Sitiri Aibu Yangu , Ili Nami Nije Kustiri Yako !

Sitiri Aibu Yangu , Ili Nami Nije Kustiri Yako !

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Rejea wakati Mungu alipotaka kuteremsha gharika , alimuamuru Nuhu atengeneze Safina , na kwayo aingie na watu wake waliomuamini , aidha na wanyama wake .

Safina ilipokua majini (baharini) iliwachukua masiku kadhaa .
Nuhu hakujua safari ile ingegota lini .
Huku wanyama wake wa aina mbalimbali wakiendelea kuzaana kila uchao .

Ongezeko la wanyama likamuhofisha Nuhu , kwani Safina ilianza kuelemewa uzito , ambapo kungeweza kupelekea chombo kuzama .

Hivyo Nuhu akawaamuru wanyama wale marufuku kujamiana .
Kitu ambacho kitasababisha mimba zisiwepo , na population isiongezeke .

Wanyama wakatii amri ile .
Hata hivyo Paka walishiindwa uzalendo .
Wakawa wanabanjua amri kwa kificho sana , tena mida ya usiku mkubwa na kwenye chocho kali . (kama wafanyavyo ktk karne hii tuliyonayo)

Kwa bahati mbaya za mwizi 40 !
Siku moja Mbwa akawafumania .
Mbwa akawaambia Paka kwamba anaenda kuwasanua (ukuda) kwa Nuhu.
Pamoja na Paka kumtafadhalisha Mbwa asende kuwachongea zoezi halikufaulu .

Mbwa alifikisha ukuda kwa Nuhu .
Nuhu akaitisha wanyama wote na kuwatangazia missbehave ya Paka .
Na kisha akawapa adhabu .
Paka nao wakatamka kwamba wameskitika sana na kuumbuliwa , na kwao ni fedheha .

Masiku kadhaa yakapita , Paka wakiwa walishajiambia hawatorudia tena kuhalifu amri ya Nuhu .

Kumbe Mbwa kwa wakati huo wakatumia loophole ya kuonekana wao ni wapeleka habari kwa mkuu , hivyo Nuhu asingekua na doubt nao .
Hivyo wakaanza nao kubanduana kwa siri .
Na kwa bahati mbaya Paka ndy aliyewafumania .

Paka wakaona wao wapeleke shtaka kwa Mungu moja kwa moja !
Wakamwambia Mungu :
"Tunakuomba mfedheheshe Mbwa kuliko alivyotufedhehesha sisi "

Na kweli fedheha ikashuka kwa Mbwa .
Wakaambiwa kuanzia leo hadi mwisho wa dunia kujamiana kwa Paka kutakua kwa stara na siri kiasi hata mmiliki wao (binadamu) haitakua rahisi kuwaona .
Na nyie Mbwa kujamiiana kwenu kutakua kwa fedheha hadi mwisho wa dunia .

Ndiyo tunachokishuhudia leo , ni rahisi sana kuwakuta Mbwa saa 6 mchana , karibu ya soko wameng'ang'aniana ! Mmoja kaelekea Temeke mwingine Ilala . Si ajabu Jike 1 , madume matano , na yote yatasakafia mzigo.

Note : Uonapo aibu ya mwenzako, funika ili nae aje afiche yako .
 
Judgement, kwani aibu yako ni ipi hadi uandike yooote hayo?
 
Last edited by a moderator:
Unajihami eeh? Aaah wapi, no compromise here.

Afu umenifikirisha kitu, kule kwenye safina huduma za toilet kwa miaka 40 ilikuwaje?

Kuhusu kadhia hiyo , inasemekana kua mara vinyesi vilipojaa Safinani , Nuhu aliselect mmoja wanyama wanyama ale waste products , na ndiyo Safina isafishike .
Na ndipo Nguruwe alipopewa jukumu hilo .
 
Safi sana bwana Judgement kwa mawazo yako mazuri kesho tena mkuu
 
Safi sana bwana Judgement kwa mawazo yako mazuri kesho tena mkuu

Asante Bibie Ladymasa , mawazo yenye afya hapa Jeiefu ndo pahala pake! Nisalimie mpenzi wako , if unae
if huna jisalimie mwenyewe .
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
ujumbe mzuri sana ama kweli ficha aibu ya mwenzio ili kesho nae afiche yako

Kuna watoao aibu za wapendwa ndugu/friends/waumini/roommate/classmate wao, na ukijawatambua , hukiri kwa nyuso kavu , na wala hawajutii .
 
Back
Top Bottom