Ladymasa
JF-Expert Member
- Oct 2, 2013
- 877
- 335
Nadhani umeshapata jibu, wifi yangu hajambo? na ninani?
kiwatengu kos alangu ni lipi hapohuyu ni mke wa mtu ati..
kizuri kula na nduguyo...Umeonaeeeeeeeeeeeeeee! chako changu changu chako, lakini usifike mbali bak hapohapo Mkuu
huyu ni mke wa mtu ati..
Shemeji Ladymasa currently sina Spousemate , eventhough huko nyuma nimepata kua na Spouses wa3 tofauti for different terms .
anataka kumjua wifi yake ni nani bestito mjibu hilo
ladyfurahia mbona una maswali mengi ? Kwani we ni polisi?
Nway muachie tu taratibu utamjua.
Mm sio polisi ni afisa usalama wa taifa wa wanandoa wa humu mjengoni
Alaa kumbe hapa kuna kitengo cha ushushu ?
Nway nawaaminia wadau wa jukwaa hili kwa kujimilikisha mivyeo .
Btw unakuaje utumike kunako issues za ndoa , ilhali we mwenyewe si mdau wa ndoa?
Sisemei ile ndoa original nje ya Jf , nasemea ya humu mjengoni (online kopo) hiyo ndo ma'points .
Rejea wakati Mungu alipotaka kuteremsha gharika , alimuamuru Nuhu atengeneze Safina , na kwayo aingie na watu wake waliomuamini , aidha na wanyama wake .
Safina ilipokua majini (baharini) iliwachukua masiku kadhaa .
Nuhu hakujua safari ile ingegota lini .
Huku wanyama wake wa aina mbalimbali wakiendelea kuzaana kila uchao .
Ongezeko la wanyama likamuhofisha Nuhu , kwani Safina ilianza kuelemewa uzito , ambapo kungeweza kupelekea chombo kuzama .
Hivyo Nuhu akawaamuru wanyama wale marufuku kujamiana .
Kitu ambacho kitasababisha mimba zisiwepo , na population isiongezeke .
Wanyama wakatii amri ile .
Hata hivyo Paka walishiindwa uzalendo .
Wakawa wanabanjua amri kwa kificho sana , tena mida ya usiku mkubwa na kwenye chocho kali . (kama wafanyavyo ktk karne hii tuliyonayo)
Kwa bahati mbaya za mwizi 40 !
Siku moja Mbwa akawafumania .
Mbwa akawaambia Paka kwamba anaenda kuwasanua (ukuda) kwa Nuhu.
Pamoja na Paka kumtafadhalisha Mbwa asende kuwachongea zoezi halikufaulu .
Mbwa alifikisha ukuda kwa Nuhu .
Nuhu akaitisha wanyama wote na kuwatangazia missbehave ya Paka .
Na kisha akawapa adhabu .
Paka nao wakatamka kwamba wameskitika sana na kuumbuliwa , na kwao ni fedheha .
Masiku kadhaa yakapita , Paka wakiwa walishajiambia hawatorudia tena kuhalifu amri ya Nuhu .
Kumbe Mbwa kwa wakati huo wakatumia loophole ya kuonekana wao ni wapeleka habari kwa mkuu , hivyo Nuhu asingekua na doubt nao .
Hivyo wakaanza nao kubanduana kwa siri .
Na kwa bahati mbaya Paka ndy aliyewafumania .
Paka wakaona wao wapeleke shtaka kwa Mungu moja kwa moja !
Wakamwambia Mungu :
"Tunakuomba mfedheheshe Mbwa kuliko alivyotufedhehesha sisi "
Na kweli fedheha ikashuka kwa Mbwa .
Wakaambiwa kuanzia leo hadi mwisho wa dunia kujamiana kwa Paka kutakua kwa stara na siri kiasi hata mmiliki wao (binadamu) haitakua rahisi kuwaona .
Na nyie Mbwa kujamiiana kwenu kutakua kwa fedheha hadi mwisho wa dunia .
Ndiyo tunachokishuhudia leo , ni rahisi sana kuwakuta Mbwa saa 6 mchana , karibu ya soko wameng'ang'aniana ! Mmoja kaelekea Temeke mwingine Ilala . Si ajabu Jike 1 , madume matano , na yote yatasakafia mzigo.
Note : Uonapo aibu ya mwenzako, funika ili nae aje afiche yako .