Rejea wakati Mungu alipotaka kuteremsha gharika , alimuamuru Nuhu atengeneze Safina , na kwayo aingie na watu wake waliomuamini , aidha na wanyama wake .
Safina ilipokua majini (baharini) iliwachukua masiku kadhaa .
Nuhu hakujua safari ile ingegota lini .
Huku wanyama wake wa aina mbalimbali wakiendelea kuzaana kila uchao .
Ongezeko la wanyama likamuhofisha Nuhu , kwani Safina ilianza kuelemewa uzito , ambapo kungeweza kupelekea chombo kuzama .
Hivyo Nuhu akawaamuru wanyama wale marufuku kujamiana .
Kitu ambacho kitasababisha mimba zisiwepo , na population isiongezeke .
Wanyama wakatii amri ile .
Hata hivyo Paka walishiindwa uzalendo .
Wakawa wanabanjua amri kwa kificho sana , tena mida ya usiku mkubwa na kwenye chocho kali . (kama wafanyavyo ktk karne hii tuliyonayo)
Kwa bahati mbaya za mwizi 40 !
Siku moja Mbwa akawafumania .
Mbwa akawaambia Paka kwamba anaenda kuwasanua (ukuda) kwa Nuhu.
Pamoja na Paka kumtafadhalisha Mbwa asende kuwachongea zoezi halikufaulu .
Mbwa alifikisha ukuda kwa Nuhu .
Nuhu akaitisha wanyama wote na kuwatangazia missbehave ya Paka .
Na kisha akawapa adhabu .
Paka nao wakatamka kwamba wameskitika sana na kuumbuliwa , na kwao ni fedheha .
Masiku kadhaa yakapita , Paka wakiwa walishajiambia hawatorudia tena kuhalifu amri ya Nuhu .
Kumbe Mbwa kwa wakati huo wakatumia loophole ya kuonekana wao ni wapeleka habari kwa mkuu , hivyo Nuhu asingekua na doubt nao .
Hivyo wakaanza nao kubanduana kwa siri .
Na kwa bahati mbaya Paka ndy aliyewafumania .
Paka wakaona wao wapeleke shtaka kwa Mungu moja kwa moja !
Wakamwambia Mungu :
"Tunakuomba mfedheheshe Mbwa kuliko alivyotufedhehesha sisi "
Na kweli fedheha ikashuka kwa Mbwa .
Wakaambiwa kuanzia leo hadi mwisho wa dunia kujamiana kwa Paka kutakua kwa stara na siri kiasi hata mmiliki wao (binadamu) haitakua rahisi kuwaona .
Na nyie Mbwa kujamiiana kwenu kutakua kwa fedheha hadi mwisho wa dunia .
Ndiyo tunachokishuhudia leo , ni rahisi sana kuwakuta Mbwa saa 6 mchana , karibu ya soko wameng'ang'aniana ! Mmoja kaelekea Temeke mwingine Ilala . Si ajabu Jike 1 , madume matano , na yote yatasakafia mzigo.
Note : Uonapo aibu ya mwenzako, funika ili nae aje afiche yako .