Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

----SEHEMU YA TANO - - -

Wale majamaa walipotoka kwenye uvungu wa bus ghafla wakanizingira wengine nyuma wengine mbele, nilipandwa na hasira nikajisemea moyoni "atakaegusa hili begi ama zangu ama zake". Kile kijamaa kigonvi kuliko wote kikataka kuchomoa kisu nikamuhawi kumkamata mikono nikampiga kichwa akadondoka wale wengine waliokuwa mbele yangu nikaona wamehamaki kabla ya kuchukua reaction yoyote nikampiga mmojawapo mtama wa kufa mtu nae chali, yule watatu sikumuona sijui alipoteaje ila kile kingine nilichokipiga kichwa nikaona kanaamka nikakandamiza kifuani na buti yangu, kule walinzi hawajui kitu maana ilikuwa ni silent league. Kutazama haraka nyuma naona yule mwingine hayupo akawa anakaita kajamaa ili wakimbie na mimi nikaona nikaachie mwanya kijanja ili kisepe. Kaliondoka chapu wakaenda kupanda pikipiki yao ilikuwa nyuma ya jengo la stend.

Nikiwa nahema sana tena kwa nguvu nilijiona sipo Sawa kabisa maana kama ndomaisha ni kutafuta sio hivi tena ilifika wakati hata ningeona banda la nguruwe Walah ningejiegesha kwenye matope maana ni banda linanistiri. Sikujua tena ule mda ni saa ngapi ila kwakuhisi ilikuwa ni majira ya saa kumi kasoro. Nikiwa nimeduwaa Sina hili wala lile nikasikia kishindo kizito puuuuuuuuh!!! Nikashtuka kuangalia chini ni bonge la jiwe sikujua limetoka wapi nikasema mpwayungu village hapa utakufa hawa watu hawana Nia njema inabidi uondoke. Shida ni kuwa hata nikiondoka naenda wapi?? Ile najiuliza nikaona jiwe limeshuka karibu na miguu yangu huku nikiskia sauti kwa mbali tuliaaaa huyu Leo Tupo nae anamaliza sisi tunaanza. Niliposkia hivo ikabidi niondoke hapo nikaenda tena kwa yule mlinzi awamu hii nikasema acha aniuwe tu saa nitaenda wapi mm jamani.

Kusema kweli sikujua wale jamaa kwa nini walikuwa hawasogei kwenye office za mashalah alipo huyu mlinzi lakini huenda wanajulikana kwa tabia zao ovu. Ile nimefika tu kwa mlinzi ikabidi nigonge mlango mlinzi akafungua nikasema kwa haraka samahani nimekuja kukata ticket. Mlinzi aliniangaliaaa mwishowe akasema weka begi hapo subiri wenyewe waje, namm nikamwambia haina shida ila naomba nijiegeshe hapa mpaka patakapopambazuka yule mlinzi sijui nini kilimkuta au kubadili fikra zake mpaka awe mwelewa kiasi kile. Nikaona katoa shuka lake akasema lala hapo. Sikuweza kuamini kwa mara nyingine naenda kupumzisha mwili wangu mida ya saa kumi usiku. Nikamwambia yule mlinzi Asante sana mungu akubariki mm nitakata tiketi ya saa moja, nimewahi tu mapema siti zinaweza kujaa, mlinzi akanielewa.

Mda huo nikiwa nimesimana kabla ya kulala nikaona kimya kizito sijui wake vibaka walienda wapi tena, kumbuka pale nje Kuna yule jamaa ambae alikuwa amelewa, nikaona kaamka nikasema hapa kazi ipo sijui nitaanza kutukanwa tena. Ahse nilidondosha chozi maana shida zote nilizopitia zilikuwa na maumivu makali sana, yani Sina pesa then wale vibaka wakawa wanataka chochote kitu, ila kama baada ya dakika 3 hivi hali yangu ikakaa sawa. Yule mlevi akaamka akaja akasukuma mlango kwa nguvu nikajiuliza nini tena?. Yule mlinzi akasikika akimwambia atoe mizigo na magunia yaliyopo mle ndani maana kumepambazuka. Sasa ajabu ni kuwa Ile booking office ni ndogo ili atoe Ile mizigo inabidi nisilale nitoke nje maana hakuna nafasi. Nikasema rahaulah!!!, kwa hiyo silali. Yule mlinzi akasema mwambie huyo mteja atoke hapo ndani.

Kwahiyo swala la kulala ikawa basi tena nasikutaka kujionesha nina dhiki na usingizi maana wangeshtuka kumbe mimi sio abiria and for sure sikuwa mteja Bali nilienda tu kukwepa ngumi za vibaka. Lakin wazo likaja ghafla kwanini nisilale alipokuwa amelala huyu mlevi. Mm nikaona haina shida ngoja nilale, Ile kwenda kuangalia mazingira ya yule mlevi alipokuwa amelala kumbe alijikojorea tena kojo jingi limechimba mpaka mfereji halafu pananuka. Miguu ilikufa gazi kwakweli ilibidi kujitoa ufahamu nilale hivyo hivyo japo nilijiuliza nikiamka asubuhi siwatasema mm ndonimejikojorea. Nikasema Poteleapote mimi navua begi langu naweka hapo ndani nilale Sasa.
Ile navua begi ili nilale nakuta limeyepuka zipu imefunguka bahasha yangu yenye vyeti siioni na baadhi ya nguo zilizokuwa juujuu,..... Ni simanzi nzito..zaidi ya maiti iliyofufuka ndani ya kaburi.

........ Inaendelea usichoke.......

Hii chai, maeneo ya Stand, kibaka hawezi kuwa na ujasiri sijui wa kunificha chin ya gari kukungoja wewe usiye na hela, na vyeti vya nini.

Inawezekana ni kweli ila umeongeza uongo mwingi, sehemu hii ya Vibaka imeharibu uhalali wa andiko lako kwa 100%
 
Inawezekana ni kweli ila umeongeza uongo mwingi, sehemu hii ya Vibaka imeharibu uhalali wa andiko lako kwa 100
 
-----SEHEMU YA TATU - - - -

Konda wa bus la MASHALAH alipotangaza kituo yule jamaa aliekanyaga samaki zangu akasogea mbele bus likasimama jamaa akashuka. Nikiwa nimeinama chini nikijikuta nadondosha chozi huku namkumbuka mama alikuwa akiniambia "Mwanangu mpwayungu village kabla hujafanya maamuzi fikiri kwanza". Maamuzi niliyokurupuka Kuanza safari ya kwenda kilwa ilihali mm sio mmakonde wala mmwera nasina ndugu wala kibarua cha kwenda kufanya maamuzi haya yaliniweka kwenye wakati mzito sana. Ghafla mama wa samaki akafika nikasikia sauti nikiwa nimeinama inasema "kaka samahani naomba 2000 nataka kushuka" lakini kwa kuwa nilikuwa kwenye msongo mkubwa wa mawazo wa kupotelewa pesa plus njaa sikuweza kumjibu zaidi ya kukaa kimya nikiwa nimeinamia siti, yule mama nikasikia analalama we mkaka nataka kushuka mbona hunijibu nataka pesa yangu aliongea kwa sauti ya radi yenye mrindimo nadhani alikuwa mndengereko wa rufiji huyu. Ilinibidi niamke kukumbana na fedheha nikamjibu kuwa mama sio tu 2000 hapa sina hata Mia pesa zangu zote sizioni maana zilikuwa kwenye pochi. Yule mama nikaona ameshika kola yangu nilikuwa nimevaa Shati jeupe akasema hunijui sikujui nilikupa samaki wakiwa wazuri naomba pesa yangu natafuta riziki sikuja kuimba injili.

Aliponishika Ile kola yule babu wa pembeni yangu nikaona anamuongelesha kilugha sikuelewa ni lugha gani baada ya maongezi mengi yenye kerere nikaona yule babu kaingia mfukoni akampa mama wa samaki shilingi 1000 nasio 2000 yule mama alipopokea nikaona kaachia Shati langu akachukua beseni kwa hasira akaenda kukaa mbele karibu na dreva pale chini yake huwa hakunaga kiti ila unaweza kaa pia hususani hawa wachuuzi wa kupanda na kushuka. Yule babu akiniambia kijana kuwa na Amani nimempa pesa yake nikasema asante sana halafu nikakaa kimya. Bus likiwa kwenye mwendo kasi huku upepo unapukuta kufungua dirisha niangalie nje nikaona kumbe usiku umeingia. Nikasema hapa nikikaa kimya sitapata msaada wowote ikabidi nimwambie mzee tuliekuwa tumekaa nae hali halisi, yule mzee akanipa pole Kisha nikamwambia mm huku niendako ni mgeni sina mtu yoyote ninae mjua nimekuja kutafuta maisha. Yule mzee akasema hata yeye anaenda kwa mtoto wake ameoa juzi Kati kwahiyo anaenda kuwasalimia na kule ni mgeni pia ila ingekuwa ni somanga angeongea mengine. Nikasema hapa nimebugi hii safari ni ngumu kuliko ya wana wa Israel kuitafuta kanani.

Saa mbili usiku tukaingia stend ndogo hivi niyavumbi nikasikia konda anasema haya jamani wa kilwa kivinje teremkeni. Yule mzee akaniaga akashuka nikabaki peke angu. Nikiwa Sina hata Mia mfukoni saa mbili na nusu usiku bus likaiacha kilwa kivinje safari ya kuelekea kilwa masoko ikaanza. Nikawa najiuliza ivi nikishafika pale stend halafu naelekea wapi usiku huu, Shati lenyewe yule mama alilikunjakunja kalipaka mishombo ya samaki limechafuka siwataniona kibaka?. Nikasema sawa wacha tufike itafahamika tu maadam niendako ni watanzania wenzangu. Saa tatu na nusu hivi tukaingia kilwa masoko nandomwisho wa safari. Pale Kuna bodaboda nyingi vijana wa pale hawalali wakajazana kwenye mlango wa bus kutafuta abiria mkono uende kinywani, nikashuka nikapewa begi langu kwenye buti nikalibeba, bodaboda kila baada ya dakika mbili wanakuja vipi bro boda nawajibu Sina haja ya usafiri lakini wanarudi tena kuniuliza mwishowe nikatoka kwa mguu pale stend nikajisogeza pembeni kidogo nikakuta Kuna prutable wanacheza hapo ikawa kama ni saa nne na nusu hivi.

Nikiwa na begi langu kama mkimbizi mida ya saa tano yule mwenye prutable akaja akasema jamani nafunga nendeni mkalale, nikasema hapa sasa kazi ipo, nikaona wale vijana wanapita Kwangu kuniuliza tena kama ni abiria nikawa na jitahidi kuwa jibu kistaarabu kwamba siendi kokote ila ingekuwa kwetu mpwayungu wangeshapokea matusi, mwishowe wote wakaondoka. Sasa tukabaki mimi na yule mwenye prutable japo niliona ana kibanda cha vinywaji pia maana alikuwa anafunga. Anataka kuondoka tu nikamuwahi akasema wewe nani nikajieleza matukio yote yaliyotokea yule kijana akasema hapana siwezi kukupa msaada wowote maana saizi binadamu tumegeuka nyoka. Ikabidi aniache tena akasema nitoke pale sehemu yake ya kazi kwa ajili ya usalama wa mali zake. Ikawa ni saa sita usiku giza tororo Sina PA kwenda Sina hata Mia njaa inanipukuta, usingizi nikawa Sina kabisa kutokana na mashambulizi ya misukosuko.

Nikaona kukaa maeneo yale hapafai Sasa naenda wapi?? Kwa mbali nikasikia mziki unaunguruma nikasema huko huko naenda nikafata Ile sauti Kuna barabara ya mchanga ikawa inaenda mpaka kwenye huko mziki kumbe Kuna disco na watoto wa kike mle japo siwezi Sema ni watoto wakali maana hata hamu ya kuangalia Kuna nini humo sikuwanayo kabisa. Ile nafika tu disco ikawa imezimwa nikaona lundo la watu wa naondoka na vidada poa ila kwa muonekano vile vidada poa vimekubuhu vimefanya sana umalaya kimboka vikichuja vinaenda huko pembeni ya mji kuwa kamata maboya. Kila mtu alikuwa ananishangaa jinsi nilivyo maana wanajiuliza huyu wa wapi usiku huu na mbegi nzito halafu Shati haitamaniki sura ngeni?. Saa saba kamili kwenye Ile disco hapa kuwa na mtu tena. Sasa tukabaki mm na wale wahudumu wa ule ukumbi wa disco nikawafata nikawaambia maswahibu yangu wakasema msaada peke watakaonipa nikunipeleka kituo cha polisi maana pale naweza Pata pakujistiri.

Nikasema kwani kituo cha polisi Kuna vitanda vya kulala wageni, wakacheka kidogo huku wakiendelea kupanga maspika yao na manyaya Kisha wakajibu kuwa polisi hawawezi kukosa pakukuweka maana ni binadamu kama mm, ila wao kunipokea ngumu kwa sababu juzi Kati Kuna tukio kubwa lilitokea la mtu kuuawa kwenye njumba yake kwahiyo polisi kila siku wanasisitiza tusipokee wageni ambao hatuwafahamu. Nikaona kwenda kuomba msaada polisi huo ni uongo ngoja niendelee kuwashawishi tu. Nikawaambia kama hawana Imani na mimi nitawakabidhi hata vyeti vyangu vya shule bado walikataa wakafunga wakaondoka nikabaki peke angu. Ikawa ni saa saba na nusu hivi. Giza likawa totoro sauti pekee nilizoziskia ni za chura kwenye madibwi na bodaboda za wahuni wasiolala usiku.

Kukaa pale niliogopa sana maana lile eneo limejitenga nikasema hapa nirudi stend nilipotoka, nikafika stend Ile kufika tu Kuna vijana watatu nikakuta wamekaa kwenye bench moja hivi pembeni ya barabara ya lami karibu na stend nikasema hapo powa ngoja niende tupige story mpaka asubuhi. Nilipo fika nikasalimia wakasema mbona upo na begi usiku nikasema kawaida tu ila asubuhi nataka niende Dar kwa hiyo nasafiri ~niliwadanganya maana sio kila mtu wa kumwambia unayoyapitia kwa mda huo utaonekana mwehu angalia na nature ya Eneo. Kuna kijamaa flani hivi ni cheupe kirefu kiasi afu chembamba kikaja pale kikasema oya huyu Nani mazee mbona sura ngeni wakamjibu lakini kile kijamaa nikishari sana nadhani kakajua huyu nimeokota Leo. Kuna jamaa mmoja umri umeenda kiasi akasema mwache unamuhoji wa nini kila mtu na maisha yake. Yule jamaa akavutwa pembeni na hiki kushkaji kigomvi akapewa nadhani ilikuwa bangi Ile jamaa nikasikia anasema shukurani mtu wangu ngoja nikalale. Kumbe aliambiwa chukua bangi huyu mtu tuachie kwa nilivyohisi.

Wakabaki watatu Sasa hawa wote nilikuja kugundua ni vibaka wanaosumbua mji baadae nitaeleza. Kile kijama kikaja kilikuwa na bodaboda mbaya zaidi haina plate number. Kakasema ebu nitoe buku ten nakurudishia. Nikajisemea moyoni kumbe huku pesa ni rahisi kiasi hiki? Yani hata simjui tayari nimpe pesa lakini kwa kuwa nimejua hawana Nia nzuri ngoja tuone. Nikasema Sina hata Mia jamaa wenzake wawili wakakaa nyuma yangu wakasema nyie ndo wezi mnakuja kilwa kuiba mnatoroka usiku huu saa saba Kuna bus gani la Dar ebu fungua Hilo beg. Nikafungua begi haraka maana sura zao hata maongezi yalibadilika ghafla, nilitamani mda huo hata Gari ya polisi ipite lakini Hola sikuskia hata sauti za pikipiki. Majamaa wakasachi begi walipoona hamna kitu wakaona vyeti vyangu vya form 4 na form six. Kile kijamaa kikawaambia oyaaaa chukua hivyo vyeti pesa atatoa. Niliposkia hivyo nikasema bora mniue cheti hakitoki Ile nashangaa nikaona kile kijamaa kimetoa kisu kikasema hiki kisu kina rangi gani nikajibu haraka nyekundu. Kikasema basi hatuogopi kukutoboa macho maana sisi hatuui sisi tunakupa ukilema tu. Jamani watu wa kilwa mtanisamehe ila mna roho mbaya Sana.
Ile nataka kuzuia begi langu kile kijama kikasogeza kisu kwenye jicho langu.

....... I naendelea........
Elimu ya tanzania sio kwa ajili ya kututoa ujinga n kwa ajili ya kupata cheti,form six leaver unaandika prutable??

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hii chai, maeneo ya Stand, kibaka hawezi kuwa na ujasiri sijui wa kunificha chin ya gari kukungoja wewe usiye na hela, na vyeti vya nini.

Inawezekana ni kweli ila umeongeza uongo mwingi, sehemu hii ya Vibaka imeharibu uhalali wa andiko lako kwa 100%
Mkuu wewe soma tu kama burudani ila hii hadithi haina ukweli wowote japo mtunzi amejaribu kuihusisha na uhalisia
 
Hii chai, maeneo ya Stand, kibaka hawezi kuwa na ujasiri sijui wa kunificha chin ya gari kukungoja wewe usiye na hela, na vyeti vya nini.

Inawezekana ni kweli ila umeongeza uongo mwingi, sehemu hii ya Vibaka imeharibu uhalali wa andiko lako kwa 100%
Umeshawahi iona stend ya kilwa masoko?. Ile stend inalaza bus moja tu la MASHALAH na hakuna bus lolote la Dar to kilwa zaidi ya hilo kwahiyo ikifika saa sita hakuna mtu hata mmoja zaidi ya wahuni
 
Back
Top Bottom