Ashampoo burning
JF-Expert Member
- May 12, 2023
- 593
- 2,219
- Thread starter
- #301
Umekaa mitaa choka sana sisi tulifikia mtaa unaitwa pipeline ndo kulikuwa uzunguni nyumba zina angalizika kwa mbali mwaka 96 nyumba nzuri kidogo na vihela kiukweli vilikuwepo tulitoka navyo dar vya uamisho wa maza tukapanga pipelineNakumbuka mitaa ya Kinyanambo mafinga tuliosoma huko ila hapakuwa na pisi
baadae ndo tukamia huo mtaa wa mikosi wenye jina la herufi tu 2003...... mtaa wa kishua sana miaka hiyo ndo majanga yalipo anzia ... na kwanini nilijua majirani zetu wanakufa kwa ukimwi mama angu alikuwa nurse so alikuwa anapiga story tunasikiliza pia alikuwa anawauguza wakiwa hoi pale mafinga hospital...
pamoja na u unurse wake ukimwi ulikuja kum bamiza RIP my mumy...sitosahau ulivyoniangalia those dying eyes my god niliumia mara mwisho na kuniambia napenda harufu(perfume nilipaka) yako mwanangu nikasema bye ukajibu bye ndo maongezi yetu ya mwisho i will always love you ...leo naandika haya tribute yako pia kuwaasa wengine.... nikapanda basi la abc kurudi dar nikijua sito kuona tena ..kweli baada week tatu kaka angu alinipigia simu kusema mama is no more....
Tulificha kifo cha kusema kafa tu kwa presha ila ilikuwa AIDS .... hata wanangu nitakuja kuwasilimua hii story ya ule mtaa na hakuna hata sehemu.nimedanganya wala kusingizia maana maza alikuwa nurse so alijua hali za watu wengi wakilazwa
Mbaya zaidi mwaka 99 waliweka hodi maalumu la watu wa HIV so ukiwa huna hela afu una ukimwi unasekwa huko nadhani ile hodi walikuja kuivunja kuondoa unyanyapaaa ilikuwa chini kabisa kule
Nimesimulia story asilimia 5% tano tu ya majanga nilishuhudia mafinga why niliyajua mengi nilikuwa mtoto wa nurse tena mtoto pendwa.....
Asanteni wadau uzi wangu umesomwa na watu wengi naamini umetoa elimu kubwa kuhusu hili gonjwa ..
Wengine wanasema bora ukimwi kuliko kansa...ni hivi ukiwa na ukimwi hata kansa unapata kiu rahisi mno yaani ukimwi ni kama boss la magonjwa yote linapiga simu moja kansa njoo mara moja inakuja....likiamua kumwite chawa wake TB fasta tu.... bado kijana wake mkanda jeshi
Ukimwi ni boss wa magonjwa ukiamua inaweza sema basi tumvuruge awe kichaa unakuwa kichaa madaktar wanajua hili yaani ninaposema UKIMWI ni boss la magonjwa yote namaanisha linaweza sema tuletee vidonda tu utapata hadi ufe
Hizo kansa kwa watu wenye ukimwi ndo nyumbani maana boss wao ukimwi si anakuwepo ndani utashangaa unapata kidonda hakiponi then kansa
AIDS SIO MCHEZO