugali dagaa was buku kwa mama ntilie nikasumbuliwa tumbo so upo sahihi Bora ukale kwa mama ntilie mwenye chakula Cha Bei kubwa
2.nimewahi kula chakula kwenye mgahawa wa Bei kidogo,wali kuku buku tatu aise niliumwa tumbo week nzima ni kuhara tu, Hospital dokta akasema chakula kile inawezekana kilikuwa na bakteria was kinyesi Cha binadamu,tulikula watu watatu wote tukaumwa,na baada ya hapo wengine nao waliumwa walionunua siku tofauti
 
Hi!
Naweza nikaonekana nakufuru au naringa. Hapana, huo ni msimamo wangu tu kama wewe msomaji ulivyojiapiza kwenye baadhi ya mambo.
Mimi sili kwa mama nitilie.
Sema ulichoshuhudia usiogope kwani nasi tunavijua vijambo vyoa wapikapo.
 
Kula kwa mama ntilie ni mwiko.

Nashauri kama hakuna namna basi kula vyakula visivyo na maandalizi mengi.

-Chips kavu
- Mihogo au viazi vya kukaanga
-Mahindi ya kuchoma

Angalizo: Usile kachumbari wala nyama yoyote ile tofauti na kitimoto cha kuchoma au kukaanga basi.
 
Naamini wamama ntilie watapita huku na kusoma wajirekebishe hasa suala la usafi vifaa vyao na mazingira.....nikiwa sekondari nilishindwa kabisa kabisa kwenda mama ntilie mkoa mmoja hapo mitaa kati....wenzangu walifurahia sana kupewa wali mwingi sana ....bei poa nilishindwa kukaa pale na kula.....nikikuwa naingia restaurant hata once kwa mwezi ....kuliko kila ijumaa kutoroka kubadili diet
 

Pitieni huku pia niliwahi kutoa taathari kwenye uandaaji wa chapati kwa kutumia sponji [emoji1312]
 
Back
Top Bottom