Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Nakumbuka mitaa ya Kinyanambo mafinga tuliosoma huko ila hapakuwa na pisi
Umekaa mitaa choka sana sisi tulifikia mtaa unaitwa pipeline ndo kulikuwa uzunguni nyumba zina angalizika kwa mbali mwaka 96 nyumba nzuri kidogo na vihela kiukweli vilikuwepo tulitoka navyo dar vya uamisho wa maza tukapanga pipeline

baadae ndo tukamia huo mtaa wa mikosi wenye jina la herufi tu 2003...... mtaa wa kishua sana miaka hiyo ndo majanga yalipo anzia ... na kwanini nilijua majirani zetu wanakufa kwa ukimwi mama angu alikuwa nurse so alikuwa anapiga story tunasikiliza pia alikuwa anawauguza wakiwa hoi pale mafinga hospital...

pamoja na u unurse wake ukimwi ulikuja kum bamiza RIP my mumy...sitosahau ulivyoniangalia those dying eyes my god niliumia mara mwisho na kuniambia napenda harufu(perfume nilipaka) yako mwanangu nikasema bye ukajibu bye ndo maongezi yetu ya mwisho i will always love you ...leo naandika haya tribute yako pia kuwaasa wengine.... nikapanda basi la abc kurudi dar nikijua sito kuona tena ..kweli baada week tatu kaka angu alinipigia simu kusema mama is no more....

Tulificha kifo cha kusema kafa tu kwa presha ila ilikuwa AIDS .... hata wanangu nitakuja kuwasilimua hii story ya ule mtaa na hakuna hata sehemu.nimedanganya wala kusingizia maana maza alikuwa nurse so alijua hali za watu wengi wakilazwa

Mbaya zaidi mwaka 99 waliweka hodi maalumu la watu wa HIV so ukiwa huna hela afu una ukimwi unasekwa huko nadhani ile hodi walikuja kuivunja kuondoa unyanyapaaa ilikuwa chini kabisa kule

Nimesimulia story asilimia 5% tano tu ya majanga nilishuhudia mafinga why niliyajua mengi nilikuwa mtoto wa nurse tena mtoto pendwa.....

Asanteni wadau uzi wangu umesomwa na watu wengi naamini umetoa elimu kubwa kuhusu hili gonjwa ..

Wengine wanasema bora ukimwi kuliko kansa...ni hivi ukiwa na ukimwi hata kansa unapata kiu rahisi mno yaani ukimwi ni kama boss la magonjwa yote linapiga simu moja kansa njoo mara moja inakuja....likiamua kumwite chawa wake TB fasta tu.... bado kijana wake mkanda jeshi

Ukimwi ni boss wa magonjwa ukiamua inaweza sema basi tumvuruge awe kichaa unakuwa kichaa madaktar wanajua hili yaani ninaposema UKIMWI ni boss la magonjwa yote namaanisha linaweza sema tuletee vidonda tu utapata hadi ufe

Hizo kansa kwa watu wenye ukimwi ndo nyumbani maana boss wao ukimwi si anakuwepo ndani utashangaa unapata kidonda hakiponi then kansa

AIDS SIO MCHEZO
 
dunia hii ina.mambo hata shetani atakataa hakueatuma kufanya hivyo
 

RIP Genius CowBama
 
Kuna kijiji kimoja mkoa wa Kagera watu walikuwa na tabia ya kumegeana wake. Ngoma ilikuja ikaingia katika hiyo chain. Iliwatafuna wale wazee ni balaa. Ilikuwa inadondosha mmoja baada ya mwingine.

Hii kitu hapa Mkoa wa Njombe wilaya moja inaitwa Makete! Walikuwa na michezo ya kurithi Wajane na kulana wake na waume za watu! Walipukutika balaa
 
Sio mafinga tu HIV vijijini mkoa wa mara pia napo ipo ya kutosha

Nilienda huko kwa kazi ya mkataba hii miradi ya wadau wanao support wanaoishi na HIV aisee

Nimekoma kwenda huko katu sirudii

Binafsi nimetumia pep mara 2 pia nimezika wengi tu na kushuhudia vijana wadogo sna wakiteseka na hilo gonjwa
 
Mkuu tunapozungumzia ukimwi ishu hapa sio kufa, ila ishu ni kufa na ukimwi. Mtoa mada kana sentence anasema "kama hujawahi kumuona au kuuguza mgonjwa wa ukimwi huwezi kuelewa vizuri"
Ah kama mateso mbona watu wanateseka na cancer kisukari n.k.
 
Vijana pale kati panatuita jamani acheni tuu tufe na huu utamu wa mbususu
 
Daaah [emoji25]

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…