Sitosahau siku niliyotishiwa bunduki na baba!

Baba yako alifanya kosa la jinai alitakiwa awe jela kutumikia kifungo cha miaka 30.
Inawezekana anamilikishwa silaha huku ana matatizo ya akili, silaha huruhusiwi kuielekezea kiumbe chochote kile hata kama una uhakika wa 100% kuwa haina risasi
upo sahihi kabisa, hata kesho nikiamua naweza mshtaki. lakini sitothubutu.
 
Mkuu sioni kama kuna kitu cha kulipiza hapo, na inabidi umuombe mzee wako akufundishe kuwa na strength aliyonayo. Kilichotokea ni kwamba mzee wako aliona huyo jamaa ni mjinga kama wajinga wengine na ndio maana hakuangaika nae. Unadhazani kwa umri aliofikisha amesha tukanwa na wangapi?
Mambo mengine ni kuyadharua tu, ukilipiza na wewe unaonekana ni mjinga pia.
 
safi sana, enenda nao hivyohivyo.
 
pole mkuu watu wa Dini wanasema samehe Saba mara sabini
Ila kwangu ukinifanyia ubaya mara Moja nakulipa mara Saba yake
Ila Mimi nakuapia hiyo jamaa ningemlia taiming ningemgonga vitasaaa mpaka maji aite mma pumbaf Hawa jamaa ukiwachekea Sana wanajitoaga ufahamu na kujiona malegend hivi
Narudia huyo boya angemtukana mshua wangu pale pale angechezea kipigo Cha mbwa Koko Tena kile Cha kustukiza anatolewa roki Kama general Mo Power!
 
πŸ˜ƒ πŸ™ŒπŸΎ πŸ™ŒπŸΎ
 
Afya ya akili ni tatizo kubwa sana bongo maana wengi hukuzwa wakiamini matumizi ya nguvu ndio njia pekee ya kumshape mtoto. Mwisho wa siku tunapata watu ambao kimaisha wapo fresh ila kihisia na kiakili wameathirika sanaa na hawajui

unashangaa upo kwenye usafiri wa umma au popote pale, unakuta kitu kidogo tu, mtu anapanic na kuvimba kuwa "atapigana". Yaani mtu anategemea misuli zaidi maana ndo ina nguvu ila kihisia na kiakili mwepesi sana
 
nafikiri afya ya akili Tanzania sio ugonjwa, wengi tumeathirika na hatujitambui
 
Kama amekupa besties in life basi usingemdhalilisha kwa kumuanika hapa alivyo short tempered.

Kukutishia bunduki na kusema uache mambo ya kijinga maana yake ni kwamba anaamini vijana hawapaswi kuwa na uhuru wao na maamuzi yao.
 
Huyo mzee wako ndo kizazi cha wababa waliokuwa baba kwelikweli. Nakumbuka nikiwa primary std IV ilikuwa likizo so tukawa tunaenda shule kwa masomo ya ziada.

Basi siku moja tumemaliza kipindi tukaruhusiwa na mwalimu twende nyumbani ilikuwa jioni ya saa 10. Basi badala ya kwenda nyumbani nkaambatana na wenzangu kwenda ziwani kuvua samaki kwa ndoano. Kwangu ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza baada ya kushawishiwa Sana.

Bass bhana hilo zoezi liliendelea mpaka giza likaingia. Hadi nafika home ishatimia saa 3 usiku jamaa walikuwa wamenipa samaki sita aina ya tilapia. Da kufika home Hilo balaa lake sitakuja kusahau mzee alinipa kipigo kisichokuwa cha nchii hii. Maza anaingilia kunitetea naye akapitiwa na fimbo. Nikasusiwa hao samaki niwale mwenyewe. Usiku huo nililala mwili wote maumivu kesho yake wale samaki nimewapika nkala mmoja wengine nkawapa mbwa na paka. Nakumbuka ndo mara ya mwisho mzee alinipiga Ila no kipigo siwezi sahau. Mzee wangu alitutoka ni miaka 11 Sasa na
Mungu azidi kumrehemu kwani alikuwa hataki ujingaujinga. Tuwe tunawakumbuka wazee wetu.
 
pole sana kaka, wazee wetu ni watu bora sana. R I P mzee wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…